Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,503
MVURUGANO mkubwa ulizuka katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya wajumbe wanaomuunga mkono Edward Lowassa, kubaini jina lake limekatwa.
Hali ilikuwa hivyo baada ya majina matano ya watangaza nia kutoka Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwasilishwa katika Kamati Kuu.
Majina hayo matano ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na Balozi Amina Salum Ally.
Watetezi wa Lowassa waliongozwa na Dk. Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, Meya wa Ilala, Jerry Silaa, Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Khamis.
Aliyeanza kuhoji viongozi wa Kamati Kuu kuhusu kufyekwa kwa majina mengine ya watangaza nia, akiwamo Lowassa alikuwa Nchimbi ambaye kama wenzake hao, alitaka kujua sababu za kuenguliwa watangaza nia wengine.
Kundi hilo lilidai kwamba hakuna sababu nzito zilizotumika kuwangoa watangaza nia wengine na kama hoja ni tuhuma za ufisadi, hiyo ni hoja isiyokuwa na nguvu, kwa mujibu wa mtazamo wao.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu kilichoketi mjini Dodoma, zinaeleza kwamba safu hiyo ya watetezi wa Lowassa ilikuwa ikipeana pasi kujenga hoja za kushinikiza kuongezwa kwa majina mengine mbali na hayo matano ili yafanyiwe kazi na kikao hicho.
Alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM, Abdallah Bulembo ndiye aliyeingilia kati na kuwataka akina Nchimbi kuheshimu viongozi wakuu waliokuwamo kwenye kikao hicho, akipinga hali iliyokuwa ikijitokeza ya kujadili suala hilo kwa njia ya kejeli.
Watu waheshimu viongozi waliomo humu ndani. Tunao viongozi humu wametumikia Taifa kwa juhudi na umakini mkubwa, wanaheshimika nasi lazima tuwaheshimu na tuheshimu uamuzi uliofikiwa ambao umeshirikisha hawa viongozi wetu (kwenye Kamati ya Usalama na Maadili), alisema Bulembo ambaye alikuwa akitetea majina matano bora ya watangaza nia wa CCM.
Baada ya Bulembo, alifuatia Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye alifikia hatua ya kumtaja baba yake mzazi, Moses Nnauye aliyekuwa kada mhamasishaji kindakindaki wa CCM kwa miaka mingi chini ya uenyekiti wa Mwalimu Julius Nyerere na baadaye Ali Hassan Mwinyi.
Taifa hili linahitaji kuongozwa kwa umakini na watu makini. Taifa linahitaji umakini na busara ya hali ya juu. Tusikubali hata kidogo kuruhusu Kamati Kuu ya Chama hiki ibariki mchezo wa kununua uongozi. Si busara kwa Kamati Kuu kuwa chanzo cha kuruhusu watu kununua madaraka. Lazima kubadilisha mfumo. Tukiruhusu hali hii, masikini hawatakuwa na chao, hawatapata nafasi na sisi wengine tusio na fedha za kununua madaraka itabidi tuondoke humu.
Inasikitisha watu wapo tayari humu ndani (Kamati Kuu) kutetea ununuzi wa madaraka. Mimi baba yangu (Mzee Moses Nnauye) amefanya kazi kwenye hiki chama kwa uaminifu mkubwa, kwa miaka mingi hadi anaondoka hakuwahi hata kuwa na nyumba, leo watu wananunua uongozi, wengine siku mbili tatu baada ya kupata madaraka ana nyumba nyingi, alisema Nape.
Baada ya Nape, alizungumza Zakhia Meghji ambaye kwa ukali aliwataka wajumbe wa Kamati Kuu kuheshimu uamuzi wa Kamati ya Usalama na Maadili akisema imeongozwa na Mwenyekiti Kikwete ambaye kwa nafasi yake ya Urais, anazo taarifa za kina kuhusu watangaza nia wote.
Kamati Kuu lazima iwe na ujasiri. Mwenyekiti anazo taarifa zote tena za kina, kwa hiyo lazima wanazo sababu za msingi za kuleta humu majina matano, alisema Meghji kwa mujibu wa nukuu ya chanzo chetu cha habari kutoka kikaoni humo.
Rais msitaafu Benjamin Mkapa naye alizungumza kwa ukali akisema; Tunapata wapi ujasiri wa namna hii wa kutetea maslahi binafsi? Naona hapa ni mtu kwanza chama baadaye, si chama kwanza mtu baadaye. Hapa hakuna mwenye taarifa za kina kama Mwenyekiti. Ni nani huyo mwenye taarifa za kina kumshinda Mwenyekiti? Tuna imani na uamuzi wa Kamati ya Maadili.
Naye Mzee Mwinyi alisema; Ni lazima tuheshimu kiti. Lazima muwe na uwezo wa kukubaliana na mambo yanavyokwenda. Nashangaa watu wapo tayari kukitishia chama, nguvu hizi za kukitisha chama mnazitoa wapi?
Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, yeye alitoa mfano wake mwenyewe namna Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alivyomwondoa kwenye kinyanganyiro cha urais mwaka 1995.
Lazima tuheshimu mamlaka, Mwenyekiti anazo taarifa nyingi. Mimi mwaka 1995 Mwalimu Nyerere aliningoa na akasema kama nitapewa nafasi CCM yeye ataondoka, anakwenda kuanzisha chama. Mimi nikanyoosha mikono na kujitoa, Mwalimu akanifuata na kunikumbatia, alisema Malecela ambaye alikuwa akisisitiza wajumbe wenzake wakubaliane na hali halisi.
Mzee Malecela ambaye alikuwa nje ya nchi kwa matibabu, alilazimika kutopumzika ili kuungana na wazee wenzake kuokoa jahazi lililoelekea kuzamishwa na nguvu ya fedha.
Rais msitaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kama ilivyokuwa kwa wenzake, naye aliweka bayana kuunga mkono uamuzi wa Kamati ya Usalama na Maadili akisema ni uamuzi uliopaswa kuungwa mkono.
Baada ya jina lake kutofikishwa Kamati Kuu na baadaye kushindwa kuilazimisha jina lake lirudishwe NEC, wapambe wa Lowassa wanadaiwa kuandaa mpango wa kutaka kumsaidia Balozi Amina aweze kupitishwa kuwa mgombea wa urais wa CCM, ili naye baadaye amtangaze Lowassa kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye aweze kuwa Makamu wa Rais.
Mkakati huo ulitiwa nguvu na Balozi Amina mwenyewe wakati akijieleza kuomba kura ambaye mara mbili alisema kwamba alikuwa tayari kufanya kazi na Lowassa.
Hata hivyo, habari zinasema mpango huo ulikuja kuvuja kutokana na papara za baadhi ya wapenzi wa Lowassa kuanza kampeni za wazi kwa ajili hiyo katika Mkutano Mkuu ili Balozi Amina ashinde kwa kura nyingi.
Kwa hisani ya RaiaMwema.