Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Ni Hesabu ndogo tu...
Gharama za Uzalishaji zikiwa kubwa basi na Bei ya Mtumiaji itaongezeka;
IKIWA MZALISHAJI NI UMMA;
Gharama za Uzalishaji zikiwa kubwa sababu Nishati ni Huduma huenda ikatolewa Ruzuku kupunguza hizo gharama au Mteja hana jinsi lazima atatumia tu
IKIWA MZALISHAJI NI BINAFSI
Kuna kipengele cha Faida kitaongezeka katika gharama za Uzalishaji sababu mtu Binafsi lazima apate Faida (na hata kama faida hio haitapatikana kwenye Bei lazima itapatikana kwa njia ya Ruzuku / Kodi za Mwananchi)
BEST CASE SCENARIO
UMMA Kusambaza umeme na kuzalisha pia lakini kama kuna mtu / kampuni binafsi inaweza kuzalisha kwa BEI NDOGO kuliko UMMA basi UMMA wanaweza kununua na kuwasambazia wananchi hii ndio best Case Scenario ila kinachotokea ni tofauti....
MFUMO WA ULAYA
Pamoja na mifumo mingi na rafu nyingi zilizotokea tangia Thatcher alivyobinafisha Nishati ila kwa sasa kuna mfumo ambao Nishati inanunuliwa kutoka kwa wazalishaji tofauti..., Bali Bei inapangwa kutokana na Bei kubwa kutoka kwa wazalishaji tofauti...; mfano hata kama wewe unazalisha kwa kutumia Jua, na kuna mwenzako anatumia makaa ya mawe na mwingine gesi na mwingine petroli; hapo wataangalia kama petroli ndio bei kubwa zaidi wazalishaji nyote mtalipwa bei ya Petroli; Kinachotokea Ulaya ndio kimesababisha Umeme / Nishati kuwa na Gharama kubwa sana..., Pamoja na hayo Political Decisions, Mfano Germany ilikuwa inachukua Gesi kutoka Russia matokeo yake shinikizo la NATO limepelekea kuwa mtumiaji mkubwa na muagizaji wa LNG ambayo ni Gharama (kwahio kuna wanaonufaika hapo ila sio Mjerumani)
South Afrika (Kampuni ya Umeme kununua Mafuta Ghafi kutoka kwa Madalali)
Hii ilitokea kipindi cha mgao Afrika Kusini, kuna watu walitengeneza mirija yao wakawa mtu kati wanaagiza mafuta toka nje na kuuzia Kampuni ya Umeme ya UMMA kwa Bei maradufu (wato hao ilikuwa ni siri kuwatambua ni kina nani na ilikuwa Siri hata kusema Bei wanayochaji ni Kiasi gani)
SECI INDIA
Hii ni Kampuni ya renewable energy ya India ila ndio hivyo hawa wanafanya kazi kama mtu kati pia na ndio walioingia Mkataba na Adani wa kuweza kuhonga viongozi na kuwapa tender na kugawana cha juu; mwisho wa siku gharama hizo za kupeana cha juu ni mtu wa mwisho ndio atapata shida
BANGLADESH
Hawa walikuwa na surplus ya uzalishaji wala hawakuhitaji uwekezaji ila walimuita Adani ili asaidie kuongeza uzalishaji kilichotokea ni Umeme kupanda maradufu kwa mtumiaji
ENRON USA (MAREKANI)
Hawa jamaa walifanya lobbying mpaka kwa Rais wa USA George Bush ili kubadilisha Sheria za Regulations; kilichofuatia ni kupika vitabu na kuanza ku fanya inside trading ya Umeme kwenye Stock Exchange;
Kilichofanyika sababu California kama state ilikuwa na sheria zake na ingeweza kununua umeme kulingana na bei kwa wazalishaji tofauti Enron walikuwa wanapanga na wazalishaji kuzima umeme na kusababisha blackouts, wakijua kabisa kama kuna mgao basi bei za umeme zinapanda hivyo wakawa wanakata Umeme kimakusudi wakijua Bei zinapanda wanauza Hisa na baadae wanazima Bei zinashuka wananunua Hisa in Short walikuwa wanafanya Betting kwa mgongo wa Maisha ya watu....
HITIMISHO
Tupime mafanikio ya Sekta ya Umeme kwa affordability kwa Mteja na Upatikanaji na sio vinginevyo.., Hili jambo ni simple sana tunavyolifanya complicated ndio tunaweka mianya ya watu kuiba...
www.jamiiforums.com

Jinsi ya kuifanya Kampuni ya Tanesco kuwa Kampuni Bora na ya Kujivunia Tanzania na Afrika kwa Ujumla
Tanzania tumebarikiwa vyanzo vingi vya nishati, Na Tanesco ni kati ya Makampuni mama ya Tanzania ambayo yanaweza yakaitangaza nchi yetu Africa na Pote Duniani (Yaani mfano wa kuigwa) Sio tu kutupatia nishati hapa bali tuweze kuwapa hata majirani zetu na kutuingizia fedha badala ya sasa kutumia...