Jinsi ndege ya Rais wa Zambia ilivyotumika kwenye ufisadi mkubwa wa kutisha

Jinsi ndege ya Rais wa Zambia ilivyotumika kwenye ufisadi mkubwa wa kutisha

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,234
Reaction score
3,192
Leo mjini Lusaka, Zambia kumekuwa na gumzo la aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Mh Joe Malanji kupatikana na hatia za ufisadi mkubwa wakati wa utawala wa hayati Edgar Lungu. Kahukumiwa miaka minne jela. Walichofanya Malanji na wenzake ni kutafuna takribani USD 11,000,000 pesa za umma zilizokuwa zimetolewa na serikali ya Zambia kununua jengo jijini Ankara ili litumike kwa ajili ya ubalozi wa Zambia nchini Uturuki.

Kulingana na ushahidi uliopelekwa mahakamani ni kuwa mara baada ya serikali ya Zambia kuingiza fedha hizo kwenye benki moja ya Uturuki, Joe Malanji alienda Uturuki na kufanikiwa kuzitoa kwa msaada wa vigogo wengine wa wizara ya fedha ya Zambia. Kwa kutumia ndege ya Rais alifanikiwa kubeba mzigo wote huo cash na kurudi Zambia. Mara baada ya kufika Zambia, Malanji alianza kuingiza kwenye account yake $100,000 kila siku hadi alipomaliza mzigo wote.

Wananchi wengi wamemtupia lawama hayati Edgar Lungu kwa kuruhusu ndege yake itumike kubeba pesa za kifisadi. Wengine wameenda mbali kwa kudai huo mzigo ulikuwa wa hayati Lungu mwenyewe huku Malanji akiwa kama punda. Ila watu wengi wamejiuliza sana kuhusu matumizi ya ndege ya rais.

Kwa upande mwingine aliyekuwa mtu wa karibu wa Edgar Lungu, Mr Chomba Kaoma amedai kuwa wakati Lungu akiwa madarakani alipata ugeni wa Rais wa Uturuki, Mh Erdoğan ambapo katika mambo walikubaliana ni kuwa na ubalozi jijini Ankara Uturuki. Rais Erdoğan alivyoondoka Zambia aliwaacha baadhi ya maafisa wa serikali yake waliokuwa wakifanya mambo kadhaa ya kitaalamu baada ya maongezi ya marais.

Baada ya siku kadhaa Joe Malanji alienda Ikulu na kumjulisha Rais Lungu kuwa tayari maafisa wa kituruki wamemaliza mambo yao na wanarudi kwao. Kiungwana Rais Lungu alitoa ndege yake iwarudishe maafisa wale kwao. Hapo ndipo Joe Malanji na wenzie wakapanda ndege hiyohiyo na kwenda kufanya uhuni kwenye hela za umma za kununua jengo. Mr Chomba Kaoma kasema hayati Lungu hahusiki.
 
Siku Bongo nayo ikifanikiwa kumpata Rais kama Hakainde Hichilema ( namaanisha Mheshimiwa Tundu Lissu) aisee Wahuni wote watahama nchi! Maana hawatakubali kuyaacha mahekalu yao na kwenda kuanza maisha mapya na ya lazima kwenye magereza ya Keko, Ukonga, Segerea, Mawenzi, Kingolwira, Karanga, nk.
 
Tanzania ni ngumu sana ndege ya Rais kutumika kwenye mambo ya kihuni.
IMG_5862.jpeg
 
Back
Top Bottom