Poa natumemuacha ale uzazi vizuri. Ila kila mbwa ana siku yake.....
Moja ya miiko ya ubinadamu ni kumuumiza mwingine hisia bila ya kumpa nafasi ya kujitetea.
Huyo mabeste amekubali kuumia na sasa anableed damu ndani kwa ndani kwa maumivu anayoyasikia. Hivi unadhani kuna usalama hapo?! Umuumize mwenzako kwasababu za kibinafsi then uje kuwa na baraka huko uendako.... Nooo way. MUNGU yupo na anatoa haki.
Kama yeye aliona ni haki kumuacha mwanaume aliyejiapiza kumpenda na wakapata watoto pamoja leo anamtreat kama takataka then tutaona labda jina lake la mwisho liwe MUNGU.....
Mabeste jembe langu, popote ulipo, uvumilia maumivu jembe, najua umeumia kuona mwanamke aliyejinasibu kukupenda milele hata iweje na mkapata watoto wawili wazuri sana, kaamua kukatisha safari ya penzi lenu na kwenda anzisha safari mpya na mtu mwingine tu kwasababu haupo vizuri kiuchumi kwasasa, na mbaya zaidi ni mtu anaekufahamu na mnajuana na pengine anajua historia ya mahusiano yenu. Na leo kukutukana kabisa anakupostia picha ya mtoto aliyezaa nae katika tumbo la uzazi lile lile alilobebea watoto wako. Inauma sana....
Mimi personally kama mwanaume nimeumia sana kuona kichotokea aisee inauma sana.... Pole sana jembe.... Ipo siku haki yako itakufikia....... Maumivu huwa hayadumu ingawa ni makali. Jikaze bro.... Jikazee sana usikate tamaa.... Tunaumia pamoja... Na ninafeel maumivu yako.... Pole sana jembe langu.
Sent using
Jamii Forums mobile app