Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumekuwa ana Mjadara Mkubwa Tanzania,Katika Maendeleo Ya kimziki Kwa Diamond Platnumz Na Wasanii wengine! Watu wanajaribu kufananisha maendeleo ya kimziki ya Diamond Platnumz na Davido,Wizkid na wengine kwa Miaka 5 nyuma Kuwa Walikuwa wanafukuzana! Ni kweli kabisaa Walikuwa Sawa lakini nini kimetokea?
Binafsi Naamini Kaabisa Kuwa LUGHA YETU YA KISWAHILI imechangia kwa Asilimia 99% kutengeneza Gap kati ya Diamond Na Wasanii Wa njee Kama Davido Na Wizkid! Nipinge uwezavyo lakini kwangu Mimi Kama Danya Naamini Kiswahilii ndio sababu kubwa
Kwasababu naamini ili mziki wako Upendwe ni lazima kile unacho imba kieleweke katika Jamii na Dunia Kwa ujumla ya wale Unao waambia! Wimbo Wako unaweza Kuwa na Maana Nzuri kabisa lakini Kama Haueleweki kwa watu kupendwa Itakuwa ngumu! Lugh ni kitu cha Msingi sana! Watanzania Tunapenda Nyimbo za Nje kwasababu Baadhi yetu Tunaelewa Kingereza Tunaelewa Lugh inayo imbwa Kwasababu Ni lugha Ya Kufundisha Katika Vyuo vyetu na Shule zetu! Lakini Kiswahili Je? Huwezi kuona Nigeria,Marekani na Mataifa Mengine wanajifunza Kiswahili! Na wasanii wakubwa Wote Duniani Wanataka Kujua Kile kinachoimbwa Kina maana Gani? Nyimbo zetu Nyingi Zimetapakaa AFRIKA MASHARIKI kwasababu Ya Kiswahili lakini huwezi Kusikia Nyimbo zetu zikipigwa Kwa wingi South Afrika, Na mataifa Ya Ulaya Kwasabau ya Lugha
Sio Kwamba Diamond hana Kipaji hapana au uwezo wake ni mdogo hapana Lakini Lugha ndio sababu kubwa inayo mtesa! Ndio maana Huwezi Kumuona Davido Au Wizkid nyimbo zao Zote wanaimba kwa lugha hao hapana Wanaimba Kwa Kingereza na Ndio sababu kubwa zinasambaa na kupendwa Duniani kwasababu zinaeleweka! Hata kwenye Show Ni rahisi Msanii Kuimba na Mashabiki zake kwasababu wanaelewa kile kinacho imbwa lakini Sio Diamond Show Za nje kuimba Na Mashabiki zake kwasababu wengi hawaelewi lugha
Naamini Kabisa Mziki wa Tanzania Na Afrika Mashariki Kwa ujumla Bado Una safari ndefu sana Kwasababu Ya lugha Ya Kiswahili! Ni either Waache Kabisa Kuimba Kiswahili waimbe Kwa kingereza Au wasubiri kiswahili kienee Duniani Kote ndio mziki wetu Utafika Mbali! Hata Ikitokea Diamond Akaimba kwa kingereza basi Matamshi yake Hatakiwa vizuri kwasbabu sio Lugha anayo ituma mara kwa mara! Ndio maana Diamond anatumia Gharama Kubwa sana Kufanya Collabo na wasanii wa nje ya Tanzania Ili kufikisha Mziki wetu mbali kwasababu ya Lugha ya kiswahilii! Ukweli ni kwamba Kwa msanii Yeyote yule wa Tanzania ili mziki wako Ufike nje Ya afrika Mashariki Unahitaji Kufanya Collabo za Kimataifa nyingi kadri uwezavyo..... Kinacho mfanya Alikiba Asiwe Wa kimatafita ni kwasababu Ya ufinyu wa Kolabo za Kimataifa hivyo watu inakuwa ngumu Kuelewa Kishwahili/Lugha Inayo Imbwa
LUGHA YA KISWAHILI NI JANGA KWA MUZIKI WETU
Ni mtazamo Tuu
Kupitia mifano uliyoitaja, inathibitisha kuwa bandiko lake halina uhalisia, ni kama porojo tuu hakuwaza wala kukumbuka na kujisahihisha kabla ya kuamua kuandika.Dah ingekuwa hivyo akina Franco Luambo Makiadi, Bongo man, Koffi Olomide n.k tusingewaju maana hata sielewi wanaimba nini ila miziki yao naipenda balaa...
Nadhani umefinya sana ktk kiwango cha kufikiri kuhusu lugha na wasani!!
Ungejiuliza maswali kwann kina Koffi Olomide had sasa miiziki yao inatisha??? Je uliwahi kuwasikia Mbilia Bell,Kanda Bongoman , Madilu, Awilo,je umejarbu kuangalia influence ya lugha na muziki ikoje!??? Je Makhirikhiri nao unawajua???
Wote hawa wameimba nyimbo kwa lugha zao lakn hadi sasa nyimbo zao zikipigwa hata wa kiingereza chako haufui dafu
Tunakariri maisha ndg Lugha haina mahusiano kabsa na ulichokisema ...ndio maans watu kama ww mnakuta mnamshangaa mtu hajui kiingereza lakn ni msomi
Sent using Jamii Forums mobile app
Hao akina tekno na wizkid wanaimba ngoma zinazo eleweka na ngoma nyingi zinazo heat ziko romantic sanaa..na maneno yao yanagusa nyoyo...
Sent using Jamii Forums mobile app
Ojolegba wa wizkidayo naukubali kinoma lakini sielewi anaimba kitu gani.
Kina Sarkodie wanaimba sijui vitu gani lakini ni moto wa kuotea mbali. Mziki mzuri ni zaidi ya lugha ndiyo maana Gang nam style ya kikorea ilitikisa YouTube
Sent using Jamii Forums mobile app
Umefikiria juu juu sana ndugu...
Unamjua jamaa mmoja kutoka korea kusini anaitwa PSY!!!!
Mwaka 2016 kama sikosei, alitoa hit song yake iliyokwenda kwa jina la GANGNAM STYLE. Aliimba kwa lugha yao ya korea na alifanikiwa kuhit dunia nzima ilhali hakuna aliyeelewa lugha yake. Gangnam style ina viewers billion+....
Mziki ni feelings
Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi Bongo tunaongea Kifaransa?!Waliimba kwa kifaransa mataifa kibao africa yana zungumza kifaransa, Diamond mjanja sana aisee ana ngoma yake inaitwa wakawaka imekuwa banned hapa bongo ila inachezwa U.S jamaa kajitahidi kulenga japo kiswahili kinatuangusha sana.
Pale los angels ndo mahali ambampo maburudisho yote ya dunia yameasisiwa....na kuna nguzo tatu za maburudisho, kila anayefanya entertainment na ili afanikiwe kwa kiwango chake lazima ahamasishe nguzo moja au mbili, au zote tatu...nguzo hzo ni Ngono (mapenzi), Mauaji na Ushirikina...bila kufanya hvo hutoboi unless ufanye God related MusicPia mwambie aache kuimba matusi maana kila nyimbo wao lazima wahusishe ngono
Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani umefinya sana ktk kiwango cha kufikiri kuhusu lugha na wasani!!
Ungejiuliza maswali kwann kina Koffi Olomide had sasa miiziki yao inatisha??? Je uliwahi kuwasikia Mbilia Bell,Kanda Bongoman , Madilu, Awilo,je umejarbu kuangalia influence ya lugha na muziki ikoje!??? Je Makhirikhiri nao unawajua???
Wote hawa wameimba nyimbo kwa lugha zao lakn hadi sasa nyimbo zao zikipigwa hata wa kiingereza chako haufui dafu
Tunakariri maisha ndg Lugha haina mahusiano kabsa na ulichokisema ...ndio maans watu kama ww mnakuta mnamshangaa mtu hajui kiingereza lakn ni msomi
Sent using Jamii Forums mobile app