Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Andres

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
502
Reaction score
815
Habari wakuu

Kwa muda mrefu nimekutana na kesi mbalimbali za watu kuibiwa kwa namna ya kupumbazwa akili ( hypnosis).

Unakutana na mtu anakusalimia, ukishaitikia tu ndo kosa lako[emoji51][emoji51] .. Unakuja kushtuka ulishampa simu, wengine huenda hata bank na kutoa hela na kuwapa hao matapeli.[emoji2365] imagine enzi niko sekondari kuna classmate yeye aliwapa mpaka mkanda wake wa kiunoni manzese pale[emoji16]

Binafsi sijawahi kukutwa na hayo maswaibu, ila najiuliza ni nini kinga ya watu kama hao au hii mbinu ina Apply kwa baadhi ya watu tu ?

--
Pia soma >Kuna ukweli wowote katika aina hii ya utapeli?
 
ilinikuta hii mzee dodoma hapo nilipigwa beg lina pc, modem, dawa za maza na tsh 200k tena nilimpigia manzi angu anitumie kabisa (majobles) pc manzi aliinunua haina hata mwezi
 
Unakutana na mtu anakusalimia, ukishaitikia tu ndo kosa lako[emoji51][emoji51] .. Unakuja kushtuka ulishampa simu, wengine huenda hata bank na kutoa hela na kuwapa hao matapeli.[emoji2365] imagine enzi niko sekondari kuna classmate yeye aliwapa mpaka mkanda wake wa kiunoni manzese pale[emoji16]
Hii imewakuta watu watatu tofauti ninaowafahamu sijui hawa wezi wanatumia dawa gani

Wa kwanza; Huyu yeye alizubaishwa Mwenge na akawapa kiasi cha pesa alichokuwa nacho pale, akaja nao mpaka anapoishi huko Skanska akawapatia Akiba, kama haitoshi akakopa kwa jirani akawapatia, akakopa kwa ndugu pia akawapatia. Baada ya jamaa kusepa ndo anakuja kustuka baada ya kuongeleshwa, ilikuwa kilio kuanza kulipa madeni.

Wa pili ni huko Bonyokwa, huyu dada yeye alipumbazwa akawapatia simu, pesa na bado akaenda nao kwake akaanza kuwapa vitu vya ndani. Majirani walipomuuliza mama fulani unahama? Fahamu zikamrudia jamaa hapo washasepa fasta.

Wa tatu ni mdada wangu wa kazi; na akaambiwa mambo ya nyota, pia akaambiwa ndani una akiba ya fedha akajibu ndiyo. Alikuwa na simu lakini hakuwapa na wala hawakuongozana but alivyofika nyumbani akaenda kukoga na simu aliweka kitandani but alivyotoka kuoga akakuta bahasha, kufungua akakuta mche wa sabuni, ile akiba nayo imetoweka. Kilio chake hakikuwa cha nchi hii ikabidi tu nimpatie simu na akiba yake.

Kwa haya mafunzo, wapendwa tuwe makini. Najua si rahisi kutomwongelesha mtu lakini tujitahidi kuepuka mitego ya namna hii.
 
Sasa bwana Yuda, ina maana unatakuwa uwe na principal ya kutokuangalia watu usoni na kutowasikiliza ? Utachujaje sasa mkuu
Umeshaambiwa potezea mtu anayejaribu kuanzisha na wewe maongezi na huna idea kama unafahamiana naye au umewahi kukutana naye sehemu, hasa hisia zako zinapokutuma hivyo potezea wala usifikirie mara mbili......
 
ilinikuta hii mzee dodoma hapo nilipigwa beg lina pc, modem, dawa za maza na tsh 200k tena nilimpigia manzi angu anitumie kabisa (majobles) pc manzi aliinunua haina hata mwezi

Dah Pole sana mkuu, wakati unampigia manzi unakumbuka ulichomwambia ?
 
Umeshaambiwa potezea mtu anayejaribu kuanzisha na wewe maongezi na huna idea kama unafahamiana naye au umewahi kukutana naye sehemu, hasa hisia zako zinapokutuma hivyo potezea wala usifikirie mara mbili......

Kitendo cha kuload na kujua kwamba huyu simfahamu maana yake si ndo ushamuangalia machoni au ? Na ukimwambia sikufahamu si ndo mmeshaongea ? Changamoto ni kujua hawa wanatumia dawa za kishirikina au ?
 
Sasa mkuu mtu kama huyo mnapokutana atakuashiria usimame ili akuulize jambo fulani au wakati mnaenda kupishana anakuwa anaongea anakupa alert kwamba anaongea na wewe, sasa ile kusimama na kumruhusu kuongea na wewe ndo hapo unapigwa lakini ukipita hivi hataendelea kukufuatilia.
 
Anhaa hapo nimekupata
 
Back
Top Bottom