Jinsi mwizi anaweza kuiba pesa kwenye simu yako ambayo haina passwords kwenye line

Hawaulizi namba ya Nida ya line iliyosajili? ninachojua bila kuwa na Nida no hawezi kufanya wala kupata chochote.
Kuna hawa vijana wanaosajili line ukiwapa namba yako ya simu wafanya wanavyojua wao wanakupa namba yako ya NIDA. So ni rahisi tu kwa mtu mwenye nia ovu kupata taarifa zako zote akatekeleza uovu wake.

Ni vyema sana kuweka password kwenye line.
 
Nikikumbuka kuna mtu alipata ajali akapoteza maisha hatukuwa tunamfahamu tukachukua simu yake ili tukague namba za watu wake tuwajulishe ikashindikana maana simu yake ilikuwa na pin, tukashauriana tutoe lain tuweke kwenye simu nyingine tupate hizo namba laini nayo ikawa na pin tulichoka mwisho wa siku manispaa walifanya kazi yao wakaustri mwili

Sjui ndg zake wanahisi nini mda huu, pin kwenye laini nilizichukia toka siku hiyooo
 
customer care huwa wana uliza no ya nida na data zingine uki miss chochote hapo .upewi code hata kama line ni yakoo
 
Mimi langu ni jinsi Serikali ya CCM wanavyoiba mafuta ya Petroli na kuhujumu wananchi kwa kupandisha mafuta bei👇
Your browser is not able to display this video.
 
Bado ni ngumu Kwa mwizi ambaye hajui namba ya simu ya laini aliyoiba... Maana kwenye kuomba PUK atahitajika kuingiza namba ya simu ya laini anayoombea pamoja na NIN iliyosajilia laini hiyo
Nikitaka kukuibia PIN haitakusaidia chochote nitakachofanya naingiza wrong PIN mara 3 naambiwa PIN blocked enter PUK kisha nachukua cm nyingine napiga customer service naomba PUK naingiza line inafunguka naambiwa enter new PIN (hii imeenda).
 
Ukisahau Password unafika ofisini kwao ukiwa na Kitambulisho na dole gumba lako...., anyway sio kwamba nasema ku-guess password tena 4 digits ni impossible ndio maana tunakoelekea security inabidi ziongezeke maradufu; Mfano ukipoteza line kuweka dole gumba kabla ya hapo mtu angedanganya kwamba ni yeye ndio kapoteza simu yako angeweza kupata line yako mpya na kuingia kwenye Sim Banking yako na Kufanya miamala (ila fingerprint imezuia hili)
 
Ukiibiwa simu piga call center funga line simple , ili mwizi akuibie anatakiwa kuwa na data nyingi zaidi ya ulizoainisha
 
Nikitaka kukuibia PIN haitakusaidia chochote nitakachofanya naingiza wrong PIN mara 3 naambiwa PIN blocked enter PUK kisha nachukua cm nyingine napiga customer service naomba PUK naingiza line inafunguka naambiwa enter new PIN (hii imeenda).
Bila ya kujua no ya simu?
 
Mimi Kampuni ya simu ikimpa mtu yeyote namba ya siri kisa tu amejua akaunti ina kiasi gani na muamala wa mwisho umefanyika lini, basi tunakutana mahakamani. Maana mtu yeyote wa Customer care anaweza kujua hizo taarifa bila kufanya jitihada yeyote ya maana. Kitu sensitive kama password ni lazima ibadilishwe physically kwa alama za vidole hata kwa wakala tu, muhusika aweke dole gumba na fingerprint ikisoma ndio umpe password mpya.
 
Sema watu huwa wanakuwa wazembe sana.
Kuna siku nimepokea msg ya viashiria vya utapeli kutoka namba ya simu ninayoijua ya dada mmoja. Niligundua kwa sababu ya mwandiko na shida aliyokuwa nayo isingekuwa rahisi kwake.

Tulivyokutana akanambia ni kweli kapoteza simu toka jana yake na watu wanalalamika kutumiwa msg za utapeli za kutaka kutumiwa pesa. Tukamshauri apige simu Customer Suport ili wafunge ndio aanze mchakato wa ku-renew. Akasema nitarenew. tukasema sawa.

Matokeo yake kajivuta vuta bila kuifunga wala kurenew hadi ndugu yake akatapeliwa.
 
Ukiweka PIN kwenye laini na ikatokea umepata ajali umekufa watu watashindwa kukusaidia kuwapigia ndugu zako
Lakini ndugu zako wataweza kukupigia na hao watu wakapokea simu kuwataarifu kuwa umepata ajali. Yaani kama wana nia ya kutoa taarifa, watatoa tu labda kama hupigiwagi simu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…