Bunchari
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 558
- 661
Habari wakuu
Katika pilika pilika za kutafuta ajira,nilijaribu kutuma maombi taasisi fulani ,mchakato wa maombi ulipokamilika nikapigiwa simu na hr nimekua selected hivyo niende kuonana naye.
Nilipofika ofisini kwake,akaniagiza siku inayofuata niende na watu watakao nidhamini niliitikia wito nikawachukua jamaa tukaenda, akanielekeza majukumu,mshahara utakua kiasi gani na mambo mengine ya kazi kisha akanielekeza niende nitapigiwa simu siku ya kuja kuanza kazi rasmi nikaitikia sawa kisha nikaondoka.
Nimekaa karibu mwezi mzima pasipokupokea simu toka kwa HR au mwakilishi yoyote toka ile ofisi nikapata wasiwasi labda nimesahaulika ikabidi niende kuulizia nilipofika nikasalimiana kidogo na mlinzi katika mazungumzo akaniambia mbona wenzako wameishaanza kazi kitambo, kiukweli nimejiskia vibaya nikaamua kuingia ndani ili kujiridhisha kama ni kweli nikakuta jamaa hayupo ofisi imefungwa sikupata majibu.
Ikabidi nikae chini najiuliza maswali,lengo la HR kufanya hivi ni nini mbona kanifedhehesha vibaya si angenipotezea wakati wa selection tusingefikishana huku.
Daah hii dunia hii