Jinsi matapeli mamboleo hutumia mitandao na saikolojia kuliza watu

Joined
Jan 9, 2026
Posts
40
Reaction score
196
Matapeli wa kisasa ni wahandisi wa akili (psychological engineers) au manipulators . Hawaji kuiba pesa zako mara moja; badala yake, wanajenga mazingira ambayo wewe mwenyewe utawapa pesa kwa hiari yako.
Hivi ndivyo wanavyotumia saikolojia kumnasa mtu:

1. Kukuvutia na Maisha ya Ndoto zako (The Lifestyle Trap)​

Hii hutumika sana na wale wanaojifanya wana pesa nyingi au wapo vikundi fulani vya siri vyenye nguvu kama Freemason bila shaka mshakutana nao sampuli ya kina Nabii Shilla na Godlove. Hawa Wanatumia picha na video za:
  • Magari ya kifahari, rundo la pesa, na hoteli za gharama.
  • Lengo: Kutengeneza hisia ya upungufu (Inadequacy) ndani yako. Unaanza kuhisi maisha yako ni duni na unatamani kuwa kama wao. Hii inaitwa Social Proof" ukiwaona wanaishi vizuri, akili yako inakuambia "huyu anajua siri ya mafanikio.

Je wanawezaje kupata vitu hivi na kuvitumia kuhadaa

a. Picha na Video za Kuchukua Mtandaoni (Stock Footage)​

Hii ndiyo mbinu rahisi na ya gharama nafuu zaidi hawa ni wale wanaoanza lakini bajeti hairuhusu basi huingia mitandaoni na kutafuta picha zitakazokidhi story zao
  • Kupakua (Download): Wanachukua picha na video kutoka kwenye kurasa za watu matajiri wa kweli kule Urusi, Marekani, au Dubai na kuzipost kama za kwao.

  • Pinterest na Telegram: Kuna channels maalum ambapo matapeli hupeana picha za rundo la pesa, funguo za magari, na vyakula vya gharama ili kila mmoja akapost kwenye ukurasa wake.

b. Ukodishaji wa Muda Mfupi (The Rental Strategy)​

Matapeli wengi huwekeza kiasi kidogo cha pesa walizowaibia watu wengine ili kupata "mafuta" ya kuwanasa wapya hii hutumika sana Bongo matapeli wengi hukodi magari na nyumba, pia wengine huingia mikataba aidha na wapangishaji nyumba magari kutumia magari au nyumba hizo ili kuwatangazia zaidi maana matapeli wengine washakua na majina mitandaoni

  • Airbnb za Kifahari: Badala ya kumiliki nyumba, wanakodisha Apartment ya kifahari kwa siku moja tu. Wanafanya content creation ya mwezi mzima kwa siku hiyo moja (wanabadilisha nguo mara kumi na kupiga picha sehemu tofauti za nyumba) mjini hapa

  • Showrooms na Magari ya Kukodi: Wanaenda kwenye showrooms za magari na kuomba kupiga picha wakijifanya wanataka kununua, au wanakodisha gari la kifahari kwa saa chache ili wapige nalo picha na video wakidai ni lao.

c. Matumizi ya Pesa Bandia au "Prop Money"​

Zile rundo la pesa unazoziona kwenye video mara nyingi siyo pesa halali za matumizi najua mshakutana nazo vimbao na kadhalika

  • Pesa za Filamu (Movie Props): Kuna pesa zinatengenezwa maalum kwa ajili ya kuigiza filamu ambazo zinafanana sana na halisi. Matapeli huzinunua hizi kwa bei nafuu na kuzionyesha kwenye kamera.

  • Mbinu ya Karatasi: Wanachukua karatasi za kawaida na kuziweka katikati, kisha juu na chini wanaweka noti mbili tu halisi. Wakizipeperusha mbele ya kamera, huwezi kujua katikati ni makaratasi.

d. Ofisi na Hoteli (The Lobby Lifestyle)​

  • Hoteli za Nyota Tano: Huwezi kumzuia mtu kuingia kwenye hoteli kubwa. Matapeli huvaa vizuri smart, wanaagiza kikombe kimoja tu cha kahawa, kisha wanapiga picha nyingi kwenye mazingira hayo ili ionekane ndipo wanapoishi au kufanyia mikutano.

  • Green Screens : Matapeli wa kisasa wanatumia wapo kasi hawaachwi na teknolojia wanatumia Green Screen nyuma yao ambayo inaweza kuonyesha ofisi ya kifahari au mji wa Dubai, kumbe yupo chumbani kwake ameweka kitambaa cha kijani ankunywa togwa

e. Lifestyle Scammers (Matapeli wa Mitindo ya Maisha)​

Hawa ni wale ambao tayari wameshaiba pesa kwa watu kadhaa. Wanatumia sehemu ya pesa hizo kuishi maisha hayo kweli (kununua gari au kuishi hoteli) ili kujitangaza zaidi na kuwapata watu wengi zaidi. Hapa ndipo mchezo wa Pyramid Scheme unapoingia wanatumia pesa ya muathirika wa kwanza kumvutia muathirika wa pili.

sasa tuendelee na jinsi matapeli wanawakamata watu kisaikolojia

2. Kutengeneza Mamlaka (Authority Bias)​

Matapeli hawa hujivika vyeo au hadhi kubwa.

  • Kwenye vikundi vya siri kama freemason: Wanajifanya ni Grand Masters au mawakala wenye nguvu za giza na utajiri wa haraka

  • Kwenye Pesa: Wanajifanya ni wataalamu wa Forex, Crypto, au wawekezaji wakubwa

  • Lengo: Binadamu tuna asili ya kutii au kuamini watu wenye mamlaka. Ukiamini wana nguvu au maarifa kuliko wewe, unakuwa tayari kufuata maelekezo yao bila kuhoji hivi unajua ni Rais kutapeliwa na kiongozi wa serikali kuliko mtu wa kawaida sababu ya mamlaka yake

3. Sheria ya Kutoa kwanza ndo upate yani nipe nikupe(Reciprocity)​

Kabla hawajakuomba pesa, wanaweza kukupa kitu kidogo bure:

  • Maelekezo ya bure, au chochote kitu , au kukuunganisha na watu muhimu.

  • Nia yao : Akili ya binadamu inapopewa kitu bure, hujisikia ina deni. Wanapokuja kuomba ada ya usajili au pesa ya kiapo, unajikuta unatoa kirahisi kwa sababu ulishaanza kuwaamini.

4.Mazingira ya uharaka na Uhaba (Scarcity & Urgency)​

Hii ndiyo silaha yao kubwa ya mwisho. Watakuambia:

  • "Nafasi za kujiunga na Freemason zimebaki mbili tu leo."

  • "Fursa hii ya uwekezaji itafungwa baada ya saa moja."

  • Nia yao : Hii inazima sehemu ya akili inayofanya maamuzi ya kimantiki na kufungua hisia (Emotional brain). Ukiogopa kukosa (Fear Of Missing Out), utatuma pesa haraka kabla hujafikiria mara mbili.baade ukishalizwa sasa ndo akili inarudi mmmh mbona kama lile jambo halikua sawa

5. USiri (The Mystery Element)​

Wanatumia lugha ya siri, viapo, na kukuambia "usimwambie mtu yeyote."

  • Nia yao : Hii inakutenga na marafiki au ndugu ambao wangeweza kukupa ushauri wa busara. Wanakuaminisha kuwa wewe ni maalum na siri hiyo ni kwa ajili yako tu.

Pamoja na kuwaelimisha hivi bado kuna "wanyambo" watapigwa...

Wale wauza sura maarufu Huko mtandaoni wanatumia mbinu hizo hapo juu..ukweli mtupu sikupingi

Tuwe makini..
 
Kama ni Wagalatia acha wapigwe mkuu,usiwasanue wataishia kukuita kobazi.. hakuna watu wanapigwa pesa na hawa matapeli kama wakristo,ni wepesi kuamini tapeli anapokuja kwa mlango wa kidini au anapoongea huku anaunguruma kama Simba,wao uamini kwamba roho mtakatifu kapanda....unakuta jitu profesa lakini linatapeliwa kwa kuuziwa udongo wa Jerusalem hetii!
 
Nzuri sana hii mkuu,nilikuwa nawaza kitu kama hiki kwa hao wanaotumia nguvu sana kujionyesha wanazo pesa.

Wakati fulani nikakutana Facebook na comment ya dogo mmoja kwenye ukurasa wa huyu mkinga aliyeonekana amenyang‘anywa magari juzi akimlalamikia amemtumia 100K amuunge freemason lakini amem-block instead amuunge,so unaweza ukaona ni wa ngapi wenye akili kama za huyo na wangapi wametapeliwa?
 
Back
Top Bottom