Jinsi kiswahili kinavyomrudisha nyuma Diamond

Jinsi kiswahili kinavyomrudisha nyuma Diamond

The ting goes skrrrahh, pap, pap, ka-ka-ka Skidiki-pap-pap, and a pu-pu-pudrrrr-boom Skya, du-du-ku-ku-dun-dun Poom, poom, you dun know

Hicho kibwagizo kilipendwa sana kwenye nyimbo ya man not hot na haina maana yoyote

"Typed with my thumbs."
 
Pia mwambie aache kuimba matusi maana kila nyimbo wao lazima wahusishe ngono
Kumekuwa ana Mjadara Mkubwa Tanzania,Katika Maendeleo Ya kimziki Kwa Diamond Platnumz Na Wasanii wengine! Watu wanajaribu kufananisha maendeleo ya kimziki ya Diamond Platnumz na Davido,Wizkid na wengine kwa Miaka 5 nyuma Kuwa Walikuwa wanafukuzana! Ni kweli kabisaa Walikuwa Sawa lakini nini kimetokea?

Binafsi Naamini Kaabisa Kuwa LUGHA YETU YA KISWAHILI imechangia kwa Asilimia 99% kutengeneza Gap kati ya Diamond Na Wasanii Wa njee Kama Davido Na Wizkid! Nipinge uwezavyo lakini kwangu Mimi Kama Danya Naamini Kiswahilii ndio sababu kubwa

Kwasababu naamini ili mziki wako Upendwe ni lazima kile unacho imba kieleweke katika Jamii na Dunia Kwa ujumla ya wale Unao waambia! Wimbo Wako unaweza Kuwa na Maana Nzuri kabisa lakini Kama Haueleweki kwa watu kupendwa Itakuwa ngumu! Lugh ni kitu cha Msingi sana! Watanzania Tunapenda Nyimbo za Nje kwasababu Baadhi yetu Tunaelewa Kingereza Tunaelewa Lugh inayo imbwa Kwasababu Ni lugha Ya Kufundisha Katika Vyuo vyetu na Shule zetu! Lakini Kiswahili Je? Huwezi kuona Nigeria,Marekani na Mataifa Mengine wanajifunza Kiswahili! Na wasanii wakubwa Wote Duniani Wanataka Kujua Kile kinachoimbwa Kina maana Gani? Nyimbo zetu Nyingi Zimetapakaa AFRIKA MASHARIKI kwasababu Ya Kiswahili lakini huwezi Kusikia Nyimbo zetu zikipigwa Kwa wingi South Afrika, Na mataifa Ya Ulaya Kwasabau ya Lugha

Sio Kwamba Diamond hana Kipaji hapana au uwezo wake ni mdogo hapana Lakini Lugha ndio sababu kubwa inayo mtesa! Ndio maana Huwezi Kumuona Davido Au Wizkid nyimbo zao Zote wanaimba kwa lugha hao hapana Wanaimba Kwa Kingereza na Ndio sababu kubwa zinasambaa na kupendwa Duniani kwasababu zinaeleweka! Hata kwenye Show Ni rahisi Msanii Kuimba na Mashabiki zake kwasababu wanaelewa kile kinacho imbwa lakini Sio Diamond Show Za nje kuimba Na Mashabiki zake kwasababu wengi hawaelewi lugha

Naamini Kabisa Mziki wa Tanzania Na Afrika Mashariki Kwa ujumla Bado Una safari ndefu sana Kwasababu Ya lugha Ya Kiswahili! Ni either Waache Kabisa Kuimba Kiswahili waimbe Kwa kingereza Au wasubiri kiswahili kienee Duniani Kote ndio mziki wetu Utafika Mbali! Hata Ikitokea Diamond Akaimba kwa kingereza basi Matamshi yake Hatakiwa vizuri kwasbabu sio Lugha anayo ituma mara kwa mara! Ndio maana Diamond anatumia Gharama Kubwa sana Kufanya Collabo na wasanii wa nje ya Tanzania Ili kufikisha Mziki wetu mbali kwasababu ya Lugha ya kiswahilii! Ukweli ni kwamba Kwa msanii Yeyote yule wa Tanzania ili mziki wako Ufike nje Ya afrika Mashariki Unahitaji Kufanya Collabo za Kimataifa nyingi kadri uwezavyo..... Kinacho mfanya Alikiba Asiwe Wa kimatafita ni kwasababu Ya ufinyu wa Kolabo za Kimataifa hivyo watu inakuwa ngumu Kuelewa Kishwahili/Lugha Inayo Imbwa

LUGHA YA KISWAHILI NI JANGA KWA MUZIKI WETU

Ni mtazamo Tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi zile lyrics anazoimba kwa kiswahili.. unaona aki translate kuwa za kimombo bado watu watasikiliza na kufurahia.. haswa zenye kuimba juu ya kutendana tendana tu anazotoa sana na wenzaketangu mwaka jana?
 
Mtoa mada. Unaposema miaka 5 nyuma Diamond na kina Davido walikuwa wanawiana. Je, alikuwa anaimba kwa lugha gani?
In short. Diamond ndo bado tena, hapa bongo tu anafunikwa na madogo kibao.... mwambie aendelee tu kunyegeka
 
Dah ingekuwa hivyo akina Franco Luambo Makiadi, Bongo man, Koffi Olomide n.k tusingewaju maana hata sielewi wanaimba nini ila miziki yao naipenda balaa...
Kupitia mifano uliyoitaja, inathibitisha kuwa bandiko lake halina uhalisia, ni kama porojo tuu hakuwaza wala kukumbuka na kujisahihisha kabla ya kuamua kuandika.

Watanzania wengi tuu wanapenda nyimbo za kizungu iv ndio kusema wanaelewa kinachoimbwa la hasha pengine ni wachache tuu ndio wanaoelewa kiimbwacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani umefinya sana ktk kiwango cha kufikiri kuhusu lugha na wasani!!

Ungejiuliza maswali kwann kina Koffi Olomide had sasa miiziki yao inatisha??? Je uliwahi kuwasikia Mbilia Bell,Kanda Bongoman , Madilu, Awilo,je umejarbu kuangalia influence ya lugha na muziki ikoje!??? Je Makhirikhiri nao unawajua???

Wote hawa wameimba nyimbo kwa lugha zao lakn hadi sasa nyimbo zao zikipigwa hata wa kiingereza chako haufui dafu

Tunakariri maisha ndg Lugha haina mahusiano kabsa na ulichokisema ...ndio maans watu kama ww mnakuta mnamshangaa mtu hajui kiingereza lakn ni msomi

Sent using Jamii Forums mobile app

MakhiriKhiri Unawasikia Siku hizi?
 
Ojolegba wa wizkidayo naukubali kinoma lakini sielewi anaimba kitu gani.

Kina Sarkodie wanaimba sijui vitu gani lakini ni moto wa kuotea mbali. Mziki mzuri ni zaidi ya lugha ndiyo maana Gang nam style ya kikorea ilitikisa YouTube

Sent using Jamii Forums mobile app

Haukuwa Wimbo Ilikuwa Style Ndio maana Style Ya ngororo Ya Diamond Isambaa lakini Ojolegba Ya Wizkid Inaeleweka sana Kuliko Kamwambie Ya Diamond
 
Umefikiria juu juu sana ndugu...

Unamjua jamaa mmoja kutoka korea kusini anaitwa PSY!!!!
Mwaka 2016 kama sikosei, alitoa hit song yake iliyokwenda kwa jina la GANGNAM STYLE. Aliimba kwa lugha yao ya korea na alifanikiwa kuhit dunia nzima ilhali hakuna aliyeelewa lugha yake. Gangnam style ina viewers billion+....
Mziki ni feelings

Sent using Jamii Forums mobile app

Kilicho Mtoa Haukuwa Wimbo Ilikuwa Style yake Sahizi Unamsikia Tena?
 
Waliimba kwa kifaransa mataifa kibao africa yana zungumza kifaransa, Diamond mjanja sana aisee ana ngoma yake inaitwa wakawaka imekuwa banned hapa bongo ila inachezwa U.S jamaa kajitahidi kulenga japo kiswahili kinatuangusha sana.
Vipi Bongo tunaongea Kifaransa?!
 
Mataifa mengine kama South Afrika wanapambana kutumia kiswahili halafu mswahili anapambana kutumia kizungu
 
Pia mwambie aache kuimba matusi maana kila nyimbo wao lazima wahusishe ngono

Sent using Jamii Forums mobile app
Pale los angels ndo mahali ambampo maburudisho yote ya dunia yameasisiwa....na kuna nguzo tatu za maburudisho, kila anayefanya entertainment na ili afanikiwe kwa kiwango chake lazima ahamasishe nguzo moja au mbili, au zote tatu...nguzo hzo ni Ngono (mapenzi), Mauaji na Ushirikina...bila kufanya hvo hutoboi unless ufanye God related Music
 
Ni upuuzi kwa mwanamuziki wa kiafrica jujitutumua kwa Kiingereza na kutegemea kutusua kimataifa. Ni kutafuta kudharaulika tu. Lugha za kiafrica ni nzuri kimuziki. Fuatilia vizuri ninachomaanisha na utanielewa.
 
Sema hakuna sehemu ya ku like mara mbili.
Nadhani umefinya sana ktk kiwango cha kufikiri kuhusu lugha na wasani!!

Ungejiuliza maswali kwann kina Koffi Olomide had sasa miiziki yao inatisha??? Je uliwahi kuwasikia Mbilia Bell,Kanda Bongoman , Madilu, Awilo,je umejarbu kuangalia influence ya lugha na muziki ikoje!??? Je Makhirikhiri nao unawajua???

Wote hawa wameimba nyimbo kwa lugha zao lakn hadi sasa nyimbo zao zikipigwa hata wa kiingereza chako haufui dafu

Tunakariri maisha ndg Lugha haina mahusiano kabsa na ulichokisema ...ndio maans watu kama ww mnakuta mnamshangaa mtu hajui kiingereza lakn ni msomi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna asiyemfahamu J Balvin na Anitta kwa nyimbo yao ya Safari.
Nani hakutikisa kichwa wakati Despacito inapigwa?!
Don Omar kibao chake cha Danza Kuduro wapi haikufika?!
Bad Bunny na Becky G - Mayores imesikilizwa na kutazama zaidi Africa baada ya Latin America (Africa ni Mataifa mangapi yenye kuzungumza Spanish?)

Lugha sio sababu.
 
Muziki ni zaidi ya lugha, kuna nyimbo kibao za Kiswahili zilizo maarufu mpaka Latino Amerika. Mwanamuziki Saida Karoli nyimbo zake zapigwa sana huko Latin Amerika ktk club na vilabu. Mfano huu hapa :

Como Bailan Saida Karoli Tanzania

 
Back
Top Bottom