Ni kisa cha miaka 10 iliyopita lakini mhusika anapitia kipindi kigumu mpaka sasa
Ilifikia kipindi anashinda sana kanisani mpaka anaacha watoto nyumbani, hapiki analipa kanisa kipaumbele, kuchukua pesa za savings kwajili ya zaka na sadaka za kitapeli, anaweza kesha kanisani, n.k. Mume wake alimuacha na yeye alikuwa brainwashed kwamba ni sawa tu kulipa kanisa kipaumbele akajazwa maneno mme ni pepo.
Baada ya ndoa kuvunjika kukawa na mgao, Aliambulia nyumba moja ndogo na mali kadhaa zenye thamani ya milioni 10 hivi, alizidiwa akili kizembe akaanza kupeleka mafungu ya sadaka na misaada huko kanisani, ndani ya miaka miwili hana mbele wala nyuma imebidi ajenge duka dogo pale nyumbani kwake, sidhani kama anaingiza faida zaidi ya elf 5 kwa siku maana imekuwa ni kawaida baadhi ya siku nyumba yake pekee ipo gizani wakati majirani kuna umeme.
Akili zimekuja kumfunguka mwishoni kabisa kwamba wachungaji wake ni matapeli.
Pia soma:Hofu ya kuongezewa mke mwenza, wepesi wa kutoa talaka na kuachana bila kugawana mali inachangia wanawake waislam kuwa na adabu kuzidi wakristo?