Kumekuwa ana Mjadara Mkubwa Tanzania,Katika Maendeleo Ya kimziki Kwa Diamond Platnumz Na Wasanii wengine! Watu wanajaribu kufananisha maendeleo ya kimziki ya Diamond Platnumz na Davido,Wizkid na wengine kwa Miaka 5 nyuma Kuwa Walikuwa wanafukuzana! Ni kweli kabisaa Walikuwa Sawa lakini nini kimetokea?
Binafsi Naamini Kaabisa Kuwa LUGHA YETU YA KISWAHILI imechangia kwa Asilimia 99% kutengeneza Gap kati ya Diamond Na Wasanii Wa njee Kama Davido Na Wizkid! Nipinge uwezavyo lakini kwangu Mimi Kama Danya Naamini Kiswahilii ndio sababu kubwa
Kwasababu naamini ili mziki wako Upendwe ni lazima kile unacho imba kieleweke katika Jamii na Dunia Kwa ujumla ya wale Unao waambia! Wimbo Wako unaweza Kuwa na Maana Nzuri kabisa lakini Kama Haueleweki kwa watu kupendwa Itakuwa ngumu! Lugh ni kitu cha Msingi sana! Watanzania Tunapenda Nyimbo za Nje kwasababu Baadhi yetu Tunaelewa Kingereza Tunaelewa Lugh inayo imbwa Kwasababu Ni lugha Ya Kufundisha Katika Vyuo vyetu na Shule zetu! Lakini Kiswahili Je? Huwezi kuona Nigeria,Marekani na Mataifa Mengine wanajifunza Kiswahili! Na wasanii wakubwa Wote Duniani Wanataka Kujua Kile kinachoimbwa Kina maana Gani? Nyimbo zetu Nyingi Zimetapakaa AFRIKA MASHARIKI kwasababu Ya Kiswahili lakini huwezi Kusikia Nyimbo zetu zikipigwa Kwa wingi South Afrika, Na mataifa Ya Ulaya Kwasabau ya Lugha
Sio Kwamba Diamond hana Kipaji hapana au uwezo wake ni mdogo hapana Lakini Lugha ndio sababu kubwa inayo mtesa! Ndio maana Huwezi Kumuona Davido Au Wizkid nyimbo zao Zote wanaimba kwa lugha hao hapana Wanaimba Kwa Kingereza na Ndio sababu kubwa zinasambaa na kupendwa Duniani kwasababu zinaeleweka! Hata kwenye Show Ni rahisi Msanii Kuimba na Mashabiki zake kwasababu wanaelewa kile kinacho imbwa lakini Sio Diamond Show Za nje kuimba Na Mashabiki zake kwasababu wengi hawaelewi lugha
Naamini Kabisa Mziki wa Tanzania Na Afrika Mashariki Kwa ujumla Bado Una safari ndefu sana Kwasababu Ya lugha Ya Kiswahili! Ni either Waache Kabisa Kuimba Kiswahili waimbe Kwa kingereza Au wasubiri kiswahili kienee Duniani Kote ndio mziki wetu Utafika Mbali! Hata Ikitokea Diamond Akaimba kwa kingereza basi Matamshi yake Hatakiwa vizuri kwasbabu sio Lugha anayo ituma mara kwa mara! Ndio maana Diamond anatumia Gharama Kubwa sana Kufanya Collabo na wasanii wa nje ya Tanzania Ili kufikisha Mziki wetu mbali kwasababu ya Lugha ya kiswahilii! Ukweli ni kwamba Kwa msanii Yeyote yule wa Tanzania ili mziki wako Ufike nje Ya afrika Mashariki Unahitaji Kufanya Collabo za Kimataifa nyingi kadri uwezavyo..... Kinacho mfanya Alikiba Asiwe Wa kimatafita ni kwasababu Ya ufinyu wa Kolabo za Kimataifa hivyo watu inakuwa ngumu Kuelewa Kishwahili/Lugha Inayo Imbwa
LUGHA YA KISWAHILI NI JANGA KWA MUZIKI WETU
Ni mtazamo Tuu
Mie niko tofauti kidogo kwa mtazamo huu,
Nadhani wewe mtoa mada Lugha yako ni kiswahili, English ni second language kwako,
Leo hii nikuletee wasanii watatu,
1)Diamond
2)Davido
3)Wizkid
Halafu nikwambie chagua mmoja tu mkali sidhani kama utachagua Diamond.
Kwa nini nimetoa mfano huo? Nimejaribu kukuletea mtu ambae unasema lugha yakiingereza ni kikwazo kwake kwenda kimataifa ili umpime katika lugha yake anayotumia na hao wengine.
Kwa hiyo unaposema hawa jamaa kuna kipindi walikua sawa yaweza kuwa kweli lakini ni kipindi walikua bado hawajapata kuonyesha uwezo wao,
Leo hii Diamond pamoja na kutumia kiswahili ambacho ndicho unachotumia wewe mtoa mada bado huwezi kumchagua kwamba ni bora kuliko wengine(japo wewe sio mzungu) kusema kwamba ligha yake huijui.
Kikubwa anachotakiwa kufanya ndugu yetu ni connection za maana, aboreshe mziki wake, na pia ajaribu kuangalia vizuri timu yake ya fitna, wanaigeria wanapata suport kubwa sana lakini management zao zinafanya vitu vya ziada kwa wao kupenya duniani.
Kuna kipindi P SQUARE waliwahi kusema wao wanapotoa ngoma mpya hutuma watu sehemu mbali mbali kusikilizia mwitikio/mapokeo yake, hata hapa Tz wanatuma mtu aje asikilize ngoma imepokelewa vipi?
Hiko ni kitu kidogo lakini muhimu sana,
Je ni vingapi kama hivyo management ya D huwa haivitilii maanani?
Sent from my iPhone using JamiiForums