Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nakumbuka Kwenye ule mwaka wa mwanzoni ya 2000, aliyekuwa IGP wa wakati ule, Omari Mahita, alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kudai kuwa wamekamata "container" lenye visu vya chama Cha CUF, ambavyo vimepakwa rangi za bendera ya Chama Chao, ambazo alidai kuwa chama hicho Cha CUF kilikuwa na mpango wa kuliingiza nchi hii Kwenye machafuko!
Hata hivyo baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka huo wa 2000, hiyo story ya hivyo visu, ilikufa ghafla na Wala sikusikia tena mwendelezo wake!
Nikukumbushe kuwa nyakati hizo chama Cha CUF na msemo wao maarufu wa wakati huo wa "ngangari" ndicho kilichokuwa chama kikuu Cha upinzani nchini.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa tunafahamu kuwa Kila inapokaribia uchaguzi Mkuu, basi homa huwa inapanda na Kwa chama Tawala Cha CCM, huwa kinatumia hata njia "haramu" za kuvisingizia, hususani chama kikuu Cha upinzani Cha wakati huo, shutuma nzito.
Ndicho ninachokiona wakati huu, ambapo Jeshi la Polisi, limeendelea kukiandama chama kikuu Cha upinzani Kwa wakati huu Cha Chadema Kwa tuhuma mbalimbali.
Mlishuhudia wenyewe namna Jeshi la Polisi lilivyovuruga na kuwapiga viongozi wa Chadema, Hadi wengine kuwaumiza na kulazwa hospitalini.
Jeshi la Polisi pia linatuhumiwa kumteka kiongozi wa Chadema, Soka na wenzie.
Pia linatuhumiwa kumteka kiongozi wa Chadema, Mkoani Tanga, Kombo Mbwana.
Kwa matukiu ya aina hii, Jeshi la Polisi, lisidhani kuwa ndiyo linakisaidia chama Tawala Cha CCM na badala yake ndiyo wanakipotezea umaarufu Kwa Kasi kubwa!
Kuna msemo wa Kiswahili unaosema kuwa mti wenye matunda mazuri, hauishi kupopolewa mawe!