Jinsi Koneksheni inavyoweza kurahisisha jambo lako

Jinsi Koneksheni inavyoweza kurahisisha jambo lako

De Opera

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
780
Reaction score
1,664
Habari za muda huu Mpwa!

Ni siku nyingine tena tunakutana katika kuangalia yale mambo kadha wa kadha ambayo yanagusa maisha yetu.

Mpwa, leo nimekuja na jambo moja tu ambalo ndio limekuwa muhimili wa sasa katika maisha ya leo yaani 'Connection'.

Ni neno la kawaida sana ukilisoma na kulitamka kwa kinywa, lakini hapa mjini bila hilo hutoboi kirahisi.

Uwe unatafuta kazi, eneo kwa ajiri ya biashara, mkopo, na mambo mengine mengi tu. Kama hauna koneksheni ni bahati kufanikiwa.

Sasa leo nataka nizungumze jinsi ya kitengeneza hiyo koneksheni.

Uswahilini hapa tunasema kuwa na mtu au kitu ambacho kinaweza kukusaidia ukafanikiwa kupata jambo lako kirahisi bila mbambamba.

Koneksheni inaweza ikawa ni Nduguyo, Rafiki yako au Pesa. Inategemeana na nini unahitaji na kipo katika mazingira gani. Kuna koneksheni zingine zinahitaji mtu na pesa na zingine zinahitaji wasiliano mazuri na watu unaoishi ama kukutana nao.

Mfano nikizungumzia katika suala la ajira. Wewe ni kijana umehitimu tayari kwa kuingia mjini kutafuta ajira mahali fulani. Unaweza ukatembea na vyeti vyako siku nzima, na kesho ukarudi, na kesho kutwa hadi mwaka unaisha hujapata kazi, mwisho unaamua kukaa tu. Inauma sana.

Lakini ukiwa na koneksheni mambo yanakuwa ni chapu chapu tu, utasikia kesho njoo ofisini asubuhi. Ndio maana, wafanyakazi maofisi ni wale wale tu wa zamani. Hata akitoka ofisi moja anao uwezo wa kwenda ofisi nyingine na 80% akapata kazi. Ni kwa sababu tu ameshatengeneza koneksheni. CV ni kitu ila si kitu kama huna kitu!

Nikiachana na hiyo, narudi hapa mjini ambapo sasa ndio napigilia msumari.

Kumekua na kasumba ya watu kuchukuliana poa awali ila akipata shida ndio anakutafuta.

Hiyo ipo na imezoeleka kabisa. Unaweza ukampa mtu mchongo akaupuuza kwa sababu kuna mahali anategemea. Kule pakifeli ndio anakuja anakuulizia vipi ule mchongo bado unaendelea?. Nitafutie baasi kazi yoyote huko!

Mpwa, hapo tayari ulishaua koneksheni.

Hata kama una kazi au kuna mchongo unausikilizia, jaribu kuwa na lugha tulivu na uutunze mchongo ulioletewa ili hata ukifeli kule unakuwa kidogo na uhakika wa huku.

Lakini sasa unakuta mtu mwingine unaweza mpigia simu hata hapokei anaiangalia tu huku akijisemea 'Hili nalo lisumbufu, kwani mimi tu ndio nafaa?' , unatuma sms hajibu halafu baadaye mtu huyo huyo anakuja kukuambia maisha magumu, mtafutie kazi yoyote.

Kiukweli, koneksheni ni watu, kiburi hakina hela, hela ni zako. Jaribu kuongea/kuwasiliana na watu vizuri. Jenga urafiki, jenga ukaribu. Usisubiri shida ikufike ndio uwakumbuke watu.

Zungumza vizuri na majirani. Unapita mwezi hamjasalimiana hata kujuliana hali na wakati upo tu nyumbani.

Ongea vizuri na marafiki na watu wote unaokutana nao katika harakati za kimaisha. Sio uko kwenye usafiri unaweka earphones masikioni kumaanisha hutaki kuongeleshwa na mtu si ndio?

Mpwa, mimi naishia hapo usije kuninyima maji ya kunywa, ila shikilia hicho nilichokuambia.

Tengeneza connection. Hela ukose, na watu pia ukose?

'De Opera' au deoperacc kwenye mitandao ya kijamii napatikana.
Blogu yangu: De Opera Hub
Uwe na siku njema.
 
Mpwa umenena ya busara mno, watu walipaswa walipie uzi huu kama wanaelewa nachosema!
 
Haloooo kweli.... Me saizi natengeneza connection na siyo marafiki
 
Back
Top Bottom