Jinsi habari ya gazeti ilivyopelekea majengo na ardhi ya Guardian Mikocheni yenye thamani ya 6.2B kupigwa mnada

Jinsi habari ya gazeti ilivyopelekea majengo na ardhi ya Guardian Mikocheni yenye thamani ya 6.2B kupigwa mnada

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
1787139553488.png

​
Mwaka 2001, Justin Nyari hakukubaliana na habari iliyochapishwa katika gazeti la Financial Times. Habari hiyo ilimhusisha na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kuwa kiongozi wa kundi lisilo na sheria, mshirika wa kampeni dhidi ya AFGEM, msaliti wa wachimbaji wadogo na mtu aliyehongwa.

Akaamua kwenda mahakamani na kuishtaki Guardian Limited pamoja na Printer Afrique Limited kwa kosa la uchafuzi wa jina (defamation). Kesi hiyo ilienda katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Arusha, ikiwa ni Civil Case No. 35 of 2001.

Nyari aliomba alipwe shilingi milioni 200 kama fidia kwa madhara aliyoyapata.

Mahakama Kuu iliposikiliza kesi hiyo, ilikubaliana na Nyari kwamba yaliyokuwa yamechapishwa yalikuwa ya uongo, ya kumdhalilisha na yaliyochapishwa kwa nia ovu. Hata hivyo, Mahakama haikuishia kwenye milioni 200 alizoomba. Badala yake, iliamua kumpa Nyari shilingi milioni 350 pamoja na riba ya asilimia 12 kwa mwaka.

Sababu iliyotumika kuongeza kiasi hicho ilikuwa, miongoni mwa mambo mengine, mabadiliko ya thamani ya fedha kutokana na mfumuko wa bei.

Guadian na Printer Afrique hawakuridhika na uamuzi huo. Wakaamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Mwaka 2024, Mahakama ya Rufani ilitoa uamuzi katika Civil Appeal No. 187 of 2020, tarehe 6 Februari 2024.

Mahakama ya Rufani ilikubaliana kwamba Nyari alikuwa amedhalilishwa na kwamba alikuwa na haki ya fidia. Lakini haikukubaliana na namna Mahakama Kuu ilivyofikia kiasi cha milioni 350.

Mahakama ya Rufani ikaona kwamba hakukuwa na msingi wa kutosha wa kutumia mfumuko wa bei kuongeza fidia kutoka milioni 200 hadi milioni 350, hasa kwa sababu suala hilo halikuwa limewasilishwa na kuthibitishwa kwa ushahidi unaofaa.

Kwa hiyo, Mahakama ya Rufani ikapunguza fidia kutoka TZS 350 milioni hadi TZS 200 milioni. Pia ikabadilisha riba. Badala ya 12%, ikaweka 7% kwa mwaka, kuanzia tarehe ya hukumu.

Kwa hiyo, baada ya rufaa, deni la hukumu likawa TZS 200,000,000 + riba ya 7% kwa mwaka.

Baada ya uamuzi huo, kulikuwa na suala la utekelezaji wa hukumu. Wakati wa kuhesabu kiasi ambacho Guardian na Printer Afrique walipaswa kulipa, kiasi kilichodaiwa kilifika takribani TZS 410 milioni.

Wadaiwa walipinga namna kiasi hicho kilivyohesabiwa. Mzozo mwingine ukazuka kuhusu mali iliyokuwa imekamatwa kwa ajili ya kulipa deni hilo, Guadian wakidai mali iliyokamatwa ina thamani kubwa sana kulinganisha na deni. Mali hiyo ilikuwa Plot No. 122, ambayo ilithaminiwa kuwa na thamani ya takribani TZS 6.2 bilioni. Wadaiwa waliomba mali iliyokamatwa(attachment) iondolewe.

Lakini Mahakama Kuu katika kesi ya mwaka 2026 ikawa na tatizo moja muhimu, haikuwa inasikiliza upya kesi ya defamation. Ilikuwa inatekeleza tu hukumu iliyotokana na uamuzi wa Mahakama ya Rufani.

Kwa hiyo, Mahakama ikasema kwa msingi kwamba ikiwa kuna tatizo katika namna hukumu ilivyotolewa, kutafsiriwa au kiasi cha riba kilivyohesabiwa, hilo si jambo ambalo Mahakama hiyo ya utekelezaji inaweza kulibadilisha kirahisi. Inapaswa kushughulikiwa na mahakama yenye mamlaka husika.

Dalali wa mahakama, Majembe wametangaza kufanya mnada wa mali husika September 25, 2026. Eneo la Guardian limeongozana na zilipo studio za ITV/Radio one.
 
Hivi vi online tv kuna kitu cha kujifunza hapa. Huwa wanatoa habari za uongo na nyingine zinadhalilisha huko youtube mpaka unashika mdomo kwa mshangao. Siku wakiingia kingi kwa mtu mtata hao wamiliki na watangazaji wa hizo online tv watafilisiwa mpaka boxer.
 
Back
Top Bottom