Jinsi nilivyo bambikwa Kesi ya Ubakaji mwanafunzi Wilayani Nzega

Jinsi nilivyo bambikwa Kesi ya Ubakaji mwanafunzi Wilayani Nzega

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,380
JINSI NILIVYOBAMBIKWA KESI YA KUZAA NA MWANAFUNZI WILAYANI NZEGA MWAKA2009.

Mwaka 2008 Kuna Binti (Bahati) alikuwa Form 4 Shule ya Sekondari Kiri-Nzega. Mdada huyo alibebeshwa mimba na mtu anayeitwa Pro akiwa kwenye mitihani ya kumaliza Form4. Mapadre wa shirika la SFS wakamwambia ang'ang'anie kuwa mimba amebebeshwa na Mimi. Mimi nilibaki kucheka tu maana niliona Kama utani maana mdada huyo alikuwa Malaya Fulani hivi kipindi anasoma.

Alipomaliza Form4 2008, mwezi wa pili 2009 akajifungua Mtoto wa kike akiwa anafanana na huyo Pro. Ndugu zake na huyo mdada wakanifungulia kesi Polisi ya Ubakaji. Niliitwa Polisi 2009 nikaenda nikawaelezea kuhusu ilivyo na nikawaambia kupima DNA, kumbe Polisi walikuwa wanajua kinachofanyika. Walimwita huyo mdada akawaambia huyu DON sijazaa naye Ila Mapadre wamesema nisingizie yeye ili arudi MOROGORO Utawani akawe Padre.

Polisi wakaiacha kesi hewani. Ila Wazazi wa huyu mdada wao wakaendelea kukomaa kwa kesi hewa isiyo na miguu wakipambana nifungwe. Badala ya kumtafuta Pro aliyempa mimba binti yao wao wanahangaika na asiyehusika. Ikanibidi nikasome Sheria ili kuzima huu Upumbavu. Sasa Mtoto wao kakua na anafanana na huyo Pro. Ni kiwaambia twendeni tukapime DNA hawataki, wao wanataka nifungwe tu. Nitafungwaje Mtoto siyo wangu.

Usalama wa Taifa wakaniwekea Vikwazo eti nimekataa Mtoto. Mambo ya kijinga sana haya, Mtoto sio wangu halafu mniwekee Vikwazo. Laana gani wakati Mtoto sio wangu. Kisasi kinakuja kikubwa Sana na hakijawahi kutokea Dunia nzima. Mpaka mawe yatasimama na kushangilia.

Cha kushangaza zaidi hata Pesa nazofanya kazi na Makampuni zikawa zinataifishwa na familia ya huyo mdada eti nilimpa mimba Binti Yao akiwa Shule huku mkwe wao Pro aliyempa mimba hawataki kumkamata. Hukohuko Nzega mdada mwingine yeye nilikuwa na mahusiano naye 2008/2009 ni Nurse jiji la Mwanza anaitwa Happy Alex naye akazaa na mwanaume mwingine huyo huyo Pro akasingizia DON ndiye baba wa watoto. Mwaka 2013 nikiwa Mwanza nilimtafuta ili tukapime DNA na watoto akakimbia. Huku anaendelea kuhudumiwa na ndugu zangu wakizani ni watoto wangu na mwenye watoto anacheka mpaka basi unyama huo unavyochezwa. Mwaka 2011 na 2013 nikiwa Wilayani Lushoto(TANGA) masomoni.

Nako yakawa yaleyale. Nikawa na uhusiano na mwalimu mmoja(Eva)2011 na baadaye mwaka2012 nikawa na uhusiano na mwalimu mwingine mmoja(Maria) . Eva akajifungua2011 na Maria akajifungua2013. Chakushangaza watoto wote hawafanani na Mimi. Kuja kugundua kumbe Eva kazaa na ndugu yangu na Maria kazaa na Rafiki yangu. Nikaomba tukapime DNA wakakimbia na kukata mawasiliano tangu 2014 mpaka leo. Huku wanasingizia wamezaa nami ili wahudumiwe. Huko Mwanza nako Kuna mdada anaitwa Vero akaja na mimba yake gheto kwangu alipoondoka ikageuzwa propaganda kuwa mimba ni yangu. Nikakaa kimya tu. Alipojifungua Mtoto hafanani na Mimi. Nikawaambia watu lakini wakang'ang'ania. Mtoto mwenyewe anafanana na Headmaster wa Mkolani Secondary.

Yule mdada alipoambiwa kupima DNA akakimbia mpaka leo. Yaani inaonesha Wanawake huwa ni Mabwege Sana ,anabeba mimba ya mwanaume anayempenda Ila anasingizia mimba ni mwanaume mwenye Pesa au mwenye nafasi Fulani ya kazi ili alelewe watoto wake. Nimefanywa Kama poyoyo kwa miaka mingi. Na Mimi DON NALIMISON Sina mtoto hata mmoja kutoka viuno vyangu. Ni propaganda zinazopikwa na Wanawake wapumbavu kwa maslahi ya kipumbavu.

Tanzania ni Nchi chafu Sana ambayo Wananchi wake wanataka kufanikiwa kupitia mgongo wangu. Sina Mtoto hata mmoja mpaka leo tarehe 22 may 2021. Nitatafuta Mwanamke sahihi atakayenizalia Mtoto wa damu yangu kutoka viunoni mwangu. Ila Kisasi juu ya kisasi kinakuja. Hao MABINTI ambao Sasa ni Wanawake watasimuliana na vizazi vyao.

DON NALIMISON
Musician and Philosopher in Political Thoughts.
KAHAMA-TANZANIA.
Phone:+255 682 94 29 01.
Photo_1614564799494_1.jpg
 
Aaaah mwanamuziki msomi kama wewe siamini kama unaona kufanana ndiyo undugu ujue we ni msomi mkubwa sana. Umefundisha miaka mingi naamini huwezi kutumia sababu ya kutofanana ndiyo siyo wanao.

Halafu hawa Usalama wa Taifa naona wanakufuata fuata sana tangu kipindi kile ulipotaka kuteuliwa kuwa balozi.
 
Hata huyo unaemtafuta ili uzae nae baadae lazma umruke useme mtoto siyo wako unalaana aise
 
Huyu jamaa yeye ansingiziwa tuu inamaana mzigo haufanyi kazi au ngugu zako wakiwahudumia sababu waliona kama ndugu yao ni NYUKI wa mashine.
 
Nilianza kusoma kisa kabla ya kusoma jina la mhusika,nilipofika kwa usalama wa taifa nikagutuka,eboo,sio mtemi wa jamiiforums kweli huyu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Msomi mzima haujui hata mfumo wa uzazi na utungwaji wa mimba ulivyo!

Kwani mtoto wa kutoka kiunoni mwako ni lazima ufanane naye? Shem on you!

Halafu kwanini wanawake wawili wa kutoka maeneo tofauti wazae na mtu mmoja aitwaye pro halafu usingiziwe wewe?

Usitufanye sote ni mabwege humu ndani ya Jf.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom