Elections 2015 Jinsi jina la Edward Lowassa lilivyokatwa Kamati ya Maadili CCM

Elections 2015 Jinsi jina la Edward Lowassa lilivyokatwa Kamati ya Maadili CCM

Kama chama kinakiuka kanuni nq taratibu,tena chama tawala,wanatoa taswira gani kwa wananchi ambao kwa namnamoja au nyingine wanaamini chama cha kijani kinaviongozi ambao wakipewa madaraka wanatabia ya kukiuka sheria na kanuni zilizotungwana bunge la JMT bila sababu za msingi... kama ambavyo wameweza kukiuka taratibu katika mchakato wa kumpata mpeperusha bendera ya urais,baadhi ya viongozi wanaokiuka taratibu na sheria za nchi ni kama waziri mkuu Pinda hasa pale alipotamka WAPIGWE TU.Japo madhara ya EL yanawezakuwa underestimated lakini yanawezakuwa makubwa kuliko ilivyo na inavyotarajiwa,leo hii nani alitegemea mtu kama James Lembeli anawezahamia CHADEMA... ngoja tuone mustakabali wa hili saga.
 
Safi sana ccm. Lasivyo yangekuwa mashindano ya nani ana hela nyingi.
 
Upo OUTDATED wewe, mambo yanatokea kila kona ya nchi wewe unasema tutasubiri sana?
Woe to you....!!!
Dada, acha kelele. Hakuna kinachoendelea isipokuwa simulation za huyo aliyechinjiwa baharini. Punguza kuangalia Bongo muvi upate akili
 
Ukiangalia hizo narration ni uhakika kuwa hata zingepigwa kura kamati kuu huyu Edward Lowassa asingeweza kupita kwani ni wazi wazee wa chama na kamati kuu hawakuwa naye. Kina Nchimbi, Sofia Simba, Kimbisa na Jerry Slaa hawakuwa na nguvu au uwingi wa kutosha kumpitisha. Hata hivyo CCM imekiuka kanuni zake mara nyingi sana nanyi wote mnajua jinsi Malecela alivyoondolewa 1995. Tena wote mnajua jinsi mlivyocheza rafu 2005 ktk kumpitisha mwenyekiti wa sasa.

Inatakiwa mjue (wale mnaolalamikia Lowasa kukatwa) kuwa haya mnayopata ni malipo kwa madhambi yenu mliyoyafanya 2005. Mkiamua kuendesha chama kihuni mtarajie uhuni kutumika. Mlitumia uhuni, Hila na gilba nyingi kumpitisha mwenyekiti wa sasa. Uhuni huo huo ameutumia dhidi yenu. Malipo ni hapa hapa!! Tena bila chenji
 
Mnaacha kuzungimza ya ukawa ambao wako hotelin mpaka sasa mbazungumza yalopita na hayatabadilika ya nn sasa!!
 
Mafuriko haya yalioanza monduli na simiyu ni dhahiri nape anahali mbaya na chama ccm maana kwa kuropoka. Mafuriko hayazuiliki kabisa hata kwa ukuta wa belini
 
Jembe la kanda ya ziwa litakuja kumaliza kabisa huu upuuzi. Hii nchi inahitaji mtu kama magufuli. Tutarudi kwenye mstari wa nidhamu. Chama kitarudisha heshima yake na kuna baadhi ya wapuuzi wataozea jela.
 
mbona upande wa membe huja tuletea mkuu...au ndo kambi moja. kwa sasa tunahitaji kujua nini kilitokea membe akapata 120 na kushika mkia..mengi tume yasikia ya fisadi lowassa haya yote sio mapya na ametukifu...tuletee upande wa pili mkuu


Kama hii habari ni kweli, basi niwapongeze sana CCM angalau kwa kuthubutu kukata gogo lililojidai halikatiki!

Hakika huu ulikuwa mtihani mkubwa sana kwa CCM. Haijapata kutokea kiongozi au mwanachama akaitisha CCM kiasi hiki!

Wengi walidhani kweli hili hogo halikatwi!

CCM ingejitakia balaa huko mbele ya safari kama isingekata! Tena kwa mkato mkali!

Hongereni sana! Dawa ya kiungo kilichooza mwilini ni kukatwa! Kukiacha ni kujichulia kifo!
 
Nyoka akitaka kufa anatapatapa sana! Ufalme wa hiyo team ndo umeisha hakuna cha kupata urais wataishia kupata urahisi wa kuvurugwa tu!na this time WANAMEZWA KWA MPIGO!!Rais atatoka CCM hata wakipiga sarakasi za kuganda hewani haitawasaidia!
 
Mkuu Ng'wamapalala Unanishangaza unaposema unaipongeza ccm kwa kumkata Lowasa zaidi umejishusha thamani yako unaposema mtu hawezi kukitisha chama na unashangaza zaidi unaposema chama ndio kenye maamuzi ya mwisho.

Ashamkun si matusi, Upumbavu wako ni unaposema chama ndio kenye maamuzi ya mwisho bila kujua kuwa wanachama ndio chama chenyewe na haiwezekani KITENGO kikafanya maamuzi ya wanachama wote.

Pia hujue kuwa kamati kuu ndio chombo pekee kilichotakiwa kifanye uchujaji wa majina 38 ya watangaza nia kwa njia ya upigaji kura ili kuyapata hayo majina 5 na 3. Na badala yake kikafanyika ubatili mkuuu uliofanya ubatili wao na kuwakata watangaza nia na kumpitisha mtu wao.

Kwakuwa Makufuli kapitishwa na chama chake kwa njia ya uvunjaji wa katiba na dhuluma nyingi na yeye binafsi analijua hilo...

Je! Makufuli akiwa Raisi wa Tanzania atapata wapi ujasiri wa kusimamia katiba na kukomesha dhuluma na ubatili wakati chimbuko la uraisi wake ni Dhuluma, uvunjifu wa katiba na ubatili mtupu?
Wewe ni muongo sana!
 
Back
Top Bottom