Jinsi mwanamuziki Salum Abdallah alivyopoteza maisha kwa majeraha ya ajali

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
KUMBUKUMBU YA MWANAMUZIKI SALUM ABDALLAH:

1700516408570.jpg

Tarehe 18 Novemba mwaka huu ilikuwa ni siku ya Kumbukumbu ya Miaka 55 ya kifo cha mwanamuziki na kiongozi wa Cuban Marimba band ya Morogoro Salum Yazidu Abdallah aliyefariki kwa majeraha ya ajali ya gari mnamo Novemba 18, mwaka 1965

KIFO CHAKE
Alhamisi tarehe 18 Novemba, mwaka 1965 ilikuwa ni siku yenye hekaheka kubwa mjini Morogoro, kwani ugeni mkubwa ulikuwa unasubiriwa katika mji huo.

Mheshimiwa Julius Kambarage Nyerere na Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa, viongozi wakuu wa nchi kwa wakati huo, walikuwa wakisubiriwa na wananchi wa hapo Morogoro katika sherehe ya kufungua Chuo cha Kilimo ambacho kwa sasa kinajulikana kama SUA (Sokoine University of Agriculture).

Pamoja na wageni hao pia alitegemewa kuwepo aliyekuwa Mbunge wa Morogoro mjini kwa wakati huo Mheshimiwa Oscar Thalatiel Kambona.

Bendi mbili kubwa maarufu za pale Morogoro mjini zote zilitegemea kupiga muziki siku hiyo, na pia zilipangiwa kutembelewa na viongozi hao wakuu wa nchi.

Kutokana na ushindani mkubwa wa bendi hizo wanamuziki na washabiki wa bendi hizo walikuwa roho juu kusubiri mpambano wa usiku huo.

Kwenye muda wa saa kumi na mbili jioni baada ya shamrashamra za kupokea viongozi kwisha bwana Ramadhan Mdidi aliyekuwa msaidizi wa mmoja wa madereva wa Salum Abdallah alikuja kumueleza mkuu wao huyo kuwa moja ya gari lake limenasa kwenye mchanga katika mkondo wa mto walikokuwa wakichimba mchanga, kwa hiyo ilikuwa busara kuliondoa gari usiku uleule au la kama mvua ingenyesha gari lingeweza kuchukuliwa na maji.

Salum Abdallah akaagiza gari likavutwe.

Salum Yazidu Abdallah ndiye aliyekuwa kiongozi muimbaji wa bendi ya Cuban Marimba, pia alikuwa ana malori kadhaa aliyokuwa akimiliki na akiyatumia pia katika mradi wa kujenga nyumba za National Housing pale Morogoro kwa wakati huo.

Salum akamtuma mwanamuziki wake Waziri Nyange atangulie kwenye ukumbi ambako wangepiga muziki ili kuweka vyombo sawa tayari kwa onyesho la usiku ili yeye aende na lori jingine kwenda kuvuta gari lililonasa kwenye mchanga.

Siku hiyo Cuban Marimba walikuwa wapige muziki Community Center wakati wenzao Morogoro Jazz Band walikuwa wapige muziki Kichangani.

Kiasi cha saa moja hivi mmoja wa waliokuwemo kwenye lori lililoondoka na Salum Abdallah alirudi mbio nyumbani na kuwataarifu kuwa kumetokea ajali na Salum ameumia.

Ajali hii ilikuwa ya ajabu na imekuwa daima ikileta maneno kwa walioikumbuka.

Kwa maelezo ya waliokuwepo, giza lilikuwa limekwisha ingia na wakati lori likikaribia Msamvu taa zilizimika ghafla na gari likayumba lakini taa zikawaka tena, kiasi cha waliokuwemo kuanza kucheka, lakini kicheko chao kilikatika ghafla baada ya kugundua kuwa mlango wa upande aliokuwa amekaa Salum ulikuwa wazi naye amedondoka.

Walirudi nyuma na kumkuta akiwa kalala barabarani akiugulia kwa maumivu.

Mzungu mmoja alipita wakati uleule na gari dogo akawapa lifti watu wawili toka kwenye lile lori, mmoja akaenda nyumbani kwa Salum kutoa habari na mwingine akaenda kuchukua taxi iliyomchukua majeruhi mpaka hospitali.

Hivyo wote waliopata habari wakakimbilia hospitali wakamkuta mwenzao anaugulia maumivu, madaktari walimuomba anyooshe mikono na kisha miguu alipoweza, wakaamini hajavunjika bali ni maumivu ya juu juu ambayo yangeisha, kiasi cha kumruhusu arudi kwake na awahi matibabu kesho yake asubuhi.

Salum mwenyewe akawaambia wenzie wafungue vyombo wasipige dansi siku ile, wengi wakakesha nae.

Usiku kucha ulikuwa wa maumivu makubwa, asubuhi mgonjwa alipelekwa hospitali akafanyiwa upasuaji ikagundulika alivunjika kiuno na mifupa alipasuka kibofu cha mkojo, jambo ambalo kutokana na kuchelewa kugundulika lilikuwa ni baya sana.

Kama saa 7 mchana alitolewa chumba cha upasuaji na wenzie waliokuwa wakisubiri wakaambiwa waende makwao wakale vizuri ili waje baadaye kutoa damu kwa ajili ya mgonjwa.

Wakatoka kwa furaha wakijua mambo yatakuwa mazuri. Walielekea kwenye klabu yao wakatengeneza chakula na kula kwa furaha. Kulianza hata kuwa na utani kuwa "Mwarabu" akipona atatoa kibao kikali cha tukio hilo. Ikumbukwe kuwa baba yake Salum alikuwa Mwarabu halisi. Lakini ilipotimu saa kumi jioni taarifa ikaja kuwa Salum amefariki. Watu wakaanza kumiminika nyumbani kwake, wakakuta hata maiti imeshafikishwa kwake na imewekwa katika chumba kimoja ambacho kilikuwa kimetayarishwa kwa ajili ya fremu ya duka.

Inasemekana baada ya Salum kufariki Daktari Mkuu wa Mkoa aliendesha gari lake hadi nyumbani kwa Salum na kupaki gari lake nje na kuanza kulia jambo ambalo mara moja ndugu walielewa kuwa mambo yameharibika, hivyo waliweza kutayarisha sehemu hiyo ambayo iliwezesha watu kuja kuweza kuona mwili wa Salum kwa mara ya mwisho.

Haikuchukua muda habari zilisambaa na ulinzi ukalazimika ukimarishwa kwa kusaidiwa na polisi.

Watu wakakesha na marehemu.

Kesho yake hali ilizidi kuwa ngumu wakati wa kusindikiza maiti kwenda makaburini ilikuwa kama kila mtu alikuwa akitaka japo abebe kidogo jeneza, hadi ikalazimu FFU wawepo kuleta amani.

Jeneza la Salum liliweza kubebwa kutoka Nunge nyumbani kwa mama yake hadi Msamvu kwenye eneo alipozikwa, watu wakiwa wamejipanga mstari mrefu, hakukutumiwa gari.

KUJITABIRIA KIFO CHAKE KUPITIA WIMBO WAKE
Wimbo wake wa WALIMWENGU alioutunga kabla ya kifo chake pia ulileta tafsiri nyingi hasa kutokana na kifo chake cha ajabu.

Wimbo wenyewe huu hapa:

WALIMWENGU
Eeeeh Mola wangu eeeeh Mola wangu,
Nivue na ya dunia,
Hao walimwengu, hao walimwengu,
Wanitafuta kwa madawa,
Wataka wadhulumu roho yangu,
Wapate furahia,
Natoa salamu zangu,
Ningalimo mu dunia,
Kwa ndugu na jamaa zangu
Za mapenzi na furaha
Za kuwatoa uchungu
Ajali itakaponifikia
Nahadithi ndugu zangu,
Nyuma waliobakia,
Kubeba maiti yangu
Huku wakinililia
Ninashtakia Mungu
Nilotendwa mu dunia.

Weka namba ya Whatsapp hapa upate wimbo huu na nyimbo nyingine za Gwiji huyu wa zamani wa muziki nchini Tanzania.

Source:

Anko John Kitime John Mwa Kitime na Wikipedia.
 
Asante sana kwa kumbukumbu hii, kifo hiki kilihusishwa na imani za ushirikina wa ushindani wa soko la muziki kati ya Moro Jazz ya Mbaraka Mwishehe na Cuban Marimba ya Salum Abdallah. Alinyooshewa kidole Mbaraka!.

Karma nayo haina ajizi!, what goes around comes around, baada ya miaka kadhaa kupita, Mbaraka Mwishehe naye yakamkuta, alikufa kwa ajali ya gari jijini Nairobi.

Karma is real!.

Huu uchawi wa ajali wanafanyiana sana matajiri wa mabasi, na mastaa, ila mwisho wa siku nao hufa kwa ajali!, ambazo japo huonekana kama real accidents na watu hufa kweli ila some ni fake accidents ili tuu kutoa roho ya mtu!.
Ajali ya Sokoine
Ajali ya Chacha Wangwe
Ajali ya Mtikila
Ajali ya Mwakyembe
Ajali ya Deo Filikunjombe
Ajali ya tajiri wa Mabasi ya Nyatco
Kifo cha Gibson Sembuli
Kifo cha Kanumba
Kifo cha Sharo Milionea
Kifo cha Magwea
Kifo cha Adili Kumbuka
Kifo cha Marijan Rajabu

The list goes on!
P
 
Asante sana Mzee Pascal Mayalla.
Mshana Jr na Rakims naomba mchango wenu kwenye hili.
 
Mkuu Pascal,Mbaraka alifia Mombasa General Hospital(makadara)
 
Tajiri...
View attachment 2822152
Kati ni Salum Abdallah na kushoto kwake ni Juma Kilaza
Juma KILAZA, Mwanamuziki huyo alikuwa na tambo na majigambo kuwa yeye ni bora kuliko gwiji la muziki Mbaraka Mwinshehe na ana uwezo mkubwa wa kutumia vyombo vya muziki kuliko Mbaraka Mwinshehe.

Ili kuondoa doubt, liliandaliwa Pambano kati ya KILAZA na Mwinshehe lakini tofauti na tambo za KILAZA, Mwinshehe alamgaragaza vibaya sana mpinzani wake na KILAZA alionesha UWEZO MDOGO SANA.
 
Asante sana Mzee Pascal Mayalla.
Mshana Jr na Rakims naomba mchango wenu kwenye hili.
Ahsante kwa mawazo yako juu ya imani za kishirikina. Lakini kuhusu imani hiyo na ushindani kati ya Morogoro jazz na Cuban Marimba na haswa juu ya kifo cha Salum Abdalah inawezekana kuwa kweli lakini wazo kwamba Mbaraka ananyooshewa kidole kuhusu hili, nina shaka nalo kwani Mbaraka bado alikuwa mchanga sana katika tasnia hii ya muziki wakati SAY alikuwa tayari maarufu sana. Isitoshe katika miaka ya 1960 ni Cuban Marimba ndiyo iliyokuwa bendi maarufu pengine kuliko bendi zote nchini, wakati Morogoro jazz ilikuwa badi inajitafuta. Mbaraka alijiunga na Morogoro jazz mwaka 1964 akiwa mpiga gitaa la rhythm na filimbi, alianza kupiga gitaa la solo mwaka 1965 na kuanza kuwa mpigaji mkuu wa kutegemewa wa ala hiyo mwaka 1966. Mwaka 1965, alichaguliwa kuwa kiongozi wa jukwaa wa bend,i yaani mwaka aliofariki SAY ambaye alifariki 17 November 1965. Kwa mantiki hiyo haijawahi kutokea SAY kuwa mshindani wa Mbaraka. Mshindani wa Mbaraka alikuwa ni Juma Ramadhan Magola Kilaza (Juma Kilaza) aliyerithi mikoba ya kuiongoza Cuban Marimba mwaka 1966 akitokea Kilosa alikokuwa akifanya kazi baada ya wenzake kuona haja ya kutafuta damu changa kuongoza bendi hiyo baada ya kifo cha SAY, yaani mwaka mmoja tangu Mbaraka achaguliwe kuwa kiongozi wa jukwaa wa Morogoro jazz. Wengi wanadhani Kilaza alirithi uongozi wa Cuban Marimba moja kwa moja, hii si kweli, sababu ya kutochaguliwa kwake moja kwa moja ni kwamba japo alikuwa mwanamuziki wa Cuban Marimba, hakuwa mshiriki wa mara kwa mara katika bendi, kwani alikuwa akifanya kazi Kilosa. Mshiriki wa mara kwa mara katika uimbaji alikuwa Kibwana Seif (AKA kata shingo) ambaye alitegemewa na wengi kuwa ndiye atakayerithi mikoba ya uongozi wa Cuban Marimba kwani ameshiriki katika kuimba nyimbo nyingi sana. Habari zaidi utazipata katika vitabu nilivyoandika juu ya nguli hawa. Juma Kilaza Nguli wa Muziki kutoka Morogoro mji wenye sifa ya mpira na Muziki: Mji kasoro bahari na Mbaraka Mwinshehe Soloist National na Muziki wa rumba la Tanzania Juma Kilaza Nguli wa Muziki Toka Mji Wenye Sifa ya Mpira na Muziki, Mbaraka Mwinshehe na Muziki wa Rumba Tanzania
 
Mkuu hongera sana Kwa kumbukumbu
 
Swadakta Sheikh
 
Umenena vyema sana hivi ndivyo nilivyo hadithiwa pia na mzee wangu na akaniambia hata wimbo wa matusi ya nini Mbaraka Mwishehe alimuimbia Kilaza sababu ya matendo ya Kilaza dhidi ya Mbaraka ndio maana mwanzo wa wimbo utamsikia Mbaraka Mwishehe akisema tulikua na Salum mpaka kaenda ahera hawakuwahi kutukanana lakini alipoingia Juma kilaza ndio matusi yakaanza yakitoka kwake Juma kwenda kwa Mbaraka..
Na katika wimbo huo pia Mbaraka anasikika akimlaumu Kilaza kuharibu muziki wa Morogoro na sifa nzuri ya mji huo katika tasnia ya muziki..
 
Pia
Asante sana kwa kumbukumbu hii, kifo hiki kilihusishwa na imani za ushirikina wa ushindani wa soko la muziki kati ya Moro Jazz ya Mbaraka Mwishehe na Cuban Marimba ya Salum Abdallah. Alinyooshewa kidole Mbaraka!.

Karma nayo haina ajizi!, what goes around comes around, baada ya miaka kadhaa kupita, Mbaraka Mwishehe naye yakamkuta, alikufa kwa ajali ya gari jijini Nairobi.

Karma is real!.

Huu uchawi wa ajali wanafanyiana sana matajiri wa mabasi, na mastaa, ila mwisho wa siku nao hufa kwa ajali!, ambazo japo huonekana kama real accidents na watu hufa kweli ila some ni fake accidents ili tuu kutoa roho ya mtu!.
Ajali ya Sokoine
Ajali ya Chacha Wangwe
Ajali ya Mtikila
Ajali ya Mwakyembe
Ajali ya Deo Filikunjombe
Ajali ya tajiri wa Mabasi ya Nyatco
Kifo cha Gibson Sembuli
Kifo cha Kanumba
Kifo cha Sharo Milionea
Kifo cha Magwea
Kifo cha Adili Kumbuka
Kifo cha Marijan Rajabu

The list goes on!
P
aliyekuwa Mkurugenzi wa Ngorika alikufa hivyo hivyo kwa ajali ya kuliacha gari lake na kuvuka Barabara akagongwa. Na mara nyingi wataviongelea vifo vyao kwa kurekodi kabla hawajafa. Hata kama sio msanii.
 
Back
Top Bottom