Jinsi mwizi anaweza kuiba pesa kwenye simu yako ambayo haina passwords kwenye line

Ukiibiwa simu piga call center funga line simple , ili mwizi akuibie anatakiwa kuwa na data nyingi zaidi ya ulizoainisha
Na ukipiga simu kutoa taarifa line ifungwe halafu kampuni ya mtandao wa simu wakachelewa kuifunga na mwizi akaifanyia uhalifu, ripoti suala hilo TCRA, utalipwa fedha zako. Huko TCRA unaruhusiwa kuwakilishwa na wakili na ni muhimu sana kwa kuwa mitandao ya simu huwa hawataki kulipa hiyo fedha. Ukitaka msaada zaidi wasiliana nami kwa 0713368153 Lusajo (wakili)
 
Nikitaka kukuibia PIN haitakusaidia chochote nitakachofanya naingiza wrong PIN mara 3 naambiwa PIN blocked enter PUK kisha nachukua cm nyingine napiga customer service naomba PUK naingiza line inafunguka naambiwa enter new PIN (hii imeenda).
Sio kweli kbs
 
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka zile password/pin ambazo ukizima simu na kuwasha inadai uingize kwanza password kwenye hiyo line kabla ya kuendelea kutumia hiyo line.

Hebu fikiri, mtu aliibiwa simu na siku moja baadae ikafanyika miamala ya kuhamisha fedha kutoka kwenye account yake ya M-Pesa kiasi cha zaidi ya TZS. 3,000,000/= kwenda kwenye namba tofauti za simu. Swali ambalo wengi wangependa kujua ni kwamba, mwizi huyo aliwezaje kujua namba ya siri ya aliyeibiwa simu hadi kuweza ku- access account yake ya M-pesa na kutoa fedha??!!

Wengi wetu wanaweza kusema watu wa kampuni za simu wanahusika katika hili. Hebu fuatilia ujue mbinu iliyotumika au inayotumiwa na wezi wa aina hii:

1. Simu ikishaibiwa, kama simu yenyewe ina password, wanatoa line na kuweka kwenye simu nyingine.

2. Hatua ya pili, mwizi atataka kujua line hiyo ya simu imesajiliwa kwa jina gani? Hivyo atapiga *106# na baada ya hapo atabonyeza No 1. Kama line imesajiliwa, atakuwa amepata kujua jina kamili la mmiliki wa line hiyo.

3. Hatua ya tatu, atataka kufahamu account ya mwenye simu, mfano: m-pesa, ina kiasi gani cha fedha? Hapo mwizi atatumia simu yake au simu ya mtu mwingine anayefahamiana naye kutuma kiasi fulani cha fedha, mfano atatuma TZS. 2,000/= kwenda kwenye namba ya simu ya aliyeibiwa. Pesa hiyo ikishaingia, automatically line ya simu iliyoibiwa italetewa sms inayoonyesha kutumiwa kiasi cha fedha, na salio lake jipya la wakati huo baada ya kutumiwa fedha.

4. Baada ya mwizi kujua salio, sasa anaweza kuweka mikakati ya kuiba kama account ya aliyeibiwa simu ina kiasi cha fedha zinazoweza kuibika.

•Hatua ya kwanza anapiga simu Customer Care na kujitambulisha kuwa yeye ndiye mwenye line ya simu iliyobiwa. Kumbuka jina analo tayari.

•Hatua ya pili akishapiga simu, atawaambia kuwa amesahau password ya account yake, Customer Care watakachotaka kujua kutoka kwake ni lini alifanya muamala wa mwisho, na ilikuwa ni kiasi gani, na salio lake kwenye account yake ni kiasi gani. Kumbuka taarifa zote hizo jamaa anazo tayari, hivyo anawaelezea watu wa Customer Care na wanamuelewa vizuri tu.

•Kutokana na usahihi wa taarifa za mwizi alizotoa kwa Customer Care, watamuamini na kumtumia code namba ambazo atatumia kubadilisha namba ya siri, na hivyo anafanikiwa ku-access account ya victim na kufanya miamala vile atakavyo.

MUHIMU
Ni vyema ikitokea mtu kaibiwa simu yake, immediately apige simu kampuni husika na kutoa taarifa ili line yake iwe blocked. Asitumie muda mrefu kutoa taarifa polisi na kufuatilia Loss Report pasipo kwanza kuwasiliana na Service Provider. Hii inaweza kusaidia kuzuia madhara yanayoweza kutokea mara baada ya mtu kuibiwa simu. Asanteni

USHAURI PIA KWA MITANDAO YA SIMU.
Mtu akipiga simu kuomba msaada wa kubadilisha namba ya siri waongeze pia idadi ya maswali ya udadisi kama namba ya kitambulisho alichosajili sajilia line, mwaka wa kuzaliwa, nk
Na mfano wakahitaji kitambulisho ulichosajilia ......huyo mwizi atajuaje namba YAKO ya Nida????
 
Line ikiwa pinned kila ukizima simu inadai pin , ukikosea mara tatu itadai puk. Puk unaweza omba kutoka kwa service provider ila mlolongo ni mrefu na siku hizi ni lazima ufike ofisini
Halotel line zao mpya zote zina pin by default na hakuna option ya kuondoa, japo unaweza kubadilisha .
Unaweza kuondoa na kubadilisha pia kwenye laini za halotel
 
Pin Kwenye line mpya za halotel haitoki
PIN inatolewa ndani ya sekunde zisizozidi 60 tangu usajili wa awali kabla laini haijasoma vizuri (ongea vizuri na mawakala wako)
 
Nikikumbuka kuna mtu alipata ajali akapoteza maisha hatukuwa tunamfahamu tukachukua simu yake ili tukague namba za watu wake tuwajulishe ikashindikana maana simu yake ilikuwa na pin, tukashauriana tutoe lain tuweke kwenye simu nyingine tupate hizo namba laini nayo ikawa na pin tulichoka mwisho wa siku manispaa walifanya kazi yao wakaustri mwili

Sjui ndg zake wanahisi nini mda huu, pin kwenye laini nilizichukia toka siku hiyooo
Mambo mengine ni kama destiny.

Naamini wengi siku hizi hawaserve majina kwenye line, wanaseve kwenye emails, hasa wanaotumia smartphones. Hivyo yawezekana hata kama hiyo line isingekuwa na password, bado mngekosa majina kwenye line.

Btw! Hao manispaa kabla hawajafanya mazishi hawakutoa taarifa nyingine kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu marehemu? Ili ndugu wajitokeze kwenda kutambua mwili? Alizikwa haraka haraka?
 
Nikitaka kukuibia PIN haitakusaidia chochote nitakachofanya naingiza wrong PIN mara 3 naambiwa PIN blocked enter PUK kisha nachukua cm nyingine napiga customer service naomba PUK naingiza line inafunguka naambiwa enter new PIN (hii imeenda).
Wee siku hizi wanataka nida number ndo utumiwe PUK...Namaswali mengine
 
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweka zile password/pin ambazo ukizima simu na kuwasha inadai uingize kwanza password kwenye hiyo line kabla ya kuendelea kutumia hiyo line.

Hebu fikiri, mtu aliibiwa simu na siku moja baadae ikafanyika miamala ya kuhamisha fedha kutoka kwenye account yake ya M-Pesa kiasi cha zaidi ya TZS. 3,000,000/= kwenda kwenye namba tofauti za simu. Swali ambalo wengi wangependa kujua ni kwamba, mwizi huyo aliwezaje kujua namba ya siri ya aliyeibiwa simu hadi kuweza ku- access account yake ya M-pesa na kutoa fedha??!!

Wengi wetu wanaweza kusema watu wa kampuni za simu wanahusika katika hili. Hebu fuatilia ujue mbinu iliyotumika au inayotumiwa na wezi wa aina hii:

1. Simu ikishaibiwa, kama simu yenyewe ina password, wanatoa line na kuweka kwenye simu nyingine.

2. Hatua ya pili, mwizi atataka kujua line hiyo ya simu imesajiliwa kwa jina gani? Hivyo atapiga *106# na baada ya hapo atabonyeza No 1. Kama line imesajiliwa, atakuwa amepata kujua jina kamili la mmiliki wa line hiyo.

3. Hatua ya tatu, atataka kufahamu account ya mwenye simu, mfano: m-pesa, ina kiasi gani cha fedha? Hapo mwizi atatumia simu yake au simu ya mtu mwingine anayefahamiana naye kutuma kiasi fulani cha fedha, mfano atatuma TZS. 2,000/= kwenda kwenye namba ya simu ya aliyeibiwa. Pesa hiyo ikishaingia, automatically line ya simu iliyoibiwa italetewa sms inayoonyesha kutumiwa kiasi cha fedha, na salio lake jipya la wakati huo baada ya kutumiwa fedha.

4. Baada ya mwizi kujua salio, sasa anaweza kuweka mikakati ya kuiba kama account ya aliyeibiwa simu ina kiasi cha fedha zinazoweza kuibika.

•Hatua ya kwanza anapiga simu Customer Care na kujitambulisha kuwa yeye ndiye mwenye line ya simu iliyobiwa. Kumbuka jina analo tayari.

•Hatua ya pili akishapiga simu, atawaambia kuwa amesahau password ya account yake, Customer Care watakachotaka kujua kutoka kwake ni lini alifanya muamala wa mwisho, na ilikuwa ni kiasi gani, na salio lake kwenye account yake ni kiasi gani. Kumbuka taarifa zote hizo jamaa anazo tayari, hivyo anawaelezea watu wa Customer Care na wanamuelewa vizuri tu.

•Kutokana na usahihi wa taarifa za mwizi alizotoa kwa Customer Care, watamuamini na kumtumia code namba ambazo atatumia kubadilisha namba ya siri, na hivyo anafanikiwa ku-access account ya victim na kufanya miamala vile atakavyo.

MUHIMU
Ni vyema ikitokea mtu kaibiwa simu yake, immediately apige simu kampuni husika na kutoa taarifa ili line yake iwe blocked. Asitumie muda mrefu kutoa taarifa polisi na kufuatilia Loss Report pasipo kwanza kuwasiliana na Service Provider. Hii inaweza kusaidia kuzuia madhara yanayoweza kutokea mara baada ya mtu kuibiwa simu. Asanteni

USHAURI PIA KWA MITANDAO YA SIMU.
Mtu akipiga simu kuomba msaada wa kubadilisha namba ya siri waongeze pia idadi ya maswali ya udadisi kama namba ya kitambulisho alichosajili sajilia line, mwaka wa kuzaliwa, nk
Hadi hapo kampuni inahusika,

Mtu akifungua case kudai kampuni imlipe Kwa kuwa imeshirikiana na wezi ,anashindwa case asubuhi tu.
 
Mambo mengine ni kama destiny.

Naamini wengi siku hizi hawaserve majina kwenye line, wanaseve kwenye emails, hasa wanaotumia smartphones. Hivyo yawezekana hata kama hiyo line isingekuwa na password, bado mngekosa majina kwenye line.

Btw! Hao manispaa kabla hawajafanya mazishi hawakutoa taarifa nyingine kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu marehemu? Ili ndugu wajitokeze kwenda kutambua mwili? Alizikwa haraka haraka?
Muhimu pia ni kuweka namba za dharura kwenye smartphone yako Yani ikiwa locked mtu akibonyeza emergency namba za dharura zinakuja ambazo uliziweka ikitokea dharura wapigiwe
 
Back
Top Bottom