Jinsi mapato ya timu yanavyoathirika wakati wa mashabiki kuingia uwanjani katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza

Jinsi mapato ya timu yanavyoathirika wakati wa mashabiki kuingia uwanjani katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza

Big gun

Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
31
Reaction score
39
Kwanza kabisa niseme mimi ni mtazamaji mzuri wa mipira ya uwanjani (Na hata leo niko uwanjani kwa mechi ya Alliance na Yanga) . Kitokana na kuhudhuria huko nimebaini kuwa timu mwenyeji za Mwanza zinahujumiwa sana kwa kukosa mapato mazuri ya viingilio hasa kwa mechi kubwa zinazohusu Yanga, Simba na hata Azam kwa namna mbili.

Moja wahusika wa kuuza tiketi wanasababisha foleni kubwa maksudi na wakati mwingine kutangaza kuwa tiketi zimekwisha wakati ukiingia uwanjani hata robo ya uwanja haijajaa. Katika kufuatilia nimegundua wanaouza tiketi hufanya udalali kwa kuwapa vijana tiketi na kuziuza nje ya uwanja kwa bei kubwa, hivyo kukatisha tamaa wadau kuingia uwanjani kwa mfano :Leo Alliance na Yanga Mzunguko kiingilio ni Tsh 5000/= lakini kwa udalali zinauzwa Tsh 7000'=

Mbili wanaosimama mlangoni kuchukua tiketi wanabaki nazo wakidai kuzichana, lakini ukiwa makini nyingi hawazichani hubaki nazo na kuziuza nje tena. Hata hivyo inashangaza mi ninavyojua tiketi ni mali yangu hivyo ninastahili kubaki nayo.

Kwa ushauri wangu naona tiketi ziwe zinauzwa siku mbili au moja kabla katika vituo maalumu badala ya kuanza kuuzwa saa tano uwanjani. Pia mashabiki waachiwe tiketi zao na ziwekewe alama wanapoingia uwanjani.
Nawakilisha
 
Hill liko wazi..na cha kusikitisha sio kwamba hawajui,wanajua ila kwa vile kuna watu wananufaika na huo mfumo ndio maana wako kimya.
 
Hujuma ya Kwanza inaitwa Ulanguzi wa Tiketi,hufanyika dunia nzima,hata wenzetu ulaya imewashinda,kitu bora unaweza kufanya ni kuboresha uuzaji ikiwamo tiketi kuuzwa mapema kama ulivyopendekeza,ulaya watu wananunua tiketi za msimu mzima,lakini walionunua wakiamua kuuza kwa bei ya juu huwezi kuzuia

Hujuma ya pili inahitajika uwekezaji wa mifumo ya electronic ambazo mashine ndio zinakuruhusu upite na kuifanya tiketi itumike maramoja tu, TFF imeshatoa tender kwa wawekezaji ni vile bado wawekezaji wanajihusisha ktk game kubwa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makomandoo wanakuchora tu. Hizo ndizo dili zao hizo miaka nenda. Mchakato wa kufunga hizo mashine za kielektroniki ulipamba sana wakati ule wa Malinzi halafu ghafla tu ukazima kama mshumaa.
 
Back
Top Bottom