Jinsi mtanzania anavyoweza ku- "self publish" - Create space au Lulu .....

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Hebu wenye uzoefu tupeane mawazo jinsi mtanzania aliyeko Tanzania anavyoweza ku "self publish" kwenye mitandao kama Create space, Lulu.com nakadhalika au kuuza kitu kwenye mitandao kama Amazon.
 
Hebu wenye uzoefu tupeane mawazo jinsi mtanzania aliyeko Tanzania anavyoweza ku "self publish" kwenye mitandao kama Create space, Lulu.com nakadhalika au kuuza kitu kwenye mitandao kama Amazon.
wenye uzoefu wa mchakato mzima
 
Okay iko hivi kwanza inabidi ujue kitabu unachotaka ku publish ni size gan either 5X8 au zaidi.
Baada ya hapo (kwa create space). Ingia katika web yao tafta template ya kitabu husika kisha copy na paste kitabu chako katika template hiyo.
Mind you template ziko za aina mbili kuna yenye maneno na iliyo blank. chukuwa yenye mamneno. Onyo usijaribu kubadilisha font wala font size.

baada ya hapo endelea. na kama huna cover page kuna free cover page. na kama huna ISBN ipo wanakupa wao.

kisha panga bei ya kitabu chako.
proof read
kisha BOOOOOM baada ya 24hrs
kitabu kiko sokoni.

ni jitihada zako wewe kukipigia promo. wao wanahakikisha kitabu kimewafikia watu 1M
make sure kitabu kiko edited vizuri
make sure kitabu kina cover nzuri (Maana hawa watu milioni moja wataona cover tu ya kitabu ikiwavutia ndo watanunua)

haya ni maelezo ya summary tu wadau
kila la kheri ila huu ujasiliamali wa kitaaluma unalipa sana jamani
 
Nimeipenda hii mkuu, hebu tiririka zaidi kwa upande wa Amazon pia.
 
Good insight... Unaweza fafanua inalipa kwa mamba gani boss
 
Nimeipenda hii mkuu, hebu tiririka zaidi kwa upande wa Amazon pia.


Kakak maelezo ni marefu mnoo mnoo sasa ila kwa kifupi ni kuwa uki publish kitabu create space au Lulu kitauza na Amazon pia.

cha muhimu edit kitabu vizuri na tafta cover zuri la kitabu. mimi kitabu changu cha kwanza niliself publish niliuza kopi 1500+ kwa bei ya $4 you can imagine hela iko nje nje ila kuna namna za kuki market kitabu chako nk.

mambo ni mengi sana kuelezea hapa labda niweke uzi kabisaa mpyaa
 
chondechonde weka uzi mpyaa mkuu
 
Halafu mkuu nimeona website ya create space wameandika kuwa hivi mapema watahamishia vitabu vyote kwenye KINDLE DIRECT PUBLISHING.
 
Yeah now Create Space imeunganishwa na KDP madhara ya ke ni kuwa kwa sasa hutaweza ku publish kitabu kwa lugha ya kiswahili tena. maana KDP haitumii Kiswahili.
 

Nashukuru sana kwa ufafanuzi mzuri na pia nimepata faraja kujua wewe ni mmoja ya watumiaji wa huduma hii ya "self publishing"

Changamoto kubwa ambazo mimi nimeiona na bado sikupata majibu yake kwenye mitandao

1. Mitandao hii tunayoiongelea ni ya kimarekani, na nimeambiwa ili uweze kuitumia ni lazima uwe tax number ya marekani, wengine wanasema unaweza ku apply hii kupitia mtandao na ukapewa lakini kupata mtu mwenye uzoefu atakatoa direction inaweza kusaidia.

2. Ni jinsi ya kufikishiwa royalties pale "author" anapokuwa amefanikiwa kuuza nakala. ukitazama nchi ambazo zinatajwa kuwa ukiwa katika nchi fulani na fulani unaweza kutumia mfumo wa benki au ile fursa ya kuchagua nchi ya origin katika registration, je kama Tanzania haionekani kwenye orodha je nini cha kufanya?

samahani kwa kuchukua mda wako lakini naamini mliotangulia kuona mbali mnaweza kujitolea kutoa ushauri unaoweza kusaidia watanzania walio wengi.

Natanguliza shukrani
 
Jamani nitatoa uzi kamili juu ya hili suala ni mambo marefu kidogo.
Ila upande wa tax info jaza wewe ni non Us citizen kuuna maelezo mengi watakupa ujaze utajaza.

kwa kuwa wewe ni non Us citizen royalties utalipwa kwa njia ya check.
wao wanakutumia check unaenda bank unatoa mkwanja wako.

Na hizi hulipwa kila mwisho wa mwezi.
So sio lazima uwe na tax number ya Marekani mkuu
 
Malipo unalipwaje mkuu maana bank account zetu chenga na hawakubali paypal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…