yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,927
- 4,199
Jana baada ya kupatwa na safari ya ghafla kuelekea mkoani, nikafika stendi wakati hela yangu ipo kwenye simu.
Nikaenda kutoa hela kwa bahati mbaya mawakala hawakuwa na fedha taslimu, nikaingia duka moja nikakuta ana Azam pesa. Nikahamisha hela yangu kutoka Yas / Tigo kwenda Azam.
La haula!!.. Kumbe lilikuwa kosa kubwa sana. Hela ikatoka kwenye akaunti ya tigo ila kwenye Azam haikufika. Nikiwapigia tigo wananiambia nisubiri masaa 72.. 😭😭😭😭
Ukizingatia safari yangu ya dharula, kila kitu kimeharibika nimechanganyikiwa. Si bora wangenitahadharisha kuwa kuna tatizo la kiufundi au mtandao wakati nataka kufanya muamala!
Naomba hela yangu iingie nifanye maamuzi sahihi kama naendelea kutumia huu mtandao au naachana nao.
ILA OMBA YASIKUKUTE