Jinsi Namibia walivyoikabili corona na leo hakuna maambukizi tena

Jinsi Namibia walivyoikabili corona na leo hakuna maambukizi tena

Namibia ni mafukara wa kutupwa ukitoa jiji lao
Sehemu nyingi za nchi ni maskini kuliko hata Tanzania. Mijini ni matajiri tu tena wa kizungu ndio wapo vizuri wengine ni kawaida tena hawana opportunities kubwa kama Tanzania. Namibia ni taifa changa na lenye kukosa usawa kiuchumi. Unaweza ukadanganyika ukifika Windhoek kwasababu mji ni mzuri sana ila ukisogea pembezoni mwa mji ndio utaona hali halisi.
Haya ni makazi ya baadhi ya Wanamibia mjini. Nchi ni kame sana.
View attachment 1440285
Ila miji ya wazungu ipo vizuri.
View attachment 1440298
View attachment 1440301
 
Chadema ni wavivu wa kazi wanalilia lockdown
Kumbe ndo maana wamefunga mipaka,''the have nothing to loose"
jaribu kumwambia mtu mwenye shamba lake la nyanya au mipapai
inayomwagiliwa kila siku akae ndani uone kama atakuelewa.
 
Hakuna nchi ambayo waweza kusema they have nothing to lose, ni suala la kuangalia mbele na kuona nini kinakuja kama hatufungi. Kwa tanzania wakati wenzetu kama Kenya na Uganda waliofunga wanaanza kuachia sisi ndio hali inakuwa mbaya sasa. Na tena wakenya, waganda, wanyarwanda , nk hawataki kupokea wageni kutoka Tz kwani wanaona hawa ndio waathirika. Tulikosea kuchukua hatua za ki-strategia kwasababu ya ujinga wa viongozi wetu na ubishi, udikteta, nk. Mtaelewa huko mbeleni.
BASI TUKAE KIMYA TUSUBIRI HIYO MBELENI,KELELE ZA NINI SASA?
 
Ufukara umeongezeka mara mia moja kule
Na ukiwa fukara lazima utekeleze kila unachoambiwa ili mkono uende kinywani,
sisi tuna chakula chetu wenyewe,hata kama mtu hatakuwa na pesa mkononi lakini ana chakula
atadunda tu,watu wasitulazimishe kufuata kila wakitakacho.
 
BASI TUKAE KIMYA TUSUBIRI HIYO MBELENI,KELELE ZA NINI SASA?
Kondoo wengi hufa kwa kukaa kimya. Niliamka siku moja nikakuta kondoo analiwa mzima mzima na mbwa watatu cha kushangaza alikuwa hata halii, niliyosikia ni milio isiyo ya kawaida ya mbwa na sio kondoo, maskini...ndivyo tulivyo watanzania.
 
Ulimsaidiaje?
Nini tofauti yako na kondoo aliyekuwa analiwa kimya kimya,
na wewe uliyeangalia analiwa ukakaa kimya?
Mabeberu wanakufa kama kuku,watawezaje kutusaidia wakati wameshindwa kujisaidia?
 
Ulimsaidiaje?
Nini tofauti yako na kondoo aliyekuwa analiwa kimya kimya,
na wewe uliyeangalia analiwa ukakaa kimya?
Mabeberu wanakufa kama kuku,watawezaje kutusaidia wakati wameshindwa kujisaidia?
Labda ningekuuliza wewe nini tofauti yako na kondoo anayekaa kimya huku anaangamia manake wewe unasema tukae kimya huku watu ikiwa ni pamoja na wewe wanaangamia. Mimi angalau nawaambia tusikae kimya tuseme hata kwa kuandika kwa namna ambayo serikali itaona kweli kuna shida, lakini wewe unawaambia watu kaeni kimya?!
 
Hebu kwanza wewe sema shida unayoiona,kabla hujaiambia serikali,
jiulize swali rahisi,na wana jf tujiulize kwa pamoja
Ni majirani zako wangapi waliougua korona au wa mepona au kufariki?
ukiondoa habari tunazoziona mitandaoni na watu maarufu tuliotangaziwa vifo vyao
bila kujua walikuwa wanaumwa nini. Ukipata jibu ndo ujiulize je? ni kweli nina sababu ya kutangaza kwamba hali ni mbaya au woga tu?
Si ajabu wewe ni miongoni mwa wanaume wa Dar,ukiambiwa
vijana wanaojiita mbwa mwitu wapo mbagala,wewe tandika unakimbia nusra uvunjike kiuno.
 
Kuna visiwa vidogo kabisa vyenye population ya watu laki 5 na vingine 1 milioni kama Zanzibar lakini wameshindwa kuidhibiti corona. Estonia na Iceland wana visa vingi zaidi ya Tanzania (ukweli ni kwamba Tz ina visa vingi sana ila vimefumbwa).
Ubaya wa hivyo visiwa ni kuwa wana banana, kovid na hali hiyo dam dam,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipokuwa na kesi moja tu walifunga viwanja vyote vya ndege za kimataifa ikiwa ni pamoja na meli za abiria. Walifunga miji miwili mikuu kwa mwezi mmoja, hakuna kutoka hakuna kuingia ispokuwa kwa ruhusa maalum.

Baada ya mwezi walikuwa na kesi 16 tu lakini waliongeza kufunga (lockdown) kwa mwezi mmoja tena, sasa sio mikoa miwili tu bali nchi nzima.

Pia tangu mwanzoni kabisa walifunga masoko yote ya kienyeji, bar zote, nyumba zote za ibada na walizuia pombe kuuzwa mahali popote hata kwenye malls kubwa.

Namibia walikuwa wanawapa wananchi wao updates za kila siku za corona hata kama hakuna kesi hata moja. Pia Namibia yenye watu 2.5 million wamepima watu 1,122 wakati Tanzania yenye watu 55 milioni wamepima watu 652 tu!

Kesi za korona zilibakia zile zile 16 hata baada ya miezi 2 na ni katika mji mkuu Windhoek pekee. Leo Namibia wameondoa lockdown na wanaendelea na kazi kama kawaida.

Hivi ndivyo wenye akili zao wanavyofanya kazi na kufanikiwa.
Wapo wachache inamana we hufikirii kabisa!?
 
Back
Top Bottom