Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi sidhani kama mondi alikuwa Sawa na hao jamaa kimuziki kabla , davido alikuwa juu kuliko mondi for that time ndio maana mondi alimtumia davido kujukikana zaidi baada ya kumshilikishaIna maana kwa kipindi ambacho walikua sawa kimuziki diamond alikua anatumia lugha gan
Lugha sio kigezo sana cha kufanya muZiki unaoufanya ufike mbali. Music it's all about melody.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yes that's pointMleta uzi mziki mzuri sio lugha asee, mziki mzuri ni melody ndio maana unaweza ukasikia wimbo ukajikuta unatikisa kichwa tu pasipo hata kujua maana yake, hao hao wakina Davido n Wiz kid nyimbo zao nyingi tu wamejaza kiYORUBA na ki IGBO na bado tunawasikiliza refer UJUELEGBA by wizkidayo
Kuna watu hawajui chochote kuhusu mzikiMkuu acha masikhara aisee, diamond ameshakuwa nominated kwenye tuzo za BET hivyo anafahamika vizuri mno, Rayvanny ameshakuwa hadi tuzo huko BET WTF useme hawajulikani?? Acha chuki
Tanzania kuna msanii anaitwa Kimbunga huyu unaweza kuwauliza watanzania million 20 na wakwambie hawamjui ila ukiwauliza watu waliyoko kwenye industry ya muziki wanamfahamu
Tueleze wewe sasa unayejua nini maana ya kijulikanaShida utakuwa ujuwi nini maana ya kujulikana.(humaarufu).
Hiki ndiyo kifaransa eeeeh!!??!Waliimba kwa kifaransa mataifa kibao africa yana zungumza kifaransa, Diamond mjanja sana aisee ana ngoma yake inaitwa wakawaka imekuwa banned hapa bongo ila inachezwa U.S jamaa kajitahidi kulenga japo kiswahili kinatuangusha sana.
😆😆😆😆😆Agaaaaa Agaaa Agaaaaa ( umenitekaa)
Dodo la yo- yooo Amena ofisa tangia chamanda
Sent using Jamii Forums mobile app
ujuwi= hujuiShida utakuwa ujuwi nini maana ya kujulikana.(humaarufu).
Mkuu wimbo wa malaika wa kiswahili ulipendwa na kuigwa na wanamuziki wakubwa sana duniani mfano Born M, na wengine wengi.
Tafadhari search google taarifa za huu wimbo. Huenda wewe ni kijana mdogo sana haujui kuhusu hili jambo.
Kitu cha msingi ni kuimba wimbo mzuri na ujumbe mzuri na ndicho kilicho ubeba wimbo wa Malaika.
Sio kila wimbo ni KifaransaBro kile Ni kifaransa, Ndio Maana Diamond Kaamua Kutafuta Collabo Na Wafaransa Kwasababu Kifaransa Huwezi Fananisha na Kiswahili
Bora kuzaliwa ulaya.......@anafaaa kupigwa risasiDah ingekuwa hivyo akina Franco Luambo Makiadi, Bongo man, Koffi Olomide n.k tusingewaju maana hata sielewi wanaimba nini ila miziki yao naipenda balaa...
Kumekuwa ana Mjadara Mkubwa Tanzania,Katika Maendeleo Ya kimziki Kwa Diamond Platnumz Na Wasanii wengine! Watu wanajaribu kufananisha maendeleo ya kimziki ya Diamond Platnumz na Davido,Wizkid na wengine kwa Miaka 5 nyuma Kuwa Walikuwa wanafukuzana! Ni kweli kabisaa Walikuwa Sawa lakini nini kimetokea?
Binafsi Naamini Kaabisa Kuwa LUGHA YETU YA KISWAHILI imechangia kwa Asilimia 99% kutengeneza Gap kati ya Diamond Na Wasanii Wa njee Kama Davido Na Wizkid! Nipinge uwezavyo lakini kwangu Mimi Kama Danya Naamini Kiswahilii ndio sababu kubwa
Kwasababu naamini ili mziki wako Upendwe ni lazima kile unacho imba kieleweke katika Jamii na Dunia Kwa ujumla ya wale Unao waambia! Wimbo Wako unaweza Kuwa na Maana Nzuri kabisa lakini Kama Haueleweki kwa watu kupendwa Itakuwa ngumu! Lugh ni kitu cha Msingi sana! Watanzania Tunapenda Nyimbo za Nje kwasababu Baadhi yetu Tunaelewa Kingereza Tunaelewa Lugh inayo imbwa Kwasababu Ni lugha Ya Kufundisha Katika Vyuo vyetu na Shule zetu! Lakini Kiswahili Je? Huwezi kuona Nigeria,Marekani na Mataifa Mengine wanajifunza Kiswahili! Na wasanii wakubwa Wote Duniani Wanataka Kujua Kile kinachoimbwa Kina maana Gani? Nyimbo zetu Nyingi Zimetapakaa AFRIKA MASHARIKI kwasababu Ya Kiswahili lakini huwezi Kusikia Nyimbo zetu zikipigwa Kwa wingi South Afrika, Na mataifa Ya Ulaya Kwasabau ya Lugha
Sio Kwamba Diamond hana Kipaji hapana au uwezo wake ni mdogo hapana Lakini Lugha ndio sababu kubwa inayo mtesa! Ndio maana Huwezi Kumuona Davido Au Wizkid nyimbo zao Zote wanaimba kwa lugha hao hapana Wanaimba Kwa Kingereza na Ndio sababu kubwa zinasambaa na kupendwa Duniani kwasababu zinaeleweka! Hata kwenye Show Ni rahisi Msanii Kuimba na Mashabiki zake kwasababu wanaelewa kile kinacho imbwa lakini Sio Diamond Show Za nje kuimba Na Mashabiki zake kwasababu wengi hawaelewi lugha
Naamini Kabisa Mziki wa Tanzania Na Afrika Mashariki Kwa ujumla Bado Una safari ndefu sana Kwasababu Ya lugha Ya Kiswahili! Ni either Waache Kabisa Kuimba Kiswahili waimbe Kwa kingereza Au wasubiri kiswahili kienee Duniani Kote ndio mziki wetu Utafika Mbali! Hata Ikitokea Diamond Akaimba kwa kingereza basi Matamshi yake Hatakiwa vizuri kwasbabu sio Lugha anayo ituma mara kwa mara! Ndio maana Diamond anatumia Gharama Kubwa sana Kufanya Collabo na wasanii wa nje ya Tanzania Ili kufikisha Mziki wetu mbali kwasababu ya Lugha ya kiswahilii! Ukweli ni kwamba Kwa msanii Yeyote yule wa Tanzania ili mziki wako Ufike nje Ya afrika Mashariki Unahitaji Kufanya Collabo za Kimataifa nyingi kadri uwezavyo..... Kinacho mfanya Alikiba Asiwe Wa kimatafita ni kwasababu Ya ufinyu wa Kolabo za Kimataifa hivyo watu inakuwa ngumu Kuelewa Kishwahili/Lugha Inayo Imbwa
LUGHA YA KISWAHILI NI JANGA KWA MUZIKI WETU
Ni mtazamo Tuu