Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 673
- 865
Mwaka 2011 nilipewa kazi ya kutafuta almasi na kumtumia mfanyabiashara mmoja wa Ulaya. Katika harakati za kutimiza jukumu hilo nikajikuta nalazimika kwenda nchini Namibia ambako kuna wauzaji wa almasi ambao mfanyabiashara huyo alikuwa ameshaonana nao na akanituma nikakague almasi zao na kuzichukua kama ziko vizuri.
Pichani chini wa mwisho kwenye ngazi ndo mimi nikipanda ndege kuelekea Windhoek.
View attachment 2301283
Mfanyabiashara wa Ulaya kuna mambo yalikuwa yanambana kwa yeye mwenyewe kwenda Namibia kuchukua mzigo huo. Ilikuwa ni vema akituma mtu kuliko kwenda yeye mwenyewe.
Katika safari hiyo niliongozana na mtaalam wa madini mTanzania mwenzangu ili akanisaidie kukagua na kuthaminisha hizo almasi. Mie nilikuwa nimepata mchongo tu, ila sina utaalam wa kukagua madini.
Jijini Windhoek tulipokelewa vizuri na wenyeji watu (ambao ndo hao wauza almasi) wakatupeleka hotelini. Ratiba ilikuwa ni ya kukaa siku tatu.
Siku ya kwanza tulifika na kumpumzika.
Siku ya pili asubuhi mtaalam wangu akampigia simu rafiki yake mmoja ambaye ni Afisa wa madini serikali ya Namibia kumsalimia na kumjulisha kuwa yupo Windhoek mara moja ikiwezekana wakutane. Akamwambia na kilichotuleta.
Rafiki yake akashtuka. Akamwambia amtumie leseni ya hao wauza almasi. Tukawaomba watutumie leseni yao wakatutumia kwa barua-pepe. Yule Afisa wa Namibia alipoipata akasema hiyo ni leseni ya kughushi hao watu ni matapeli.
Basi mpaka hapo tukakubaliana na mtaalam wangu kuwa hao jamaa tusihangaike nao. Tuwazuge tu (kwamba pesa za kulipia mzigo zimekwama benki tunazisubiria) ili siku hiyo ipite kesho yake turudi Dar es Salaam.
Mfanyabiashara wa Ulaya nikamtaarifu ili ajue kinachoendelea kama wakimtafuta moja kwa moja awape stori hiyohiyo.
Wale wauzaji wa almasi wakaja pale hotelini kwenye saa tano asubuhi. Wawili wakaingia ndani chumbani, na mmoja (dereva) alibaki nje. Wakauliza vipi biashara tunafanya saa ngapi na malipo yatakuwaje.
Nikawaeleza kuwa pesa imekwama benki.
Wakaonesha wasiwasi na kauli yangu, maana walikuwa wameshaongea na mfanyabiashara wa Ulaya kwamba malipo yatakuwa kwa pesa taslimu mkononi. Sio kupitia akaunti za benki.
Na mie nikajiongeza kwamba benki sio kwenye akaunti, bali ni kupitia MoneyGram. Kwa hiyo nitatoa pesa taslimu MoneyGram na kuwapatia zikishakuwa tayari.
Wakabaki na nyuso za wasiwasi, lakini wakasema sawa, ikiwa tayari niwatushtue. Wakauliza inaweza ikachukua muda gani? Nikawaambia inategemea na Mfanyabiashara wa Ulaya atamalizana saa ngapi na benki yake.
Basi nikaona niitumie hiyo siku kutalii katika jiji la Windhoek. Mwenzangu (mtaalam) yeye akasema atapumzika tu hapo hotelini hajisikii kuzurura.
Nikakodi gari kunizungusha Windhoek. Nikamilizia utalii katika jumba la sinema.
Sinema ikaisha saa moja usiku. Nikarudi hotelini. Kufika nakuta gari la Polisi liko nje ya hoteli pamoja na gari lile la wauza madini. Teksi yangu ikawekwa kizuizini na mapolisi wawili mmoja akanitoa kwenye teksi na kunifunga pingu huku askari mwingine akipiga picha za kutosha za tukio zima kwa kamera kubwa ya kikazi, maflashi yakinimulika usoni na kuniumiza macho.
Nikapelekwa kwenye gari la Polisi, kuingia ndani namkuta mtaalam wangu na yeye yupo humo mikono nyuma ikiwa imepigwa pingu kama ya kwangu.
Kiukweli nilichanganyikiwa.
Nikamuuliza mtaalam wangu vipi imekuwaje tena?
Akaniambia hao wauza madini walikuja jioni kama nusu saa iliyopita wakaingia chumbani kwetu (tulikuwa tumechukua chumba kimoja chenye vitanda viwili) na kumdhibiti. Wakapekua chumba na kuchukua vijisenti tulivyokuwa navyo, halafu wakaita Polisi ndo wamemkamata.
Hatukuongea sana Polisi wakawasha gari na kuondoka. Gari la wauza almasi likatufuata kwa nyuma.
Tulitembea kwa mwendo wa wastani kama nusu saa hivi mpaka nje ya jiji la Windhoek ambako kuna kiza kinene nyika tupu. Njiani askari walikuwa wakituhoji.
Kwenye upekuzi wao mle chumbani walikuwa wameshakamata zana zote za kazi alizokuja nazo mtaalam. Katika zana hizo ilikuwepo chupa moja ya tindikali nzito aina ya naitriki kwa ajili ya kupima dhahabu, maana hao wauza almasi walisema pia na dhahabu pia wanayo.
Nikawaeleza kwamba tumekuja kwa ajili ya kununua almasi na dhahabu, kwa hiyo vifaa vyote walivyovikamata ni kwa ajili ya lengo hilo tu na sio jingine.
Wakatuambia kwamba wao waliitwa kuja kutukamata kwamba tumeficha almasi za magendo. Kumbe nilipoondoka pale hotelini kwenda kutalii wale wauza almasi walikuwa wameacha mpelelezi wao kwenye mgahawa wa ile hoteli akawapa taarifa kuwa nimetoka na akanifuatilia kwa nyuma. Alipoona naingia kwenye shopping mall akawaambia kuwa nimeshapokea hela MoneyGram na nimeenda kununua almasi sehemu nyingine.
Kwa sheria za Namibia ni marufuku kuwa na almasi ghafi mkononi bila leseni ya serikali. Wakasema pia hata tindikali ya naitriki tuliyokutwa nayo ni kosa kisheria kuwa nayo bila ya kibali.
Wakasema pia watu tunaodili nao sio watu sahihi maana hawana leseni ya biashara ya madini.
Nikaomba msamaha na kuwaeleza mkanda kamili kuwa sisi tulitumwa tu na mfanyabiashara mmoja aliyeko Ulaya ndo maana hatukuhangaika sana kuchunguza mambo yote hayo. Tuliamini kwamba yeye amesharidhika na watu aliokutana nao, na kwa kuwa pesa ni ya kwake hatukuona haja ya kuhoji sana. Kwamba machale yalitucheza baada ya kuwa tumeshafika Windhoek.
Tukawa tumefika huko porini tukachepuka kutoka kwenye lami na kuingia njia ya vumbi. Wakaegesha gari.
Tukiwa pale wakatuambia maneno ambayo mpaka leo sitayasahau.
Wakasema kwamba tumeusikia mkasa wenu na leo ilikuwa mkalale Polisi, kesho ndo suala lenu lishughulikiwe. Ila sisi waNamibia hususani katika kada za majeshi tunawaheshimu sana waTanzania kwa sababu ya Nyerere alivyoongoza harakati za ukombozi wa nchi yetu. Watanzania mlitusaidia kupata uhuru. Pale hotelini kwenye daftari la wageni tulipoona tu kuwa nyie ni waTanzania tulikwishawasamehe.
Kwa maneno hayo wasiwasi ukanitoka. Nikajua kesho nitarudi nyumbani Dar.
Askari wawili wakashuka na kwenda kuongea na wale wauza madini. Maongezi hayakuwa marefu sana wauza madini wakawasha gari na kuondoka zao.
Wale Polisi wakaturudisha hadi hotelini na njiani wakatuagiza kuwa tuondoke mara moja kurudi Tanzania, na kama tunataka kuja kununua madini nchini humo madini yapo ila tukanunue kwa wauzaji wanaotambulika serikalini.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimefarijika sana kwa jinsi jina zuri alilotujengea Mwalimu Nyerere kama taifa la waTanzania lilivyonisaidia miaka 12 baada ya kifo chake. Na kwamba ni muhimu kiasi gani katika maisha kujenga na kuacha jina zuri.
Mwaka 2019 serikali ya Namibia ilimuenzi hayati Mwalimu Nyerere kwa kumpa mtaa wa maana wenye jina lake. Mtaa huo yako makao makuu ya Polisi Namibia pamoja na ofisi zingine za serikali.
View attachment 2301286
Katika uzinduzi huo Rais wa Namibia alisema, "Mapenzi ya waNamibia kwa Nyerere yana mizizi mirefu. Ni mapenzi ambayo yamejikita katika chimbuko la taifa letu wakati wa harakati za kupigania uhuru."

Upvote
8