Jinsi mapenzi yalivyofanya ufalme wa Egypt/Mizraim kuanguka na kusambaratika

Jinsi mapenzi yalivyofanya ufalme wa Egypt/Mizraim kuanguka na kusambaratika

Halafu mwanamke mwanyewe (Cleopatra) alikua wa kawaida tu ila watu walikua wanavunjana miguu kumkimbilia.
Btw kila mwanamke ni mzuri machoni pa mwanaume aliyemtamani.
Cleopatra was too far hyped
Technology ya Picha ilikuwepo enzi yake!? Ili tuone alivyokua wa kawaida!?
 
Technology ya Picha ilikuwepo enzi yake!? Ili tuone alivyokua wa kawaida!?
Haikuwepo, ila teknolojia ya uchoraji na uchongaji (Sculpturing) ulikua upo juu kwa kiasi kikubwa
 
Tukiachana na kichwa cha mada na hitimisho lake, hii mada ina mambo mengi ndani yake ambayo yanaweza kuzaa mada nyingi sana.
Nimevutiwa na hio ya wajeisuit kumiliki karibu vitabu vya maarifa vyote vya dunia.

Ila hakuwa na wasiwasi na upeo wa maarifa kwa wanazuoni wa kikatoliki, lau kama wangekua na upana wa maarifa au tuseme wangekua na elimu juu wasingingekuwa wanafanya vitu vinavyo onekana vya kijinga kama kuabudu sanamu nk.
Umeanza vizuri ila mwisho umeharibu mkuu, Wakatoliki hawaabudu sanamu. Nataka nikueleze kuha hatuabudu sana kwa njia ya maswali.. naomba ujibu maswali yafuatayo Tafadhali
1: Kuabudu ni nini??
2: Hatua za kuabudu ni zipi?? (Zitaje)
Ukishindwa kuzitaja basi kanisani kama unaenda hua unaenda kutembea tu.
Lets roll.....
 
Kwenye uchongaji vinyago kuna kinyago cha queen mmoja wa Misri anaitwa Nefertiti ni mrembo sana lakini hajasifiwa urembo wake.

download (3).jpeg
 
Ile kofia iliitwa Double Crown Iliunganisha kofia nyeupe ya Upper Egypt na nyekundu ya lower Egypt. Ila mimi kofia ninayoipenda ni ile inayoitwa Nemes ipo poa halafu inaswagger kama msemavyo vijana.
Wamisri ilitakiwa watuabudu maana sisi (Ziwa victoria) ndio chanzo cha. maendeleo yao.
Lakini Wakazi wa mwanza mbona wananuka umaskini??😄View attachment 2010658
Mbona wabantu hawa?? any way wewe ungeanza na dada zako wa Bukoba walivo choka !! wewe unarukia Mwanza mbaali kule tena kusini mashariki mwa ziwa? mkuu kweli? hiyo moja

pili ni kuwa Cleo patra alikuwa Mweusi tii!! kwa sababu vitotovya kigiriki ilikuwa ni marufuku kuongea Kimisri!! sababu tu ya ubaguzi!! cleopatra alizaliwa na mmoja ya wafanya kazi wakalimani mweusi kwenye Kasri la Ptolemy!! kwa sababu ya uzuri wake kakawa kantumiwa kukalimani mambo ya kifalme!

na wakati ule warumi waliamini Weusi wana akili mingi sana!! ivo wakasisitiza sera ya kuoana, kabla mfalme alexander hajakufa ndo ulikuwa mpango wao ili wapate ilimu ya kutosha wakajenge ma pyramids km yale ya Misri nchini mwao Macedonia!

Vijana wa Ptolemy wakamfanya Cleopatra kuwa mkalimani kati yao na wamisri sababu alizaliwa huko kwenye Castri la Mfalme!! siyo kwamba watawala wa wakati huo hawakutaka kuongea Ki-Misri coptic language no!

walitaka sana ajili ya kubeba maarifa ya kule misri na kuyapeleka kwao! ila tatizo hawakujua kirahisi ilE LUGHA ya wamisi! pia ilifika mahali wamisri hawakuwapenda watawala wale! kwa sababu ya ukatili wao!
 
Mbona wabantu hawa?? any way wewe ungeanza na dada zako wa Bukoba walivo choka !! wewe unarukia Mwanza mbaali kule tena kusini mashariki mwa ziwa? mkuu kweli? hiyo moja
Hahahaaa mimi sio wa BK mzee
pili ni kuwa Cleo patra alikuwa Mweusi tii!! kwa sababu vitotovya kigiriki ilikuwa ni marufuku kuongea Kimisri!! sababu tu ya ubaguzi!! cleopatra alizaliwa na mmoja ya wafanya kazi wakalimani mweusi kwenye Kasri la Ptolemy!! kwa sababu ya uzuri wake kakawa kantumiwa kukalimani mambo ya kifalme!
Hii mpya kwangu, kwamba Cleopatra alikua mweusi?? Sidhani. Ni kweli wagiriki walikua hawaruhusiwi kujifunza kimisri but hakuna fact inayoonyesha Cleopatra alikua mweusi
na wakati ule warumi waliamini Weusi wana akili mingi sana!! ivo wakasisitiza sera ya kuoana, kabla mfalme alexander hajakufa ndo ulikuwa mpango wao ili wapate ilimu ya kutosha wakajenge ma pyramids km yale ya Misri nchini mwao Macedonia!
Nakubali kua wamisri walikua weusi ndio na mchamganyiko umekuja kuyokea baada ya warabu kuingia na kuzaliana na weusi
Vijana wa Ptolemy wakamfanya Cleopatra kuwa mkalimani kati yao na wamisri sababu alizaliwa huko kwenye Castri la Mfalme!! siyo kwamba watawala wa wakati huo hawakutaka kuongea Ki-Misri coptic language no!
Nijuze zaidi hapa mkuu
walitaka sana ajili ya kubeba maarifa ya kule misri na kuyapeleka kwao! ila tatizo hawakujua kirahisi ilE LUGHA ya wamisi! pia ilifika mahali wamisri hawakuwapenda watawala wale! kwa sababu ya ukatili wao!
Ni kweli lugha ya kimisri ilikua ngumu sana... Ila nado siamini uweusi wa Cleopatra
 
Alooo Da'Vinci asimwambie mutuu Cleopatra alikuwa mxuri sana watu wanadai alikuwa akioga kwenye maziwa ya ngamia.
Hiyo library ya Roma ni hatari na nusu humo ndo kuna vile vitabu vingine vya biblia vilivyo pigwa ban, na baraza moja wslilokaa waroma. Unakuta mkristo tofauti na mromani anadhani anajua Bible kuliko Waroma! Heheeee... Yaani watu waliochagua hiki kiende uraiani hiki kisiende.
Nikurekebishe Kidogo, Vitabu vya biblia havikupgwa ban bali vilichambuliwa na kuwewa kando vingi vinatumika kama mapokeo vingine havifiki kabisa kwa waumini maana vinaweza kutuvuruga. Ndio maana Wakatoliki sio wajinga kuruhusu picha ya yule mtu aliyeko makanisani kua ndio Yesu. Wanajua wanachofanya coz wana docs zote.
 
Hapa Mkuu nacho jua ni kuwa Biblia, na kanisa la kwanza kabisa la Yesu wa kweli vilipigwa marufuku na Mfalme Constatine!! tena matani na matani ya Biblia yalichomwa moto! lkn kadri ilivopigwa marufuku ndo ilizidi kuonekana zaidi!!

mpaka leo wataalamu wanagundua Biblia zile za mwanzo kabisaaa!! mfano hapa juzi juzi wamepata Dead sea scrow Bibles! hizi zilikuwa zimefichwa huko kwa usalama zaidi na wafuasi kindaki ndaki!! kufuatia agizo la Mfalme constatine! zikasahaulika huko!! na hata uki-google humu zimo!

Baadhi ya vitabu vimepigwa marufuku mpaka leo mfano ''Apocryphas'' sababu kubwa ya kupigwa marufuku ni kwa sababu vinamuonyesha mtu mweupe kuwa ni Nephilms! kisayansi wanaitwa Neandethals!!

Duniani ni mweusi tu asiye kuwa na vinasaba vya Neandethals! weupe wote wanavyo! kwa nini? Biblia haitaji Neandethals kwa nini? vile vile sayansi haitaji Nephilims why? ukiangalia vizuri Nephilims na Neandethal kihistoria wanaenda sambamba! ni hao hao kwa sababu nakupa mfano tu kidogo ;

Wote Neandethals mifupa yao ilipatikana imerundikana mabondeni mfano ni Giblatar Valley kwa nini ili rundikana huko? ? jibu walisombwa na maji!! ......maji gani ya hivi?? ...... mafuriko ya gharika!

Neandethal walipotea Ghafla japo walikuwa na stadi kubwa za maisha --vile vile Nefilims pia walipotea kwa gharika gahfla! na Biblia inasema walikuwa vizuri uwezo!
Kama Nephilims walikufa kwa gharika mabaki yao yako wapi?? mbona ya Neandethals yanapatikana!........jibu; ndo hao hao!

sasa ebu jiulize inakuwaje Maviumbe makubwa yenye uwezo maguvu yafe yaache viumbe vidogo wasiokuwa na miili mikubwa wala stadi za maisha lk wote ni binadamu! jibu ni Gharika!! uliwahi jiuliza hivi kabla ya ALEXANDER the Great hawa wazungu waliishi wapi?

Sababu Bara Ulaya lilifunikwa Barafu rupu siyo? toboa tu Yule kijana yesu Mzungu ndo yeye kweli? Bwana Davinci?? km siye kwa nini wamefanya vile?? na Yesu original ni yupi? hapa kuna kitu unajua ila unazunguka
 
Maelezo yako yana make sense ila mkuu hua mnanishangaza sana mnaosema Yesu alikua mweusi au binaadamu halisi ni mweusi. Kwangu sio big deal kabisa.
Halafu swala la gharika la nuhu lina utata sana siamini kama mvua ilinyesha dunia nzima
CC
Mathanzua
 
Neandethal walipotea Ghafla japo walikuwa na stadi kubwa za maisha --vile vile Nefilims pia walipotea kwa gharika gahfla! na Biblia inasema walikuwa vizuri uwezo
Biblia sometime inachanganya sana ina contradiction hawa Nefilims utawakuta katika vitabu vya musa na gharika kuwafuta. Cha ajabu unawakuta tena kwa wana wa Israel wanawakuta katika ile ardhi ya ahadi nadhani mwandish alichapia au namna gani.

Halafu swala la gharika la nuhu lina utata sana siamini kama mvua ilinyesha dunia nzima
Naungana na wewe gharika ina fikirisha sana
 
Hello...
Previous I wrote a topic centered on Greece and we discussed a bit about Egypt, So this Topic will be serving as a spin-off of that Topic. Will focus on Rise and fall of Egypt , Pharaoh's Dynasty Respectively

Baada ya gharika iliyoikumba dunia wakati wa Noah (Nuhu) watoto wake wakaanza kuzaliana. Ham alimzaa Mizraim (Misr) Misri alihamia eneo la kaskazini mwa afrika (NB. enzi hizo Mabara yalikua hayajagawanyika) kisha akaanza maisha eneo hilo, waliishi pembezoni mwa mto nile wakijishughulisha na kilimo watu wakazaliana na kuongezeka.

Watu walivyoongezeka wakaanzisha Ustaarabu (Civilization) na Tamaduni (Culture) zao wakachaguana viongozi wao kwa wao, Kulikua na misri ya chini (Lower Egypt) na misri ya Juu (Upper Egypt) Ila zote zilikua kitu kimoja. kwenye Lower Egypt ndio kulikua na miji mashuhuli kama Memphis nk. Wamisri walijaliwa akili nyingi sana katika kufikiria, walizitumia bongo zao vizuri sana katika kutatua shida mabalimbali zilizowakabili. Lakini huwezi kutaja maendeleo ya misri bila kuutaja mto Nile, huu mto umebeba dhima kubwa katika Mafanikio ya misri ya kale na ya sasa katika kila nyanja....Mto Nile ndio sababu kuu ya misri kua hivyo ilivyokua kipindi hicho, viongoz wao waliwaita Pharaoh.. waliwaheshimu,kuwaabudu na kuwaogopa kama miungu. maana wamisri waliamini mapharao huongea na Mungu (Mungu mkuu wa Misri huitwa Ra)

Miaka ikapita alizawa jamaa mmoja anaitwa Imhotep, huyu jamaa alikua ana akili sana sana, alikua ni kuhani mkuu/High priest wa Mungu Ra. alikua kabobea zaidi katika uhandisi wa majengo na Matibabu. pyramid nyingi unazoziona kajenga yeye kaandika maandiko mengi sana yanayohusu tiba na uhandisi
Misri ikawa misri katika ubora wake, miaka ikasonga mbele.

Mwaka 356 BC huko Ugiriki akazaliwa Alexander, alipoinukia baba yake akampeleka kwa Aristotle mwanafalsafa nguli wa kipindi hicho amfundishe hekima na matumizi ya akili katika kupanga na kutatua mambo, Alexander akaiva akawa very smart kichwani. baada ya miaka 16 muda wake wa kusoma ukawa umeisha siku moja baba yake (King Philip II) alienda vitani akamuacha Alexander kama ndio mfalme alinde ufalme. Wakati akiwa amebaki yeye kama mfalme kabilaona la
Thracian wakaasi wakataka kuanzisha vita na ufalme, Alexander akakusanya kikosi akawapa kichapo akafanya mjia wao kua Koloni lake na jina la mjia wao likabadirshwa na kua Alexandropolis.

Mengi yalitokea, alianzisha kupanua utawala wake kutoka huko Ulaya akaenda hadi Asia kisha akafika Misri.
Alexander alipanua himaya yake hadi kufika mirsi akawapa kichapo wamisri wakasarenda akachukua nchi. Kitu kimoja alichofanikiwa alexander ni kuheshimu na kufuata mila za sehemu anazotawala. Mfano alivyoichukua misri alitawazwa kua Farao wa Misri akawa aaweka muwakilishi wake halafu anasonga mbele kwenda kutanua himaya. Ila akirudi kwenye moja ya himaya zake anaheshimu mila zao na kuzifuata bila shida ndio maana alikua ana vyeo vingi sana

Enzi hizo Memphis ndio ilikua kitovu cha mirsi kila kitu kizuri kipo hapo kama nilivyoelezea sasa Alexander aliupend mji mmoja unaitwa Rhacotis akaubari jina ukaitwa Alexandria huu ulikua mji maarufu zaidi misri hadi mwaka 641AD walipokuja warabu kuivamia miri na kuufanya mji wa Fustat kua mji mkuu, Fustat ulibadirishwa ukawa unaitwa Cairo.

Sasa hapo Alexandria kulijengwa Maktaba ya kwanza duniani (World First Library) ambapo maarifa kutoka kila pemebe ya dunia yalikusaywa hapo. Alexandria ikawa kitovu cha dunia enzi hizo kama ilivyo NewYork sasa hivi, kila mtu ndoto yake ilikua kufika hapo Alexandria, wanafalsafa wengi na wanasayansi wengi wqliend kusomea hapo Alexandria... Daktar wa Kanisa Lucas ambae aliandika kitu cha Injili ya Luca nae amesomea hapo Alexandria.
Kiufupi Alexandria ilikua kitovu cha elimu duniani hadi wapuuzi wawili walivyokuja wakaharibu kila kitu.

Maisha yakazidi kusonga Alexander akafa 323 Ugiriki ikaanguka ikawa sio tena taifa lenye nguvu wala kutegemewa katika nyanja mbalimbali..Akaibuka mbabe Mrumi (Ufalme wa Rumi/a).

Wajinga wawili , Mapenzi kitovu cha uzembe.
Plotemy I Soter
Baada ya Alexander miaka kadhaa mbele (Mwaka 305BC) Moja kati ya majenerali waliokua nae huko mirsi alibadirisha mfumo wa utawala wa Misri akaibadiri misri kua Ufalme wa Plotemy (Plotemaic Dynasty) Waliweka sheria kua wafalme wanatakiwa kuyunza mila na desturi za nyumbani kwao Ugiriki (Makedonia) ili kutimiza hilo walioana wao kwa wao yaani kaka anamuoa dada au shangazi na ndugu wengine na walikua hawaruhusu kujigunza lugha wala tamaduni za wamisri.
Mwaka 69BC kadada kazuri kalizaliwa huko Alexandria Misri, kadada hako kaliitwa Cleopatra.

Cleopatra alikua anatoka kwenye huo ukoo wa Plotemy ila alikua anapenda kujifunza na kua na watu hivyo yeye ndio akawa wa kwanza kujifunza lugha na tamaduni za kimisri ndio maana wengi hua wqnadhani kua cleopatra alikua mmisri...inasemekana Cleopatra alikua anaongea lugha zaid ya 12 alipiga vitabu ipasavyo maana kalikua hapo Kwenye kitovu cha elimu duniani.

Kama kawaida Land alianation, forced labour, Huge tax, nk vilifanya waafrika tuwaimbize wakoloni basi na wamisri walipigwa Kodi ya kichwa hadi wakachanganyikiwa wakona hapa bila vita mura mambo hayaendi. wakaanza maandamano kumshinikiza Mfalme wa kipindi hicho ambae ni baba yake na Cleopatra atoke madarakani. Mfalme akaona mambo yameharibika akamchukua binti yake akakimbilia Roma, akaomba msaada arudi madarakani. Seneta ya Roma ikakubali kumpatia kiasi kikubwa cha fedha na wanajeshi akarudi misri akawapa kichapo waliochukua kiti cha ufalme akawa Mfalme tayari. Kama kawaida kukopa "sherehe kulipa matanga" mfalme alikosa pesa ikabidi arudise kodi kandamizi kwa wananchi ili alipe fedha za Watu hata hivyo ilishindikana alifanya madudu hapo hadi thamani ya pesa ikashuka kwa kiwango chan SGR.

Mwisho mzee akafa akaacha usia kwamba mtoto wake wa kiume na Myoto wake wa kike ambae ni Cleopatra ndio wawe watawala. Warumi hawakupinga wakaruhusu ila sheria ikawekwa kua pesa ilipwe na watakua wanalipa kiasi fulani cha dhahabu kwa mihula/terms. Sasa mpaka hapo Roma ikawa ina full control ya Misri, kama nilivyosema Cleopatra alipiga vitabu hasa hivyo alikia mjanja sana alikua mzuri kweye diplomasia, Alianza kutumia kila mbinu kuikuomboa nchi yake Misri kutoka kwa Warumi.

Chakwanza alianza kujipendekeza kwa bedui Julio Caesars akamdanganya dangaya Dikteta kashikika wakawa wapenzi mzee baba Kaisari akawa anajilia Mtoto mzuri with Classy Cleopatra. Hadi siku Caesars anachomwa visu na maseneta wake Cleopatra alikuwepo ikulu Roma wengine wanasema nae alishiriki kwenye njama za kumuua Julio Caesar ila uhusiano wao ulileta mtoto wa kiume aitwae Caesarion ambae nae alikuja kuwa mtawala wa Roma (?).

Bado mwanadada aliendelea kutumia uzuri wake kuwapagawisha viongozi wa rumi ili kutafuta jinsi ya kuikomboa nchi yake.

Second Triumvirate.
Baada ya maseneta kumuua Caesar walishindwa kukaa madarakani hivyo basi kiliundwa kikosi cha watu watatu ambao ni Gaius Ocatavian ambae alikua mtotowa Caesar wa kuasiliwa (Adopted), Mark Antony na Marcus Aemilius Lepidus.
Kuweka kumbukumbu sawa Huyu bwana Octavian ndio alikuja kuijiita Caesar Augustus (Kasiari Agusto) ambapo wakati Yesu anazaliwa yeye ndio alikua mtawala wa Yudea kwa kutumia muwakilishi wake ambae ni Gavana akaitisha watu wote waandikishwe yaani sensa ambapo Maria na Mumewe alihudhuria sensa hiyo huko Bethlehem kisha Yesu akazaliwa huko
usimachanganye na Tiberius. Caesar Tiberius Augustus (Kaisari Tiberio) huyu alimfuata Agusto ana alikua mwanae wa ku-Adopt (inaonekana waroma ndio ilikua kazi yao kuasili watoto)

Turudi kwenye mada.... Second Triumvirate
baada ya umoja huo kuundwa waliwashikisha adabu wote waliohusika kumuua Julio Caesar.
Sasa bwana Cleopatra kazama mapenzini na Marcus Antonius (Mark Anthony) yaani walipendana hadi Mark akamuacha mkewe Octavia amabe alikua dada wa Octavian/Agusto.

Mark Anthony akaagizwa aende misri kudai ile kodi ambayo watawala wamisri wanatakiwa wailipe Mark alipofika huko akazama penzini kwa Clepatra. wanakwambia Cleopatra alitumia mwaka mzima kula bata la nguvu (Luxury) na mpenzi wake Mark Anthony huku wakiwaacha wamisri/wananchi kwenye ufukara wa kiwango cha kabisa. Hawakuiahia hapo tu Mapenzi yaliwatuma kwamba ili wawe huru na penzi lao inabidi waivamie Roma waipige na kuichukua waendeleze kula bata la penzi lao.

Kule Roma taarifa zikamfikia Kaisari Agusto yaani aliyetumwa pesa kapewa penzi kanogewa kasahau kurudi lakini hajaishia hapo anapanga mbinu za kuvamia wenzake-Nchi yake kwa shinikizo la mapenzi/penzi la Cleopatra. Kaisari akaona dharau akatuma majeshi yakaenda misri yakagawa kichapo cha nguvu...Yaani Cleopatra na Mark walichapwa hadi wakakimbia wakajifungia ndani wakanywa sumu na kujiua. Octavian/Augusto alifika mwenyewe Alexandria na kuitawala hakuishia hapo kwa hasira alichoma ile Library/maktaba ya kwanza kujengwa duniani akaunguza kila kitu.. Ila hakua mjinga jamaa alibeba maarifa makubwa/Vitabu akahamishia Roma. Alexandria ukawa sio kitovu tena cha maarifa ulimwenguni hapo sasa ndio Rome ikawa kitovu cha maarifa.......ndio maana kwa kutumia tukio hili ndio maana kuliibuka wanafalsafa wengi wengi na watu wenye akili sana hapo Roma akiwemo Leonardo da vinci nadhani wengi mshasoma Renaissance. ambapo ilichagizwa pakubwa na tukio la Augusto kubeba vitu kutoka Alexandria kuja Roma. though hii fact hua wanaikataa wanasema kila kitu kilichomwa moto.

Cleopatra ndio Farao wa mwisho nchini misri...Japo historia inasema baada ya Octavian kuitawala misri anae alifanywa kua Farao

Baada ya Kaisari Constantine kufaya mageuzi makubwa sana kwenye kanisa la Kristo la mwanzo na kufanya kanisa hilo kuhamisha makazi kutoka Yerusalemu hadi Rome kanisa hilo lilichukua kumbukumbu na maarifa yote na kuyahifadhi mpaka leo hi. Jesuits wa Roman Catholic wamehifadhi kila aina ya maarifa kutoka pande zote za ulimwengu na kuzihifadhi Hapo Vatican ambapo ni moja kati ya sehemu ambazo ni haziruhusiwi watu kufika. Hata pope anaenda huko kwa sababu maalumu Labda Pope Francis aaweza kua anaingia Regularly kutokana naye ni mfuasi/member wa Jesuist.

Mapenzi ni matamu ila yasitufanye kusahau majukumu yetu kama hao wapendanao wawili Cleopatra na Mark Anthony.

Panapo majaaliwa I'll be focusing on different deities around the globe, Ares, Valkyrie,Jesus, Samson, Zeus, etc are slatted to appear and reprise their role as God of war, goddes, Masiah, judge respectively.

Mwisho...
Da'Vinci
-excelsior
Mtu mwenye akili timamu hawezi kusoma ujinga huu,kwa kuwa nia ya uzi ni ku-distract watu from real issues.Sijui CIA wanawalipa nini for this distraction.
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kusoma ujinga huu,kwa kuwa nia ya uzi ni ku-distract watu from real issues.Sijui CIA wanawalipa nini for this distraction.
Unanichekesha kwakweli serikali yako tu hapa haijui kama mimi nipi sembuse hao CIA. Mkuu hua hutaki kupingwa kwenye mada yoyote na ukipingwa unamshambulia mtu kwamba ni agent wa Shetani. That's not cool mate
 
Biblia sometime inachanganya sana ina contradiction hawa Nefilims utawakuta katika vitabu vya musa na gharika kuwafuta. Cha ajabu unawakuta tena kwa wana wa Israel wanawakuta katika ile ardhi ya ahadi nadhani mwandish alichapia au namna gani.
Biblia ina sema walikuwepo kabla na baada ya gharika Mwanzo 6;4 --- 1samwel 9,2. Kisayansi Weupe Duniani walitokea Cauccus Mountain!! wakatemka kusini mwa Dunia! hivo kwa muktadha huo tukapata neno Cauccasians!

Kwa nini Milimani huko?? bila shaka ndiko waliko ponea! km ujuavyo penye mpango wa Mungu shetani ana plan B'' yake! km haitoshi kuna yuleee!! mfalme Ogu wa Bashan!! ni mnefil pekee aliye pona gaharika!

kitu cha ajabu sasa Alexander the Great alipo pigana vita!! hakuelekea Kaskazini wala Mashariki bali alizichapa kuelekea kusini! Mashariki! ambapo palikuwa ndo penye Maendeleo makubwa Duniani wakti huo!!
 
FB_IMG_16342519392030782.jpg
 
The world on fire and you think all is forgiven?
I Don't look for forgiveness and I'm away past seeking permission
 
Wanawakuza warabu waliopo sasa na kuwabeza watu weusi waliokuwepo kufanya ustaarabu😢
 
Back
Top Bottom