Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Mwaka 2005 nikiwa nimezama kwenye imani kali ya ulokole, hapo nikiwa kiongozi wa Ukwata na pia kiongozi wa kiroho kwa vijana wa mtaani kwetu (nilikuwa napita majumbani, naongea na wazee waniruhusu niwafundishe maadili mema watoto wao ikiwemo kazi za nyumbani na za kitaaluma).
Kutokana na tabia yangu ya kipekee ya huruma, upole, kujitoa kwa ajili ya wengine, unyenyekevu na upendo was dhati wa hali ya juu, wazazi wengi sana walinipenda na nikawa gumzo mtaani, kila mzazi akitaka mtoto wake awe kama Mimi.
Basi ikatokea bahati mbaya Bibi yangu akafariki, lakini kabla ya yote aliniomba mara kadhaa anivalishe ngozi ya Chatu na chui, anipe ngao na mkuki na maziwa ya Simba, ili hapo rasmi niwe mzee wa ukoo.
Kwa kweli nilikataa na kupinga sana, nikakemea na kuharibu hila za yule muovu ibilisi, nikasam aratisha ngome na maagano yote ya kimila yasiyo mpendeza Masihi wa Bwana.
Basi Bwana, Bibi yangu akafariki kukiwa hamna mrithi wa mkoba. Mizimu ilikuwa imenichagua Mimi na si mwingine.
Basi kabla Bibi hajazikwa marafiki zangu walikuja kunipa pole, wakalala msibani pamoja nami ili kunifariji.
Usiku tuliimba na kucheza, tulihubiri habari za Bwana Yesu na wokovu, tulifanya maombi na ibada ndefu.
Mida ya saa kumi na moja alfajiri, tukapitiwa na usingizi mzito na tukalala fofofo.
Ndoto nilizokuwa nikiziota zilikuwa za kutisha na za kuogopesha sana, niliota Kuna radi kubwa inapiga, ikaua watu wote nikabaki Mimi peke yangu Mji mzima.
Magari yote NI yangu, pesa zote ni zangu, majumba yote ni yangu. Ila harufu ya mizoga na miili ya watu waliokufa ndivyo vinavyonizunguka.
Nikashtuka usingizini, nikajkemea hiyo ndoto na siku lala Tena.
Mida kidogo jamaa zangu wakaamka, tukaoga na tukatoka kwenda kutafuta supu.
Tukafika mgahawani, wenzangu wakaagiza supu, ila Mimi sikuagiza supu, nikaagiza chai na chapati mbili, baada ya hapo, ufahamu wangu ukatoweka, nikajikuta nimerudi tena kule kwenye mizoga na maiti zenye kunuka zilizopigwa na radi.
Basi Bwana, kumbe huku kwenye kibanda cha supu niliagiza chai na chapati mbili, zaidi ya mara 18, chapati zikaisha nikawaambia wanipe maandazi, nikawa naagiza chai na maandazi miwili, vikiisha naongeza Tena, hadi maandazi yote yakaisha, nikaanza kuagisa chips, muda wote huo walokole wenzangu wananishangaa, Niko kimya macho yamenitoka kama yule waziri wa majalalani.
Wenzangu wananisemesha mie nakula tu.... Basi nikala siku nzima na hela hatukulipa.
Muda wote huo Niko kimwili na wenzangu, ila baada ya Kula nikaanza kutoka jasho jingi, na viumbe Kama dagaa wakawa wanatoka mwilini mwangu, walitoka wengi zaidi ya kujaza ndoo ya Lita kumi
Nikapewa maziwa ili nitanyiwe Mila, nikawa na nguvu za ajabu, Mila ikashindikana kufanyika mpaka alipokuja ndugu yetu mmoja hivi, ni ngumu sana kuelezea muunganiko wetu.
Lakini yeye akaagiza achinjwe ndama wa miezi sita, kisha damu yake inyunyiziwe kwenye maiti ya Bibi.
Ngozi ya ndama itengenezwe mkoba Kisha utumbo wote uwekwe humo na nivalishwe.
Haya Mambo ya Mila yasikieni TU na usiombee yakukute.
Kama una shida yako ninauwezo wa kukuangalia.
Sisafishi nyota, Sina Pete za bahati Wala za majini.
Asante