Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 1,964
- 3,496
Na uzuri wenu mmenyooka hamna mambo mengi, cha msingi tu ni kutimiza job description inayonihusu basi.Kuna kina sie hapo 35 na kuendelea hatutaki mchezo,,!!!!
Tunajua kabisa huyu mwanaume Yuko kwangu na kazi yake ni ipi???!!!
Kama baba uwe baba bora maana ninachohotaji ni baba bora si bora baba...
Kama ni mpenzi na huna hela ujue kabisa una cha kunipa ambacho nitaridhika nacho maana hela huna.
Kama ni danga una hela basi unipe hela kweli sio vilaki laki maana wewe una hela tu na huna kingine cha kunipa ambacho kitanipa furaha zaidi ya hiyo pesa.
Kama ni mpenzi na tunaringana kipato basi tupeane mapenzi mahaba bila kusahau kupeana pesa maana ndivyo vitu vinanogesha penzi letu.
Na kama ni wapenzi wale tusio na kitu basi tuenjoy penzi letu la kimaskini yaani mwendo wa kubebana, kuogeshana chumba limefungwa lock saa 24 ni mahaba tu yasiyo na usaliti maana maskini kuchit kwake ni msamiati wa kireno.
Mpewe maua yenu.