Jinsi madalali wanavyonufaika masokoni

Jinsi madalali wanavyonufaika masokoni

Jamaa mmoja alifika sokoni na mchele gunia 180 za kilo mia kila moja.

Akatokea dalali mmoja akaja kama mteja. Wakaanza kupatana bei mpaka ikafika 1700 kwa kilo bei ya jumla.

Dalali akalipa cash 1700x180x100 = 30.6m. Jamaa akachukua mkwanja akasepa.

Dalali akaunadi ule mchele kwa 1800 akapiga 1800x180x100 = 32.4m.

Hapa alinufaika kwa 1.8m.

Ushauri wangu. Kwa wanopeleka mizigo sokoni tuwe wavumilivu. Ukienda na pupa za kuwahi kuondoka utajikuta unauza bei ya hasara afu dalali anapiga ela ndefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Madalali kuwa by pass inahitajika nguvu ya ziada. At least mchele unaweza kuvumilia, je ikiwa perishable goods kama nyanya itakuwaje? Na hata huo mchele unaweza kuvumilia ukaishia kuingia gharama zaidi kwa ajili ya ghari. Na wanunuzi wameshajizoesha kununua kwa dalali. Kuwaondoa madalali yajitaji ubunifu wa hali ya juu. Huyo aliye nunua ka hela yake si dalali. Dalali hatoi hata senti yeye kazi yake kukulink na wanunuzi halisi halafu anapata cha juu.
 
Mkuu labda mimi sijaelewa kwani jamaa ako kuna mtu alimshikia bunduki kukubali ofa ya madalali??
Madalali wameleta ofa unaona haikulipi hupati faida unaachana nao unatafta njia nyingine.
Mimi sioni shida hapo kwa madalali jamaa ako ndo miyeyusho kukubali ofa ambayo haimlipi afu anakuja kulalamika.
Au wewe ulitaka dalali anunue mzigo wa jamaa na kuuza pasipo faida??
Negotiations skills ni kitu cha msingibsana kwenye biashara jamaa yako alifeli hapo na yeye ndio wa kulaumiana na sio madalali.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unapofanya biashara angalia umewekeza gharama kiasi gani,muda na faida yako..basi mengine hayo hayana maana
 
Dalari/madalari Wanaumuhimu Mkubwa Sana, Ni Halari Yao Kupata Faida Kubwa, Na Kuwaondoa katka mnyororo wa thamani ni haiwezekani! lakni ,the best way is to replace them by digtizing the value chain,only technology can change the lose-lose to win-win situation btn producer and consumer, kwa sasa si mkulima wala mlaji anaye nufaika na kilimo, mazao yananuliwa kwa bei ndogo kwa mkulima, yanauzwa bei kubwa sana kwa mlaji, hali inayopelekea wote mdhalishaji na mlaji wakose faida, ni kazi kwetu wajasiliamari kuleta teknolojia itakayopunguza/kutoa hii changamoto, ninazo idea mbili za kuondoa hii changamoto na pia kwenye kada ya sheria muda ukifika nitashare nanyi to partner , urgent digtization is needed in both agriculture and law , let techology lead the way we want
 
Hapa huwa sielewi,unapomkabidhi dalali mzigo,huwa kuna kuandikishana au ni kienyeji?,dalali hawezi kudhulumu mzigo wa mtu?
 
Hapo bado sijaona ubaya,wameelewana sasa huyo mkulima angetaka kuuza mwenyewe huo mzigo angekaa nao mwenyewe,Maisha ni kutegemeana kama ivyo kumbuka hapo iyo hela aliyochukua dalali hata makuli wa kushusha wamepata riziki yao
 
Mkulima mahesabu ya faida inabidi uyafanye tokea unapanda mazao yako, hya mambo ya kusubiri mpaka ufike sokoni ndyo ujue faida yako siku zote utakula za uso

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndo maana inatakiwa kama biashara zako mfano ni kuuzia dar,at least ukodi chumba hata kwa miezi mitatu,sio unafanya biashara huku una presha za gharama za gest
 
Back
Top Bottom