Jinsi gani unaweza kupata talaka ya ndoa iliyo chini ya miaka miwili?

Jinsi gani unaweza kupata talaka ya ndoa iliyo chini ya miaka miwili?

unataka kuvunja ndoa ya nini?hivi wakati unaolewa ulosahau kua uliambiwa huyo ni mwenza wako wa shida na raha?

Mnang'ang'aniza muolewe haraka ili mtambe na kujisifu kwa marafiki zenu then mnalilia talaka.

Mnaboa sana madada wa kaliba yako
 
Kama ni mkristo hata ukivunja kama kosa si la uzinzi bado itahesabika ni ndoa mbinguni na ukiolewa tena utahesabika ni mzinzi pamoja na aliyekuoa

Ndoa siyo mchezo wengi huwa tunakimbilia tu pasi na kujiandaa kuhimili mikimikiki ya ndoa
 
Nifahamisheni taratibu za kufuata kwenye ndoa chini ya miaaka 2
Kama miaka miwili haijafika pia ni indicator kwamba hiyo ndoa ilikua na dosari flan from very beginning. Ukikusanya ushahidi vzur wa sababu zinazofanya utoe/uprocess talaka bas unaweza kupeleka sababu hizohizo kanisani kwako (hasa Roma) kisha ukafungua shauri la ndoa ili kanisa litamke kwamba ndoa yenu ilikua batili. Kwamba mwanandoa mwenzio hakudhamiria kudumu katika ndoa kinyume na kanisa lilivyo ielewa ndoa yenu.

Kama ukishinda shauri hilo kanisa lita-nullify ndoa yenu kwamba ni batili. Maana yake ni kwamba kama angekua ni Mungu mwenyewe aonae sirini ndiye alitakiwa kufungisha ndoa ASINGEFUNGISHA. Ila kwkua ndoa ilifungishwa na padre au kasisi yy ni binadam na ni inawezekana kwamba siku ya ndoa yenu mwanandoa mwenzako alikubali kuoana na ww mdomoni tu

Kisha ndipo ukafungue shauri la talaka mahakamani ukiwa na hukumu ya kanisa.

Talaka ikitolewa maana yake ni kwamba kanisa na mahakama vyote haviitambui ndoa yenu. Hapo utaweza tena kuoa/kuolewa kanisani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom