Jinsi kiswahili kinavyomrudisha nyuma Diamond

Jinsi kiswahili kinavyomrudisha nyuma Diamond

Kumekuwa ana Mjadara Mkubwa Tanzania,Katika Maendeleo Ya kimziki Kwa Diamond Platnumz Na Wasanii wengine! Watu wanajaribu kufananisha maendeleo ya kimziki ya Diamond Platnumz na Davido,Wizkid na wengine kwa Miaka 5 nyuma Kuwa Walikuwa wanafukuzana! Ni kweli kabisaa Walikuwa Sawa lakini nini kimetokea?

Binafsi Naamini Kaabisa Kuwa LUGHA YETU YA KISWAHILI imechangia kwa Asilimia 99% kutengeneza Gap kati ya Diamond Na Wasanii Wa njee Kama Davido Na Wizkid! Nipinge uwezavyo lakini kwangu Mimi Kama Danya Naamini Kiswahilii ndio sababu kubwa

Kwasababu naamini ili mziki wako Upendwe ni lazima kile unacho imba kieleweke katika Jamii na Dunia Kwa ujumla ya wale Unao waambia! Wimbo Wako unaweza Kuwa na Maana Nzuri kabisa lakini Kama Haueleweki kwa watu kupendwa Itakuwa ngumu! Lugh ni kitu cha Msingi sana! Watanzania Tunapenda Nyimbo za Nje kwasababu Baadhi yetu Tunaelewa Kingereza Tunaelewa Lugh inayo imbwa Kwasababu Ni lugha Ya Kufundisha Katika Vyuo vyetu na Shule zetu! Lakini Kiswahili Je? Huwezi kuona Nigeria,Marekani na Mataifa Mengine wanajifunza Kiswahili! Na wasanii wakubwa Wote Duniani Wanataka Kujua Kile kinachoimbwa Kina maana Gani? Nyimbo zetu Nyingi Zimetapakaa AFRIKA MASHARIKI kwasababu Ya Kiswahili lakini huwezi Kusikia Nyimbo zetu zikipigwa Kwa wingi South Afrika, Na mataifa Ya Ulaya Kwasabau ya Lugha

Sio Kwamba Diamond hana Kipaji hapana au uwezo wake ni mdogo hapana Lakini Lugha ndio sababu kubwa inayo mtesa! Ndio maana Huwezi Kumuona Davido Au Wizkid nyimbo zao Zote wanaimba kwa lugha hao hapana Wanaimba Kwa Kingereza na Ndio sababu kubwa zinasambaa na kupendwa Duniani kwasababu zinaeleweka! Hata kwenye Show Ni rahisi Msanii Kuimba na Mashabiki zake kwasababu wanaelewa kile kinacho imbwa lakini Sio Diamond Show Za nje kuimba Na Mashabiki zake kwasababu wengi hawaelewi lugha

Naamini Kabisa Mziki wa Tanzania Na Afrika Mashariki Kwa ujumla Bado Una safari ndefu sana Kwasababu Ya lugha Ya Kiswahili! Ni either Waache Kabisa Kuimba Kiswahili waimbe Kwa kingereza Au wasubiri kiswahili kienee Duniani Kote ndio mziki wetu Utafika Mbali! Hata Ikitokea Diamond Akaimba kwa kingereza basi Matamshi yake Hatakiwa vizuri kwasbabu sio Lugha anayo ituma mara kwa mara! Ndio maana Diamond anatumia Gharama Kubwa sana Kufanya Collabo na wasanii wa nje ya Tanzania Ili kufikisha Mziki wetu mbali kwasababu ya Lugha ya kiswahilii! Ukweli ni kwamba Kwa msanii Yeyote yule wa Tanzania ili mziki wako Ufike nje Ya afrika Mashariki Unahitaji Kufanya Collabo za Kimataifa nyingi kadri uwezavyo..... Kinacho mfanya Alikiba Asiwe Wa kimatafita ni kwasababu Ya ufinyu wa Kolabo za Kimataifa hivyo watu inakuwa ngumu Kuelewa Kishwahili/Lugha Inayo Imbwa

LUGHA YA KISWAHILI NI JANGA KWA MUZIKI WETU

Ni mtazamo Tuu
Hivi watanzania wengi sana wanapenda sana nyimbo za wacongo zinazoimbwa kwa kilingala na wacongo kama koffi olomide,je watanzania hao wanaelewa kilingala ?
 
Nyie ndo mnaowadanganya hao wasanii waimbe kingreza wakati hawawezi!
Naona hata harmonize nae siku hizi anachomeka maneno ya kingereza mengi!

Mkuu mziki ni hisia unapogusa hisia za mteja wako basi umemaliza kila kitu!
Na ili uweze kumkuna vilivyo msikilizaji wako imba kwa lugha yako!

Nakumbuka miaka yetu ile kulikua kuna muziki ule wa south africa ebhanaeeeee wale wajomba walikuwa wanaimba kwa hisia hatari unajikuta kanda nzima unasikiliza vizuri kabisa ila huelewi chochote!

Na nilibahatika kuwaona wakiwa wanaimba laivu walipokuja kupata mafunzo ya kwenda kupigania uhuru huko kwao miaka ya 90+ kwenye kambi yao kule Iringa
 
Haukuwa Wimbo Ilikuwa Style Ndio maana Style Ya ngororo Ya Diamond Isambaa lakini Ojolegba Ya Wizkid Inaeleweka sana Kuliko Kamwambie Ya Diamond
Inaelewekaje wakati kiswahili ni popular kuliko hicho ki-yoruba sijui igbo/Hausa? Acha porojo bana

Gangnam style ni wimbo sio style, kubali kuwa hoja yako imekosa mashiko
 
Hiyo lugha ni kihispanola ambayo inazungumzwa na watu wengi kuliko kiingereza , hata US kihispanola inazungumzwa Sana , Texas, California ( kumbuka California sehemu kubwa yake ilikuwa ni sehemu ya Mexico kabla ya kuporwa na marekani) , Puerto Rico etc , mtoa mada kiasi Fulani Yuko sahihi , kwenye active market ya muziki dunia kiingereza kinachukua nafasi , ndio maana Julio igleas sio maarufu Sana kuliko mwanae Enrique igleas , waimbaji wengi wa kihispanola na french utoa nyimbo hiyo hiyo kwa English version , kwanini unafikiri Celine Dion haimbi nyimbo kwa lugha ya kwao ( french ( Quebec) kwa sababu alishaimba kwa kifaransa lakini hakufanikiwa Sana , ndio maana the Scorpion wale jamaa wanaopiga rock wa Germany wanaimba kiingereza, music active market yake ipo Sana US na ulaya, ingawa kuna few exceptions
[emoji870][emoji870][emoji870] Pamoja boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lil kesh,Olamide na Phyno wa Nigeria ngoma zao wanatumia sana Igbo na Yoruba language, lakini ngoma zao nazielewa kinoma na zinavuka border hata wasio elewa lyrics wana-enjoy... tafuta sababu nyingine
 
Lil kesh,Olamide na Phyno wa Nigeria ngoma zao wanatumia sana Igbo na Yoruba language, lakini ngoma zao nazielewa kinoma na zinavuka border hata wasio elewa lyrics wana-enjoy... tafuta sababu nyingine
Kabisa ksma phyno na olamide hawaimbi kingereza kabisa Ni kilugha tu lakini magoma Yao yanatusua.
Diamond sikuhizi ubunifu umepungua nyimbo zake nyingi maneno yanajirudia rudia mfano maneno Kama
kitandani unanimaliza,
Msambwanda
Sotojo
Mtoto fundi
Kungwi
Hayo maneno ukisikiliza nyimbo za hivi karibuni lazima ukutane nayo Ni maka unasikiliza kitu kimoja



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiingereza wabachoimba wanaijeria wanaelewa wanaijeria wenyewe tu. Nilisikiliza wimbo wa Davido alioimba na Meek Mill aibu niliona mimi.
 
Kabisa ksma phyno na olamide hawaimbi kingereza kabisa Ni kilugha tu lakini magoma Yao yanatusua.
Diamond sikuhizi ubunifu umepungua nyimbo zake nyingi maneno yanajirudia rudia mfano maneno Kama
kitandani unanimaliza,
Msambwanda
Sotojo
Mtoto fundi
Kungwi
Hayo maneno ukisikiliza nyimbo za hivi karibuni lazima ukutane nayo Ni maka unasikiliza kitu kimoja
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Kweli mkuu, hicho kitu nimekiona kwenye ngoma zake za hivi karibuni.. ubunifu ni Zero kabisa hata Discipline ya kazi saivi Imepungua sana, Kingine Management yake inaogopa kumchana
 
Mleta uzi mziki mzuri sio lugha asee, mziki mzuri ni melody ndio maana unaweza ukasikia wimbo ukajikuta unatikisa kichwa tu pasipo hata kujua maana yake, hao hao wakina Davido n Wiz kid nyimbo zao nyingi tu wamejaza kiYORUBA na ki IGBO na bado tunawasikiliza refer UJUELEGBA by wizkidayo
 
Mziki hauna lugha mkuu,Kuna migoma ya kispaniola huwa naiselebuka mpaka chini lakini sijui maana ya nini?
 
Mkuu acha masikhara aisee, diamond ameshakuwa nominated kwenye tuzo za BET hivyo anafahamika vizuri mno, Rayvanny ameshakuwa hadi tuzo huko BET WTF useme hawajulikani?? Acha chuki

Tanzania kuna msanii anaitwa Kimbunga huyu unaweza kuwauliza watanzania million 20 na wakwambie hawamjui ila ukiwauliza watu waliyoko kwenye industry ya muziki wanamfahamu
Shida utakuwa ujuwi nini maana ya kujulikana.(humaarufu).
 
Ina maana kwa kipindi ambacho walikua sawa kimuziki diamond alikua anatumia lugha gan

Lugha sio kigezo sana cha kufanya muZiki unaoufanya ufike mbali. Music it's all about melody.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu hata yeye anaamua kubalance kwa kushirikisha wa nje waimbe lugha yao kingereza
 
Muziki wenyewe tayari ni lugha ambayo inaeleweka dunia nzima. Music itself is a universal language. Wahindi wametuimbisha sana masongi na tulikuwa hata hatuelewi wanachoimba. Sasa Kuch Kuch Hota Hai nani alikuwa anaelewa?

Una hoja dhaifu.
 
Muziki wenyewe tayari ni lugha ambayo inaeleweka dunia nzima. Music itself is a universal language. Wahindi wametuimbisha sana masongi na tulikuwa hata hatuelewi wanachoimba. Sasa Kuch Kuch Hota Hai nani alikuwa anaelewa?

Una hoja dhaifu.
 
Muziki wenyewe tayari ni lugha ambayo inaeleweka dunia nzima. Music itself is a universal language. Wahindi wametuimbisha sana masongi na tulikuwa hata hatuelewi wanachoimba. Sasa Kuch Kuch Hota Hai nani alikuwa anaelewa?

Una hoja dhaifu.
 
Back
Top Bottom