Ray J Enterprise
Member
- Jul 18, 2022
- 49
- 57
UTANGULIZI
Migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo vijijini na mahusiano baina ya wakulima na wafugaji katika nchi nyingi zilizo katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara. Pamoja na kuwa na juhudi za maksudi za kutatua migogoro hii bado kumekuwa na kukosekana kwa suluhisho la kudumu.
Kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo na mifugo imekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wake ambapo wahusika wamekuwa wakipuuzia kutekeleza utaratibu huu. Mifugo imekuwa ikizagaa na kuharibu mazao ya wakulima na wakati mwingine wakulima kulima eneo la mifugo. Kwa ufupi hii imekuwa ikipelekea migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi hususani nchini Tanzania. Migogoro hii imekuwa ikipelekea mapigano kati ya wakulima na wafugaji na hivyo kupoteza maisha ya watu.
JINSI HARUFU YA SIMBA INAVYOWEZA KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI
Baada ya kuhitimu masomo ya shahada ya kwanza nilijikita katika kilimo cha nyanya, vitunguu na mboga mboga (bustani). Katika maisha yangu ya kilimo nilikutana na changamoto ya mifugo kuingia katika bustani yangu na mara nyingi nilipata hasara. Tatizo hili halikunikuta mimi tu isipokuwa wakulima wengi walikutwa na changamoto hii. Ng’ombe kwa asilimia kubwa ndio walikuwa waharibifu wakubwa kwa kuwa wako kwa wingi sana. Nilitengeneza uzio wa miti na muda mwingine kulazimika kushinda shambani kuwa mlinzi na muda ambao nilikuwa sipo shambani uharibifu ulitokea.
Nilimuuliza mzee mmoja, ni kitu gani ambacho ng’ombe hukiogopa na asiweze kusogea eneo husika kilipo hicho kitu? Lengo lilikuwa ni kujaribu kukomesha mifugo - ng’ombe wasiendelee kufanya uharibifu shambani kwangu. Yule mzee akasema ng’ombe anaogopa sana simba na fisi. Nikamuuliza kwa hiyo nikimweka simba anilindie shamba langu sitapata hasara tena ya mifugo kulisha shambani? Akasema, ndio. Lakini nilijiuliza maswali naweza nikampata simba nimuweke kila eneo? Na je atakaa?
Na kama akikaa nitamlisha nini? Na atatulia eneo moja kama sanamu? Nikaona kumbe kuna kitu cha ziada kinachopaswa kufanyika. Nikajiuliza, kama tunatumia viuatilifu mashambani kwetu kuua/kufukuza wadudu waharibifu shambani kumbe hata hawa wanyama waharibifu wanaweza kufukuzwa pia. Nilikumbuka mwaka 2012 kuna utafiti ulifanywa na chuo cha SUA kutumia mkojo wa paka kutumika kama kiuatilifu cha kufukuza panya shambani. Katika utafiti huo watafiti wa masuala ya kilimo na ikolojia ya panya walibaini kwamba mkojo wa paka unaweza kutumika kufukuza panya majumbani na mashambani bila kuwaua.
Nikaona kuna uwezekano wa kuwa na kiuatilifu (cattle repellent) cha kufukuza mifugo shambani hususani ng’ombe bila kuwadhuru kama ilivyo kwa panya. Nilianza kufanya utafiti kwa kuwatembelea maafisa kilimo, mifugo, wanaikolojia wa wanyama pamoja na wafugaji ili kujua tabia za wanyama hawa na kitu wanachoogopa hususani ng’ombe.
Katika utafiti wangu nilibaini kuwa mnyama SIMBA anaogopwa sana na ng’ombe na akiwa katika eneo hilo yeye au harufu yake basi ng’ombe hawezi kusogea eneo hilo. Kwa mfano katika jamii ya kimasai wakulima huweka ngozi ya SIMBA dume ili kuzuia mifugo isiingie shambani kutokana na maumbile ya kimofolojia SIMBA dume ambaye ana harufu kali sana.
Jamii zingine kama Wasukuma hutumia mafuta ya SIMBA kuweka mashambani mwao mbayo pia hutoa harufu ya SIMBA na mifugo huhisi kuwa SIMBA yuko eneo hilo. Hivyo kama harufu yake itapulizwa katika eneo la shamba itasaidia kuzuia/kufukuza wanyama waharibifu shambani wakinusa harufu wakidhani SIMBA yuko shambani.
NINI KIFANYIKE ILI KUPATA HARUFU YA SIMBA?
Utafiti wa kimaabara ufanyike kupata viini vilivyoko kwenye mafuta au mkojo wa SIMBA ili kutengeneza harufu ambayo itawafanya ng’ombe wakinusa wakimbie na kutorudi tena wakihisi SIMBA yuko shambani. Utafiti huu ukikamilika na kiuatilifu kikatengenezwa, kutakuwa na suluhisho zuri kwa asilimia 100 ambalo litatumika kufukuza wanyama waharibifu wavamiao mashamba na kupelekea migogoro ya wakulima na wafugaji. Kiuatilifu hiki kitamsaidia mkulima kufukuza wanyama na kuondoa uharibifu kwa kuwa wanaopata adha kubwa ya wanyama hawa ni wakulima.
WAZO HILI LITASAIDIA KATIKA MAMBO YAFUATAYO
Kutokomeza njaa kwa kuwa kutakuwa hakuna uharibifu wowote wa mazao na wakulima kuvuna mazao kama ilivyotarajiwa.
Kupunguza kiwango cha umaskini. Kutokana na uharibifu ambao umekuwa ukifanywa na mifugo mashambani wakulima wengi wamekuwa wakipata hasara mara kwa mara na hivyo mitaji yao kupotea na hatimaye kujikuta katika wakati mgumu kiuchumi. Kwa ubunifu huu wakulima watawekeza bila hofu ya kupoteza mitaji yao.
Afya njema na utulivu. Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini imepelekea vifo na ulemavu wa kudumu kwa baadhi ya wananchi. Kupitia ubunifu huu amabo unaenda kutatua kadhia hii ya migogoro itapelekea wananchi kuishi kwa amani na utulivu huku wakiwa na afya njema.
Usawa wa kijinsia. Katika migogoro yoyote ile ya kijamii, kiuchumi, siasa na kidini waathirika wakubwa huwa ni wanawake, watoto na walemavu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa wanaonekana ni kundi la wanyonge ambao hawawezi kujitetea hususani kukimbia. Kwa muktadha huo, ubunifu huu utaenda kurejesha usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake pamoja na makundi maalumu ambayo yamekuwa waathirika wakubwa wa kadhia za migogoro.
Utunzaji wa mazingira
Itakumbukwa kuwa kumekuwa na jitihada za kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji. Lengo ni kuepusha muingiliano wa kila kundi. Hii ilienda sambamba na kudhibiti ufugaji holera wa mifugo kwenye vyanzo vya maji kama mito, maziwa na mabwa pamoja na uhifadhi wa miti ambayo huvuta mvua na kutunza maji. Katika hali hii ilikuwa ni vigumu kufikia malengo haya kutokana na aina ya ufugaji tulionao Tanzania. Wazo hili litakuwa sehemu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa kuwa mifugo haitaweza kufanya uharibifu katika maeneo ambayo siyo sahihi kwa malisho.
Kupunguza tofauti katika jamii. Migogoro ya wakulima na wafugaji imetengeneza matabaka makuu mawili ambayo ni wakulima na wafugaji. Katika makundi haya kila kundi linajiona ni bora kuliko lingine. Hali hii inaenda kutoweka kwa kuweka usawa katika jamii.
Jamii endelevu. Ni vigumu kuwa na jamii endelevu ikiwa kuna makundi yanayokinzana. Kupitia wazo hili jamii endelevu itapatikana kwa kuwa hakutakuwa na makundi yenye uhasimu na kukamiana. Pia itachochea ushirikiano wa taasisi na watu binafsi katika kufanikisha malengo ya pamoja kwa kuwa kutakuwa hakuna uhasimu wowote kati ya taasisi za wakulima na zile za wafugaji.
Uzalishaji wenye kuwajibika. Katika wazo hili kila mtu atawajibika kulingana na nafasi yake. Na asiyewajibika atalazimishwa kuwajibika kulingana na mazingira. Mfano mfugaji amepuuzia majukumu yake ya kuangalia mifugo yake itazuiliwa kuingia eneo lisilotakiwa (shamba) kupitia kiuatilifu hiki.

Upvote
7