Jinsi mnyama atavochinjwa

Kivule

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
639
Reaction score
662
Mimi nikiwa mwanayanga halali kabisa na namiliki kadi ya YANGA AFRICA, kwanza kesho mnyama anakaa bila wasiwasi ila yafuatayo lazima yafanyike.
1. Simba mechi iliyopita walitutesa kwa sababu walieka viungo wao watatu pale kati, hivyo nasie kesho inabidi tujaze viungo katikati ikiwezekana waanze THABANI KAMUSOKO (fundi hatari ikitokea faulo goli), HARUNA NIYONZIMA (kiungo bora africa mashariki na kati) na SALUM TELELA.
2. Geofrey mwashiuya uwezo wake ni wa wastani ivyo mechi ya kesho ni heri aanze DEUS KASEKE.
3. KAMUSOKO lazima nae awe anatembea na mpira mana hakai na mpira miguuni km niyonzima, sio vibaya ila muhimu kesho akae na mipira ili tuwapoteze kati
4. Simon msuva yuko vizuri sana na lazima aanze kesho ila ana mpira wake wa kuogopa kuingia kulia na kupiga krosi ivyo kesho awe ana force kupiga chenga na kutia majalo na imani anaiweza vizuri.
Kesho yule mchawi wao hayupo wanamwita OKWI ivo kifo ni lazima mana nikimuonaga uwanjani nahisi mda wowote kwenda chooni ahsanteni.
 


Duh, lkn bora wewe umekiri jinsi Okwi alivyokuwa anawakosesha raha. Ila kitu kimoja nashangaa kwenye mechi ya Simba kila mchezaji wa Simba hata yule wa kawaida anabadilika na kuwa na uwezo wa juu sana.
Kumbuka kazi aliyofanya William Lucian na Ndemla enzi zile, angalia Awadhi Juma na Maguli kwenye mtani jembe, nk.

Usishangae Kiiza, Ibrahim Ajib na Mgosi kwenye mechi hii wakatengeneza partnership kama ya Ronaldo, Bale na Benzema
 
Yanga kwenye majigambo mko powa sana lakini tukikutana uwanjani vichwa chini, mnabaki kusema simba ipo kwa ajili ya kumfunga yanga tu, sasa safari hii tupo kwa ajili ya kuwafunga wote. Mnyama kula kandambili haooo
 
yANGA HAMSHINDI HATA KWA BAHATI MBAYA...............
 
Yanga kwenye majigambo mko powa sana lakini tukikutana uwanjani vichwa chini, mnabaki kusema simba ipo kwa ajili ya kumfunga yanga tu, sasa safari hii tupo kwa ajili ya kuwafunga wote. Mnyama kula kandambili haooo

Kesho simba mnakufa mbili bila
 
mkuu umesema ukweli ila kesho afe mmasai afe mmangati kipigo lazima......YANGA 2 - 0 SIMBA
 
Nauona mchango wako kama hotuba ya magufuli akiwa ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…