Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 856
- 1,662
Kwa binadamu yoyote ambae ana akili timamu ni jambo lisiloepukika kupitia changamoto ya dharau, kashfa , kebehi , matusi kutoka kwa majirani, marafiki au watu wetu wa karibu kama mke , mume au familia zetu.
Tukiwa kama binadamu, hatuwezi kuzuia hali ya kuchukizwa , kuwa na nogwa au hasira pindi tunapofanyiwa vitendo hivyo.
Nyoyo zetu hujaa huzuni, mfadhaiko na chuki, mtu huweza kupata msongo wa mawazo hivyo kupoteza Nuru na siha njema katika mwili wake.
Kila ukikumbuka ulilofanyiwa moyo unaingia ganzi na simanzi unakosa hata hamu ya kula hali inayopelekea kudhorotesha ustawi wako wa kiakili, kimwili na kiuchumi.
Ndani ya miaka 3 nyuma nilikumbana na changamoto hizo kutoka kwa watu wangu wa karibu, hali iliyopelekea kudhoofu kimwili , siha ikapotea kabisa, nilikonda vibaya
Ndipo nikaja kugundua tiba ya msamaha kutoka moyoni.
Ilikuwa Kila nikifikiria nilichofanyiwa moyo wangu unajawa na chuki kubwa. Kila nikikumbuka natamani na wao yawarudie kama waliyonifanyia au wapate zaidi ya waliyonifanyia.
Kumbe bila kujua chuki ile ilikuwa inaniathiri mimi mwenyewe kwa kiasi kikubwa. Sikutaka kupoteza siha yangu zaidi.
Nikaweka dhamira ya kusamehe kutoka moyoni.
Niliwezaje kufanya Hilo ilihali bado nilikuwa nina maumivu moyoni.
Kuna msemo unasema " kama huwezi kubadilisha mtizamo wa mtu juu yako basi badili mtizamo wako juu yake".
Kwamaana hatuwezi kulazimisha watu watuheshimu, watujali au watuthamini. Nikajiuliza.
"Je, chuki yangu nilonayo inaathari gani katika maisha yao!?.
Chuki yangu sio sumu au risasi kusema itawaua, maisha yao yanaendelea, pamoja na chuki yote niliyonayo juu yao"
"Na je, ninavyotamani yawafike walonifanyia mimi ntafaidika nini na Hilo!?.
Hapana siwezi kufaidika na chochote kile , anguko lao haliongezi lolote katika maisha yangu, kama nina maisha magumu yataendelea kuwa magumu hivyo hivyo hata wao wakianguka".
"Pia sio kazi yangu kulazimisha watu waniheshimu au wanithamini, hayo ni maamuzi ya mtu binafsi, anaweza akafanya hivyo au asifanye".
"Kama sikuweza kuwa na ushawishi juu Yao basi hata na wao kuanzia sasa Hawana ushawishi wowote juu yangu ".
Nisafari iliyochukua muda lakini nilifika na nikajifunza kusamehe kutoka moyoni kwa Amani ya nafsi yangu.
Chuki, hasira, vinyongo ,sononeko langu juu yao vyote vikatoweka, nikawatakia kheri ya dhati katika maisha yao. Baada ya muda siha yangu ikarejea.
Na tangu wakati huo ikageuka desturi iliyojijenga moyoni mwangu, sichukii mtu hata anikosee vipi zaidi ntampa msamaha wa kutoka moyoni Kisha maisha yangu yanaendelea kama alivyoyakuta na Amani zake.
Ukiwasamehe waliokukosea huwasamehi wao bali unasamehe kwaajili Yako mwenyewe. Unatunza ustawi wa afya Yako ya akili, mwili na uchumi.
Ukiweza kujifunza hili basi utaona namna maisha yako yanavyojaa Amani tele.
Wote mnaopitia maumivu , maumivu yenu yakawe ngao ya kuwajenga kifikra na muwe watu bora na imara zaidi ya awali.