Jinsi jinamizi la soka la kasi linavyotesa vilabu vya soka nchini Tanzania

Jinsi jinamizi la soka la kasi linavyotesa vilabu vya soka nchini Tanzania

ToniXrated

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
1,134
Reaction score
2,993
Amani iwe nanyi:

Natoa pole kwa vilabu vya Tanzania vilivyoumaliza mwendo katika mechi za awali za Mashindano ya Afrika ,nazungumzia Yanga,Azam na Kipanga.

Mara baada ya mechi za jana nilitulia kidogo kufanya tathmini kujua mapungufu ya vilabu vya Tanzania katika soka la Kimataifa, nikagundua tatizo kubwa linalotusumbua ni KASI, jinsi gani tunautembeza au kuukimbiza mpira uwanjani. Ama kwa hakika tupo (very slow) taratibu sana.

Timu za waarabu huwa zinazitesa sana timu za Tanzania kutokana na kucheza mpira wa kasi.Nimekuwa na nitaendelea kuwa muumini wa soka la kasi kwani ndio soka la nchi zilizopo ulimwengu wa kwanza kisoka.

Katika hii mechi ya Al-Akhdar dhidi ya Azam tutakuwa tumejifunza kitu kuwa wenzetu wa Afrika ya kaskazini ambao wamepakana na mataifa ya ulaya kwa kutenganishwa na bahari ya mediterrenia wamefanikiwa sana kupata chembechembe za soka la ulaya.

Kwa jinsi ya hawa Al-akhdar walivyokuwa wakicheza kwa kasi unaweza kujiuliza imekuwaje wakacheza kombe la shirikisho badala ya klabu bingwa Afrika!?

Kama Al-akhdar alimaliza ligi ya nchini Libya akiwa nafasi ya tatu ,vipi hao vinara wa nafasi ya kwanza na ya pili?!

Soka letu limebarikiwa kuwa na wachezaji ambao wana individual skills ila linapokuja suala la kasi uwanjani ,naweza kusema kwa kjnywa kipana kuwa wapo chini sana!! Work rate ya wachezaji wetu wa ligi kuu ya Tanzania ipo chini sana. Wachezaji wa Al akhdar muda wote walikuwa katika movements iwe wana mpira au hawana mpira na hivi ndivyo soka la kisasa linahitaji mchezaji awe.

Ni rahisi sana kwa wachezaji kutoka mataifa ya Afrika ya kaskazini kwenda kucheza mpira katika ligi za ulaya ,kutokana wana kasi. Mpira wa kisasa hauhitaji mambo mengi sana uwanjani. Ukiweza kucheza basic football na ukiwa na kasi basi unaweza kucheza ulaya bila ya tabu.

Wachezaji wetu huonesha movements wakiwa na mpira tu tena ni kwa baadhi , ni jambo la kawaida kuona timu inashambulia huku wachezaji wa safu ya kiungo wakiwa wapo nyuma wanatembea badala ya kukimbia. Wanapokuwa hawana mpira ndio tatizo kabisa maana huoni kujituma wala kukimbia kuhakikisha kuwa wanaumiliki mpira ama kuziba mianya .Badala yake wanatembea tu huku wakiruhusu timu pinzani ziongeze presha golini kwao.

Kama tunahitaji kufika mbali kimataifa ni lazima tubadili mfumo wetu wa uchezaji. Na kama inawezekana basi wachezaji wavishwe vifaa ambavyo vitakuwa vikionesha ni kwa umbali gani wamekimbia uwanjani , hii itawasaidia makocha katika kubadili taswira nzima ya mpira wetu.

Wenzetu huko ulaya na afrika kaskazini kwa wastani mchezaji anatakiwa akimbie sio chini ya umbali wa kilometa 9-12 kwa dakika 90 awapo uwanjani. Na viungo wa kati ndio wanaotakiwa wakimbie zaidi kuliko wachezaji wa nafasi yeyote kiwanjani.

Sasa si ajabu kuja kukuta kuwa wachezaji wetu wanakimbia umbali chini ya kilometa 4 wawapo kiwanjani ktk kipindi cha dakika 90.
 
Na ukitaka ujue Kasi hakuna angalia mechi za ndani hapa sijui ihefu anacheza na prisoni ni vituko,kifupi Mimi nasema hivi hatuna quality player Wala average player tuna low class player ambao Hawana Kasi,ubunifu Wala vision uwanjani
 
Na ukitaka ujue Kasi hakuna angalia mechi za ndani hapa sijui ihefu anacheza na prisoni ni vituko,kifupi Mimi nasema hivi hatuna quality player Wala average player tuna low class player ambao Hawana Kasi,ubunifu Wala vision uwanjani
Nasadiki haya uyanenayo!!

Al hilal walifungulia busta dk 30 za mwisho tu...ona kilichowapata YANGA. Kama sio kudra za Mungu walikuwa wanakufa goli hata 4.

Kibwana shomari ambae ndio alikuwa anasifika kwa kasi na kukaba ndio alikuwa kichochoro cha wasudan.
 
Na ukitaka ujue Kasi hakuna angalia mechi za ndani hapa sijui ihefu anacheza na prisoni ni vituko,kifupi Mimi nasema hivi hatuna quality player Wala average player tuna low class player ambao Hawana Kasi,ubunifu Wala vision uwanjani
Tutakuwa nao vipi wakati hatuna mfumo mzuri wa kuwakuza wachezaji wetu. Mbeleko mbeleko nazo zinatuchanganya
 
Kasi ambazo zipo kaskazini na ulaya nadhani ni matokeo ya malezi ya kimpira na mazoezi na vifaa sasa huku kwetu wale prison wanachojua ni kula sana na kupiga drill za kufa mtu tu mchezaji kashiba kande tumbo lote
 
Katika watubwaliokutana na timu hatari zaidi ni AZAM. Yale majamaa ysmeshiba yana kasi na vipaji vya hali ya juu.

Nilimshangaa sana Hersi kuingia kwenye mgogoro na Tff kisa tuisila. Angalau angehangaika na beki mwenye umbo na kipaji

Sijawahi kuona timu inayokomas kununua forward pekee. Kwa siku nyingi beki ya yanga ni dhaifu, wengi ni wafupi hawajui majukumi yao, wanajifanya kuwaiga mageiji akina roberto carlos waliokiwa na uwezo wa kwenda mbele na kurudi fasta. Sasa hawa mabeki wafupi kutoka mlima wa vidunda morogoro wanakwenda mbele wanaacha nafasi nyuma wanafungwa kirahisi kwa caunter attack
 
Hii kitu tunatakiwa kuanzia mbali sana. Kwanza nchi/club ziamua tunataka kucheza mpira wa kiholanzi,german France or kibrazil or hispania.

Then tuwekeze or hata wachezaji wanaonunuliwa wawe na falsafa hio.

Mfano Azam yule kocha mmaerekani alikua na falsafa ya kihisaniola. Ile process inahitaji muda nakuwe naviwanja vizuri.

Kwa mazingira ya TZ nadhani mpira wa kifaransa unatufaa zaidi.
 
Back
Top Bottom