Kwanza kabisa niseme mimi ni mtazamaji mzuri wa mipira ya uwanjani (Na hata leo niko uwanjani kwa mechi ya Alliance na Yanga) . Kitokana na kuhudhuria huko nimebaini kuwa timu mwenyeji za Mwanza zinahujumiwa sana kwa kukosa mapato mazuri ya viingilio hasa kwa mechi kubwa zinazohusu Yanga, Simba na hata Azam kwa namna mbili.
Moja wahusika wa kuuza tiketi wanasababisha foleni kubwa maksudi na wakati mwingine kutangaza kuwa tiketi zimekwisha wakati ukiingia uwanjani hata robo ya uwanja haijajaa. Katika kufuatilia nimegundua wanaouza tiketi hufanya udalali kwa kuwapa vijana tiketi na kuziuza nje ya uwanja kwa bei kubwa, hivyo kukatisha tamaa wadau kuingia uwanjani kwa mfano :Leo Alliance na Yanga Mzunguko kiingilio ni Tsh 5000/= lakini kwa udalali zinauzwa Tsh 7000'=
Mbili wanaosimama mlangoni kuchukua tiketi wanabaki nazo wakidai kuzichana, lakini ukiwa makini nyingi hawazichani hubaki nazo na kuziuza nje tena. Hata hivyo inashangaza mi ninavyojua tiketi ni mali yangu hivyo ninastahili kubaki nayo.
Kwa ushauri wangu naona tiketi ziwe zinauzwa siku mbili au moja kabla katika vituo maalumu badala ya kuanza kuuzwa saa tano uwanjani. Pia mashabiki waachiwe tiketi zao na ziwekewe alama wanapoingia uwanjani.
Nawakilisha