Asante mkuu...nimesoma "Mtaki Mwanyenza" nikakumbuka "Kapele" ambaye naye alipewa hadhi ya uchifu mdogo kama mtaki. Kapele naye alikuwa Mnyamwezi, aliyepelekwa ufipani kwa chifu Milanzi wa wafipa baada ya wakoloni - waarabu kisha wajerumani kukumbana na upinzani mkali. Hasa wajerumani walipokuta Wafipa tayari wanatengeneza magobole.
Falme hizi mbili za wafipa na wahehe zilikuwa tishio kwa Chifu Isike wa Tabora, na hata chifu Milambo wa Urambo-Tabora Magharibi alimchukia sana Isike kwa kuwa kibaraka wa wakoloni. Ukizingatia kuwa Mirambo alikuwa chotara wa muha na mbungu. hakuwa pure mnyamwezi.
Isike alikuwa anatumia trick hiyo ya kuwapeleka vibaraka wake katika himaya ngumu kwake na kwa wajerumani, na hata kuwatoa wanawake binti zake na jamaa zake wakaolewa na machifu hao, na hata kuwashawishi waachane na dini zao za asili waembrace dini za wakoloni, hasa dini yake mpya aliyokuwa ameshaipokea kutoka kwa waarabu. trick ambayo alifanikiwa sana kwa mkwawa.