Jinsi kilimo kilivyobadilisha maisha yangu

Jinsi kilimo kilivyobadilisha maisha yangu

majam19

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2024
Posts
900
Reaction score
971
Habar za mda ndugu zangu.
Leo nmependa kujumuika na vijana wenzangu ambao hawana ajira na bado wanalilia ajira nawapa pole sana.

NIANZE HAPA;mm ni kijana wa miaka26 Sasa,
nilizaliwa mkoani Tanga katika familia hata kula yetu ulikuwa Haina mpangilio wa ratiba,
kunawakat tulilala njaa kabisa
nikasoma katika mazngira magumu kidogo na Kwa bahati mbaya matokeo yang ya kidato Cha nne hayakuwa mazur nlipata four ya 28
nikiwa na pass za masomo 10 yote niliyofanya mtihani hapo ndipo ugumu wa maisha yangu
ya kusaka tonge ulipoanza nlikutana na
upinzani wa maneno makali kutoka Kwa
babayangu mzaz maana shuleni nilikuwa vizur sana masomo ya sayansi niliyapenda sana

ingawa matokeo ya mwisho yaliniumiza sana na kunikatisha tamaa kabisa kabisa huo ulikuwa n mwaka 2017 na hapo nilitimiza miaka 18,
baada ya matokeo ilinibidi niwe mtu wa
mawazo sana kiufupi nilikonda na kuonekan ni
kijana zaifu sana ukichanganya na maisha ya
nyumban jinsi yalivyokuwa pale nilijiona nimepoteza tumaini la maisha yangu yote niliyo yapambania sababu niliamini huo ndyo mwisho
wangu wa elimu maan Mzee asingekubali
kunipeleka chuo chochote ingawa bado
nilikuwa na nafasi nyingne ya kusoma kozi
nying na nzur tuuh,basi bhn maisha ya kazi mtaani ni saidia fundi Kwa siku ulikuwa n 9 au 10 elfu sababu sikuwa na ujuz wowote nilijuana na watu wengi sababu walifahamu sifa zangu za kusoma na maisha yangu kiufupi wengine walinicheka nkaumia sana😤😤😤😤

wengine walinipa pole na kunifariji katka nyakati hizi ngumu pamoja na majiran zangu mafundi ujenzi kuniita wakipata Kaz niwe napata riziki kidogo mana waliyajua maisha ya nyumban kwetu na ninayoyapitia kiujumla,maisha ya saidia fundi bado nayo hayakuwa mazur maan kuwanawakati unaweza kaa wiki2 huna Kaz ivyo nilizid kuwaza ni Kwa jinsi nitaishi na je?hii ndio hatma ya maisha yangu kweli niliumia nikatamani ninywe sumu nife maana Sina mtetez nlikuwa nikilia bila tumaini hasa ninapowaona wenzangu
wamerud likizo za shule,vyuon kiukwel nilitaman nijinyonge kabsa mwaka2018 Kuna braza mmoja nilikuwa namchulia kama kakangu alinipa nafasi ya kutafuta wazo lolote la ujasiliamali lenye kuanza na mtaji mdogo Kisha atanipa mtaji then baada ya kupata faida nmrudishie mtaji hapo kazi ikaanza ya kutafuta wazo la biashara Sina experience yeyeto na biashara basi nikapata wazo la kuwa nanunua nazi vijijini nakuja kuuza mjini kweli braza akani kiasa Cha laki3 kwaajir ya kuanzia nakumbuka nilipata tabu sana sio kidogo kulala vijijini wakat mwingne kwenye vijumba vibovu huko mashamban na bado nilipofika mjini nlikutana na upinzani mkubwa wa Bei sababu mtaji wangu ulikuwa hafifu na either nipate faida kidogo sana au nkose kabisa kabisa urudi mtaji tuuh basi nlifanya Kwa miez kazaa bila matunda yeyote mpaka ikafika mda niliona Bora nirudishe pesa ya watu isijepotea nitalipa nn mie.basi nilifika tamati ya iyo biashara nkafuta kaka nmpe jina la Jose siku narudisha ile pesa nikiwa ninamawazo na nmekata tamaa kweny biashara iyo Jose akaniuliza.

Jose;vp mbona mapema Leo

Mim;kaka naona Hali inazid kuwa ngumu

Jose;kwnn mdogo wangu (.....)??

Mim; biashara ni ngumu Hadi naogopa
nisijepoteza hii pesa Yako kaka maan sipati faida

Jose;ahahaha 😁😁 ndyo biashara zlivyo uwezu Anza Kwa faida tuh lazma upitie yote hayo

Mim;yaan kaka mpaka nahisi kuchanganyikiwa hapa

Jose; usiogope mdogo wangu mm Nina wazo jingne

Mim:wazo gani kak(.....)??

Jose;kwann usiwe unasafirisha kupeleka Arusha kule kuuhitajibmkubwa wa nazi sana

Mim;kweli kaka huku nikiwa nmepata faraja kidogo

Jose;iyo ela Bakinayo nakuongeza laki3.5 ili ufanye Kwa ukubwa kidogo saw dogo

Mim;saw kak nitambana mpaka mwisho nione napata faida.

Safari ya Arusha itaendelea na Mikasa yake huko
 
Muendelezo wa nilipoishia
Safari ikaanza ya kutoa na nazi mashamban kupeleka Arusha
Safar yangu ya kwanza ilikuwa ni ngumu na yenye maumivu makubwa kwani nilibeba mzigo wa lak6 nikitegemea kupata faida lakn jamaa wa pale soko la kilombelo walijuwa mm ni mgeni kwenye biashara hivyo walinipiga kwenye Bei
Nlimshukuru mungu kwani niliuza nazi zote Kwa Bei ya jumla sh.550 na shamban nlinunua Kwa sh.200 nikapiga hesabu ya usafiri,malazi,chakula walau kidogo nlipata faida Kwa mara ya kwanza

Hapo nikaanza kuona matunda ya kazi kwa mda mfupi tu niliweza kutoka kweny lak6.5 mpaka 1m nilijiona mwenye bahat sana nlimueleza braza Jose na kumpa mrejesho wote Kisha akanisihi niongeze juhud ya kupambna na kuhusu mtaji niendelee kuuzilungusha zaidi
Kiukwel nilifurah sana na kuona naweza kupiga hatua kubwa zaid kama kijana mdogo bas nakumbuka kunakipindi nazi ziliadimika kabisa nilienda mashamban napata mzigo kidogo ambao nkipiga hesabu ya usafiri na gharama nyinngene naona hakuna faida nakaona Bora kuwa nawatumia mzigo baahadhi ya wateja wangu Kisha wao wananitumia pesa yangu bila kufika Arusha

Hapo ndipo nilitapeliwa na mfanyabiashara mmoja pale sokon sitokaa nmsahau yule brow alikuwa ni ostaz madevu kabisa mtu wa kanzu na barashia akanipiga mzigo wa lak4 nliomtumia kiukwel hapo nlianza kuona mapichapicha kweny biashara iyo

Niliwaza na kuwazua sikupata majibu kabisa ilinibidi niende kwa braza nimueleza situation ilivyokuwa na nikabizi lak8 kama fidia ingawa yeye alivhukua lak7 Moja akanirushia
Nkaanza safari ya kutoka Tanga mpaka arusha kuanza kufutilia pesa yangu sina ndugu mji ule Sina pakulala ila nilijipa moyo kama kijana mpanaji nilikalia roli la kampuni ya mangate distributor nakumbuka nilifika usiku saa8 Sina ndug Wala jamaa asee ulikuwa hatar nililala kwenye karavati iliyopo tale tripleA njiapanda ya
Arusha technically asubuh na mapema nilifika kilombelo nikapewa maelekezo jinsi ya kumdai mfanyabiashara pale sokoni

Nilienda kumripoti akafautwa na mgambo mpaka pale Kisha nikatoa maelezo na vielelezo vya sms nilivyokuwa namuelekeza kuhus deni langu
Iyo ilinisaidia jamaa hukuwa na iyana litoa ahad ya kulipa baada ya wiki na kuweka sahihi kweny makubaliano
Sikuwa na budi zaid ya kusubir baada ya nikiangalia Sina ndugu Alo wiki hiyo haisimulik kiukwel nilala kweny majumba mabovu,makalavati
Mbu,alafu Kali zote zilikuwa zangu baada ya wiki kukamilika jamaa ostaz madevu alikuja na laki3 na nkikabidhiwa pale nyingne akasema atatoa baada ya siku 3 au 4 niliacha namba yangu ya simu na kuwashukur pale nikaacha chochote kwaajir ya usumbufu na kupata hakibyangu Kisha niliwapa maelekezo kama akileta iko kias kilichobak wanitumie kwenye namba yang
Mim nikarud Tanga na bus aina ya raqeeeeber nilikuwa na mawazo njia na uchovu wa kula sehemu ambazo ni hatarishi kupita kiasi
Nilipofika nyumbn nliwaza nitafanya jambo gani ikiwa Sina Tena biashara Wala pesa ya mtaji nilikuwa ni mtu mawazo sana kiukwel nilizid kukonda kupita kias

Wazo la kilimo
Nlipata wazo la kilimo baada ya kukosa fursa ya kufanya Kisha nikajiuliza maswali
1.nalima nn(.....)?
2.ntalima wap(......)???
3.kilimo ni biashara mtaji hela Sina(.....)???

Kiukwel machozi ya uchungu yalinitawala kweny maisha yangu na kukata tamaa nilijiona nipo Duniani kimakosa kwann niwe nakosa mm tuh
Wakat wengine mambo yao yanyooka niliwaz bila matumain ila nkajipa moyo nilianza kukata Kuni porin Kisha nakuja kuuza mjini nipate fedha ya mahitaj

Nlichekwa sana katika kipindi hiki na wengne walinisema kuwa nmechanganyikiwa na maisha baada ya matokeo yangu ya shule kutokuwa mazur
Niliumia ila nkajipa nafasi nyingne kweny maisha yangu nlifanya iyo Kaz ya Kuni pamoja na kulima vibarua na kupalia mazao huku wazo kuu langu ni kuwa mkulima
Watu walionifahamu kiundan waliumia sana wengine walihis nimejikatia tamaa ya maisha kama kijana mwenye uelewa Leo nakata Kuni
Nitaendelea wakati mwingne
 
Itaendelea ni ujanja ujanja wa wapiga dili....Unataka dili gani kwenye story yako...!!? 😁
 
Habari za wikiendi ndugu zangu ,
Poleni na majukumu naomba samahan kutokana na majukumu kidogo ila Leo naendelea


BASI mAisha yakaendelea nakumbuka 27/07/2018 ndyo safari ya kutoka Tanga mpaka mbeya baada kuona maisha ya tanga ni magumu nilirudi mpaka mbeya ambapo babayangu ndipo alipotokea na familia yake IPO uko na baadhi ya kaka na dada zangu niliomba lifti mpaka morogoro Kisha nikapanda basi mpaka mbeya -mbalari

Nilifikia kwabibi yang nikapokelewa vzur tu na maisha ya ugenini yakaanza kunabaadhi ya ndugu hawakupenda ujio wangu waliona kama nimeenda kula chakula Cha Bure maan ulikuwa ni mda wa mavuno

Changamoto za kiangazi zilikuwa nyingi sababu sikuwa na kazi ugeni ulinitesa wengi walishinfwa kuniamin sababu ya ugeni wangu ila nilipiga moyo wangu konde
Baada ya kukaa Kwa bibi Kwa mda ilinibidi nihamie Kwa shangaz yang kutokana na changamoto za pale Kwa bib yangu namshukuru mungu nilipokelewa baada ya kiangazi kuisha mvua za masika zilianza

Baada ya mvua za mwaka kuanza kama kawaida ya mkoa wa mbeya kilimo kwanza ndyo UTI wa mgongo
Nyumbn Kwa shangaz walinipenda sana kupita kiasi
Sababu nilijituma kupita maelezo nlifajifunza kupanda
Mpunga,kupalia mahindi n.k

Kiukwel nilijitoa kupita kiasi na wengi waliniona kama kijana mpambanaji hawakuamin kama nimetokea tanga baada ya mavuno tulivuna mpunga zaid ya roba 150 nilipewa roba 1 na mm npate nguo na baadhi ya mahitaj na mm kiukwel moyoni wangu niliumia ila
Sikuwa na namna yakufanya

Sababu nilikuwa nakaa nyumbn hivyo walinikulia bado mtoto ingawa pale nyumbn tulikuwa vijana kama 3 na wenzangu walipewa mitaji zaid ya maroba ya mpunga 20 Kila mmoja ila mm niliambiwa mwaka ujao ila sikukata tamaa nilijipa matumain baada yakuona fursa kubwa ya kilimo Kwa maeneo hayo na pesa nying kama ukiwa mtu wa kujituma na kazi

Mwaka uliofuata nikiwa nmeshaanza kuwa mzoefu na mtu kazi niliendelea kulima pale nyumbn tukiwa na mjomba na shangaz yang kiukwel nilisimamia shughuli zote za shambn Kwa ufasaha kabisa na kuhakikasha mazao yanarud salama baada ya mavuno nilikuja kupewa gunia3 kama fidia au malipo ya Kaz yangu Kwa msimu huo
Kiukwel nilijiona nachanganyikawa na napoteza mda miaka miwili hata sijanunua godoro Wala shuka amekweli nilijisemea kuwa Mimi naelekea kuwa masikini au fukara mpaka Leo Sina muelekeo wa maisha na wenzangu niliosomanao walikuwa wameanza university na mm bado sielewi kabisa
Hapo kichwan kwangu kulijaa mauzauza matupu

Basi ikanibidi nifanye maamuzi magumu ya kuuza gunia 2 nilizpewa kama malipo yang niliuza Kwa Bei ya 80elfu Kisha Moja nkakoboa mchele ili kupelekea wazaz wangu Tanga nilienda kukata ticket lengo lilikuwa ni kwenda kuangalia mazingra Kisha nirud Tena mbeya ambapo niliamua ndyo yawemakaz yangu
Nilianza Safari ya kupelekea Tanga njiani nikiwa najitafakari sana maswali yalikuwa mengi pasi na majibu
Je?mm ni Nan

Kusudi langu ni nn Duniani(
.....)??

Naelekea wap ikiwa umri ndyo unakwenda(....)??

Je?machoz ya Kila siku yananistali bila tumaini (.....)???

Hakika huwezi hata hamu ya kula sikuwanayo Toka safari inaanza mpaka nafika tanga.
Nilifika usiku sana hivyo chumba nilichokuwa na lala alishapewa mtu mwingne kwahyo usiku huo nililala nje na mizigo ilikwenda nyumbn na bodaboda
Asubuh nilijihimu kuamka nlikutana ndugu zangu pale mama,baba n.k

Kisha nilianza kutembelea marafiki,jamaa na Kisha nlikutana na braza Jose tulisalimiana na kupiga story mbili tatu Kisha akawa ananitania kuwa mbeya maisha yamenikubali maana walau mwilin ulikuwa vzur chakula hakikua hafifu pamoja na Kaz zangu ngumu nilifarijika kusikia wengi wakiniambia nmebadilika

Jose;mdogo wangu naona mbeya imekupeza sana Sasa unaonekan kijana smatie

Mm;hamna kaka bado nipo na mahangaiko uko ingawa walau namshukuru mungu

Jose; ulinianimbia unalima kule vp kiliko kinalipa uko(...)???

Mm; kiukwel kaka kilimo sio kibaya kikubwa ni kumomba mungu mvua ikinyesha bas ugumu wa maisha unapungua sana tofaut na Tanga

Jose; kwahyo bado unalima na mjomba Yako(...)??

Mm;ndyo lakn kwasas nimechoka maana sio faida nahis kupoteza muda then nawaona vijana wenzangu wanafanya maendeleo huwa nkaumia sana 😤 😤

Jose;kwan hakupi kitu baada ya kuvunja(...)??

Mm;kiwango Cha Kaz hakilingani na malipo hata kidogo msimu huu nlipwa gunia 3 tuuh na zote nmemaliza kweny nauli na huo mchele nlio kupata

Jose;sas shangaz ukimwambia anasemaje kuhusu ilo(...)??

Mm; kiukwel huwa na mwambia ila ananiambia nimvumilie mjomba mpak hajisikie yeye kunipa mtaji

Jose;pole mdogo wangu umekuwa mtu wa majanga Toka shule mpaka mtaani ila isikate tamaa hayo ni mapito tuuh

Mm;Kuna wakati nahis tabu nimeumbia maan najitahid kufanya kazi lakn wap, najitahid kuwa mtulivu,mpole mtu wa kusamehe lkn wap

Jose;nakujua vzurii mdogo wangu ucjal kwahyo umerud Tanga kuanza upya(....)??

Mm;hapan npo Kwa mda kidogo baada ya Kaz ngumu kule n Bora npumzshe kichwa maana nahis kukata tamaa

Tuliongea mengi sana ila alinisihi nisikate tamaa Kisha nirudi mbeya niulizie Bei za kukodi mashamba Kisha atanipa Mataji baada ya mavuno tuangalie kama Kuna faida kubwa basi nmrudishie mtaji

Kiukwel siwezi msahau huyu braza katka maisha yangu ingawa si ndugu yangu hata kidogo yeye mkristo mim Islamic lakn alijitoa kwangu hata kuliko watu familia yangu niseme Kwel
Bas nlikaa Tanga wiki 3 iv nkaondoka kurud mbeya

Nilipofika nilianza harakati zangu taratibu bila kushirikisha mtu pale nyumbn nilibahatika kupata shamba nkamfamisha braza akanitumia kama laki4
Na mm nlikuwa napiga mishe ndogondogo naweka akiba zangu nlinunua gunia1 kwaajir ya mbegu
Na shamba lilikuwa hekar 2

Mdu wa kilimo ulifika na shangaz nilikanae nkamueleza ingawa hakupenda na Wala hakuonyesha kuchukia mjomba nilimueleza baadaye
Ingawa alikubaliana kishingo upande kiukwel kweny ILO hakuwa na furah kabisa
Hapo nilishakuwa niamua liwalo na liwe tu siwez kubali kuwa mtumwa wa watu Kila siku ingawa maneno yalikuwa mengi kuwa nmetoa wapi pesa ya mtaji pia inaonekan nilikuwa naiba mpunga wa nyumbn mpaka nimepata pesa kukodi shamba

Kiukwel Mzee yule aliweka vikwazo vingi kama kunipa ratiba nying za shambn kwake ili anikomoe maana uwezo wa kwenda kupanga nyumb sikuwanao kiufupi nlikuwa bado hata godoro Sina Hali yang ilikuwa ni ngumu sana hata habari za wachumba sikuwaga natak hata kidogo mm bize na shamba tu
Hakika yule mjomba alihis atapoteza mtu muhmu sana kwhyo nlipitiwa wakati mgumu kikaz

Namshukuru mungu nilifanikiwa kupanda shamba langu nlitunza kiasi sababu sehemu kubwa ya pesa nlitemea kutoka Kwa braza hivyo hata yeye kunawakt anakwama inanibid nitumie akili na uwezo Wang kuendesha mambo hakika mungu hamtupi mja wake na penye Nia Pana njia hakiaka nilivuna gunia 51
Na riziki mwanzo wa chuki hakika wahenga walisema

Jamn mtanisamehe kidogo ila Leo ni lazma nimalize hiki kisa lengo ni kuwapa hamasa vijana wenzangu tusiogope maisha hatujui

Ntamalizia baada ya muda kidogo
 
Back
Top Bottom