Jinsi kamari (betting) ilivyonipotezea shilingi laki 6 ndani ya siku 60 tu

Jinsi kamari (betting) ilivyonipotezea shilingi laki 6 ndani ya siku 60 tu

Na hii shilingi laki 6 ni hesabu ndogo tu niliyoifanya katika betting zangu za mchezo wa football tena kwenye kampuni moja tu ya betting bado sijapiga hesabu ktk virtual games ambako nako nimepoteza pesa nyingi tu.

Na pia sijapiga hesabu kwenye kampuni nyingine ambazo nimeshazitumia sana kubeti ndani ya hii miezi 2.
Tafute odd 2 kila siku kwa mtaji wa 50000/= utarudisha pesa yako na faida juu
 
Sasa hv watu wanaona athari yake ni ndogo ila watu watakuja ku-realise baada ya miaka 10 ijayo vp hii industry imewaathiri wao na vizazi vyao
True mkuu.

Screenshot_20220223-235443_Chrome.jpg

QUR AN 5: 90
 
Usitupangie we umepoteza laki 6 kwa miez 2 watu tupo ndani ya hii game kwa miaka 5 na kuendelea sema kama vip niwe nakupa odds za uhakika.
Kesho tudondoshe odds 1.7 za uhakika
 
Kuna aya inasema kuwa kamari ina manufaa kwa watu ila madhara (madhambi) yake ni makubwa kuliko manufaa yake.

Yes hapa tunaona manufaa yake makubwa ni kwa bookie aliyeanzisha kampuni ya kamari. Na madhara makubwa ni wale wanaocheza kamari. 99% are loosers .
 
Usiumie mzee u achangia pato la taifa na pia sector ya michezo
Siumii kuhusu pesa cuz impact yake huwezi kuiona sasa hv .Ni mpaka ipite miezi,mwaka na miaka .Ukija kupiga hesabu ushatupa zaidi ya 50million halafu hata kibanda huna .

My biggest concern here is this addiction thing that kept building over time.

Sijui ushakutana na mraibu wa pombe ambae anasema kuwa hawezi kuacha pombe cuz hawezi kufanya ishu yoyote mpk anywe kidogo!? Sasa uraibu wa kamari nao ndio upo hivyo
 
Kuna aya inasema kuwa kamari ina manufaa kwa watu ila madhara (madhambi) yake ni makubwa kuliko manufaa yake.

Yes hapa tunaona manufaa yake makubwa ni kwa bookie aliyeanzisha kampuni ya kamari. Na madhara makubwa ni wale wanaocheza kamari. 99% are loosers .
Sijaiona. Ntaifuta mkuu niendelee kujifunza
 
Hayo maneno ya beti kistaarabu ni maneno ya kisiasa tu.Ukweli ni kwamba hakuna mwanadamu duniani anaepensa kuwa looser, haijatokea na haitatokea. Unavyozidi kucheza na kupoteza ndio hasira zinazidi kujengeka ile haiba ya furaha na uchangamfu hupotea na hayo ndio maisha ya wakamaria wengi
 
Sijaiona. Ntaifuta mkuu niendelee kujifunza
Q2:219

They ask you ˹O Prophet˺ about intoxicants and gambling. Say, “There is great evil in both, as well as some benefit for people—but the evil outweighs the benefit.” They ˹also˺ ask you ˹O Prophet˺ what they should donate. Say, “Whatever you can spare.” This is how Allah makes His revelations clear to you ˹believers˺, so perhaps you may reflect
 
Muhindi (kanji) ,ukipata anakupa sh 10 ukikosa anachukua sh 100 yako.

Yeye ndie anayepata manufaa
 
Wewe hata user name inajieleza tu kuwa wewe ni mkamaria

By the way hamna nmna Mimi najua huwezi kuacha kamari

Maana ushakua teja no way out
 
Siumii kuhusu pesa cuz impact yake huwezi kuiona sasa hv .Ni mpaka ipite miezi,mwaka na miaka .Ukija kupiga hesabu ushatupa zaidi ya 50million halafu hata kibanda huna .

My biggest concern here is this addiction thing that kept building over time.

Sijui ushakutana na mraibu wa pombe ambae anasema kuwa hawezi kuacha pombe cuz hawezi kufanya ishu yoyote mpk anywe kidogo!? Sasa uraibu wa kamari nao ndio upo hivyo
Pole mzeya sie wengine uraibu wa mbususu yaani ulale bila kicheza na vuzi la mwanamke usingizi haupiti
 
Usitupangie we umepoteza laki 6 kwa miez 2 watu tupo ndani ya hii game kwa miaka 5 na kuendelea sema kama vip niwe nakupa odds za uhakika.
Miaka 5?? Nipo mwaka wa 12 huu, nilianza na zile za premier bet za karatasi
 
Miaka 5?? Nipo mwaka wa 12 huu, nilianza na zile za premier bet za karatasi
Vip bado upo kwenye game??? Maana mkeka wa leo kazi ya mikono yangu mwenyewe.
IMG_20220224_034641.jpg
 
Binafsi uraibu wangu wa kamari nimekuwa nikiuficha sana kiasi kwamba nobody in my family knows about it.

Ila nimeazimia kutumia kila jitihada kuacha masuala ya kubeti ,Mungu ajaalie iwe hivyo na anifanyie wepesi.
Mimi nilianzaga kimasikhara sikuwa na elimu na siku ya kwanza tu niliwwka 15000 nikabet mechi za siku 3 nikala 210000.
Nikaona eh kumbe easy.
Hapo ndo nikaanza rasmi, nikhawa na bet basket nakuka na kuliwa.
Siku moja nilipigwa ela ndefu sana, zaid ta 800k kwa siku moja.
Nikasema kuanzia leo mimi na betting basi, sasa ni mwaka wa pili sijabet.
Nikuwa nimebet kwa takribani mwaka mmoja.
 
Hongera kwa kuacha na muombe sana Mungu akulinde usije kurudia huu mchezo
 
N
Ahlan wa sahlan.

Leo naomba niongelee experience yangu fupi katika betting (Kamari).

Binafsi, mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wanaipinga sana michezo ya Kamari, maarufu kama betting. Ila kutokana na upweke (boredom) pamoja na udadisi (curiosity) wa kutaka kujua nini kipo nyuma ya michezo hii ya kubahatisha nikajikuta nimeweka pesa kwenye simu yangu nikaanza kubeti. Nilikuwa sijui A wala B kuhusiana na masuala haya, Ila kutokana na kielimu nilichojaaliwa kidogo halikuwa jambo zito kwa mimi kuanza kufaham terms mbalimbali kuhusiana na betting pamoja na masoko na mbinu zake.

Nilianza na single bet, nikashangaa baada ya dk 90 matokeo yakaja nimeshinda.. nilipata profit ya zaidi ya 3,0000/= nikajisemea mchezo ndio huu wa kupata pesa fasta fasta. Sikuitoa ile pesa kwenye simu akili ikanituma niendelee kubeti mechi nyingine.

Nikawa nakula baadhi na nyingine naliwa, hali ikaenda nikawa sasa mzoefu kuhusiana na betting. Masoko yote nayajua, mbinu mbalimbali za kubeti nazijua, pia nikawa member wa uzi wa kubeti humu JF.

Hali imeenda kwa miezi 2 sasa. Nimejikuta nazama katika uraibu kidogokidogo umekuwa sio ule mchezo wa kucheza kwa fujifurahisha tu bali umekuwa ni mchezo wa lazima kwangu. Kiasi naweza kushinda siku nzima napanga mikeka tu, huku ukizingatia kuwa sasa hivi tumerahisishiwa kubeti kiganjani kwa kutumia simu.

Hivi karibuni nimekaa nikasema ngoja nicheke bet history yangu, nikachukua na calculator nikaanza kupiga hesabu kiwango nilichocheza kwa muda wa miezi miwili. La haula nimejikuta nimepoteza zaidi ya sh laki 6 (600,000).

Ni kiwango kidogo kwa mwenye pesa na pia ni kiwango kikubwa kwa asiyekuwa na pesa. YES! Laki 6 zimeteketea ndani ya miezi 2. Mbaya zaidi hata ikitokea nimeshinda beti bado ile pesa naona nisiitoe kwenye account yangu ya betting badala yake niendelee kuizungusha kitendo kinachopelekea kuipoteza yote.

Ukiachana na jambo la kupoteza pesa kizembe, betting imenilete depression (msongo wa mawazo) pamoja na kuharibu mahusiano yangu kifamilia na kijamii. Kiasi muda mwingi nakuwa busy na simu yangu tu bila kujali familia inayonizunguka mke na watoto.

Experience niliyoipitia katika miezi hii miwili sitaki mtu mwingine aipitie. Uraibu wa kamari una nguvu sana kuliko uraibu wa sigara. Ni ngumu kwa mvuta sigara kutumia sh 600000 kununua sigara na kuzivuta zote kwa kipindi cha miezi miwili ila kwenye betting ni jambo la kufumba na kifumbua tu.

Wosia wangu kwa vijana ni kuwa KAA MBALI NA KAMARI IKIWA UNATAKA KUFANIKIWA. KAMARI (BETTING) SIO MCHEZO WA KUKUPATIA KIPATO. BALI NI MCHEZO WA KUKUTIA UMASIKINI.

Pia jambo lolote baya usipende kulidadisi ubaya wake, kuna mambo mengine mabaya ukishaingia kuyadadisi ili kujua kwanini ni mabaya utajikuta umenasa humo, mfano ni madawa wa kulevya, kamari, pombe, uchawi, zinaa n.k Wazungu wanasema "Curiosity kills the cat". Kuna vitu humu duniani havidadisiki. Ukiambiwa jambo kwenye vitabu vya dini kuwa ni ovu na ni baya usilisogelee kaa nalo mbali sana. Otherwise utakuja kujuta.

Imagine ndani ya miezi miwili nimepoteza zaidi ya laki 6, je ndani ya mwaka mmoja ningeenda kupoteza zaidi ya kiais gani? Binafsi sijutii kiasi cha pesa nilichokipoteza ila ninachojuta zaidi ni hii hali ya uraibu (addiction) inayoelekea kujijenga ndani ya kichwa changu.

Je, wewe msomaji nawe unasumbuliwa na tatizo la kubeti (kucheza kamari) kama ndio share basi hapa tuweze kusaidiana.
Nakazia
 
Back
Top Bottom