Uko vizuri
Nina 1 million hapa biashara gani itanitoa kipindi hiki cha magu
chief1 wewe ni mmoja ya watu smart sana mliopitia huu uzi. Nilitegemea swali kama hili tangu page ya kwanza, but sikumbuki kama kuna mtu aliuliza, ni kama watu waliosoma huu uzi wote wako financially stable.
Mil 1 ni pesa ndogo lakini trust me inaweza kukubadili maisha kama ukiwa una uthubutu na pia uwe smart.
Toa 50,000 kwaajili ya research, kama upo Dar zunguka kwenye hizi Bar, viunga vya chakula, mabucha nk ongea nao biashara. Waambie una mbuzi wakubwa, wazuri, wa kienyeji. Wengi hununua kati ya 70-90 saa zingine hadi zaidi. Wape offer kuwa wewe utawapa mbuzi kwa 60,000. Mfanyabiashara makini hawezi kukataa hii offer, elfu 10 ni kubwa sana kwenye biashara ndogo ndogo.
Ukijiridhisha kuhusu soko, tafuta usafiri. Mtafuta boss mwenye "Toyota carry", wengi huchukua 20,000 kwa siku kutoka kwa madereva wao. Wewe mpe offer ya 30,000 kwa siku ili akubali bila kinyongo.
Weka mafuta ya 40,000 kanyaga wese hadi sehemu 1 inaitwa "kwa makocho" ipo wilaya ya Chalinze, anavuka wami mbele kidogo. Kule nimeshuhudia mbuzi wakiuzwa kati ya 35-40 elfu. Nunua mbuzi 20 kwa 400,000 jumla laki 800,000. Mzunguko wote mpaka hapa utakua umetumia 920,000 - una kiakiba cha 80,000.
Rudi Dar faster uza mbuzi wako kwa 60,000 kwa wale wateja wako. Utakua umegonga 1,200,000. Una faida ya 200,000. Fanya hivi mara 4 kwa wiki. Kila wiki utafuwa na 800,000 faida. Fikiria kupanuka na kupanuka - go an extra mile, kuwa consistent, kubali kuumia.
Biashara sio smooth kama nilivyoandika, lakini wewe ndie mwenye password ya kuifanya smooth. Mwanzo mgumu - lakini haimaanishi kuwa haiwezekani. Changamoto ziko nyingi - fanya maamuzi ya haraka. Kumbuka "growth is everything" anza na mbuzi 20 lkn fikiria kusupply mbuzi 100 au hata 500.
Leta mrejesho uwape nguvu masela.
Kila la hkeri.