Jinsi nilivyoibiwa gari kizembe bar

Jinsi nilivyoibiwa gari kizembe bar

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Maisha ya mwanadamu yamejaliwa na kumbukumbu nyingi sana, nyingi na mbaya, zenye kutufundisha na zenye kuburudisha. Al mradi ni matukio yalitokea na yakapita.

Nakumbuka mwaka 2018, tarehe kama ya leo na mwezi huu huu, nikiwa na gari ndio lina siku nne tu tangu lipite pale gati namba mbili na kutua mikononi mwangu, mzee nikajitoma nalo Bar, Maryland Mwenge.

Kilichonipeleka hapo bar, niweze kukutana na mrembo mantashahu, chotara wa Kigiriki na Kichaga, mtoto mwenye urefu wake wa futi tano point kumi na moja, chuchu mkuki, viwango vya kimataifa.

Kabla sijafika Maryland nilikuwa Break Point ya mjini, kisha nikaingia The Governors Kinondoni, lakini cha kustaajabisha nilikuwa nikikutana na sura zilezile.

Nilipofika Mwenge nikampigia bibie kwamba niko ndani ya nyumba namsubiri yeye ili tuanze safari ya kwenda Morogoro kula raha za dunia.

Kabla hajafika, wakaingia jamaa ambao nimekuwa nikiwaona tangu Break Point na The Governors.

Moja kwa moja wakaja kwangu, mmoja akatoa bastola na kuniwekea kidevuni, wakati ubaridi wa mtutu wa bastola ukikikera kidevu changu, mara nikaona mwingine naye anatoa bastola yake na kupiga risasi tatu hewani, wakasema niwape funguo ya gari.

Nikawapa funguo, wakaondoka huku wakipiga risasi hewani kuwatisha watu wasiwafuate.

Nikabaki hapo bar nimepigwa na bumbuwazi. Nikawapigia simu rafiki zangu mapolisi akiwemo Mentor wa JamiiForums.

Jitihada za kulisaka gari zikaanza mara moja. Mimi na ubwege wangu nikaendelea kubung'aa pale Maryland kama kada wa CCM aliyekosa wali maharage wa kampeni.

Hazikufika dakika kumi, jamaa (majambazi) wakarudi tena na kunikuta pale, wakanibeba msobemsobe hadi kwenye gari yao, wakanitupia humo na wakatoa gari mbio huku wakiendesha kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tulipofika maeneo ya Udasa tukakuta gari imezimika, na haiwezi kuwaka mpaka uweze kugusa sehemu fulani.

Ilikuwa kila ikipiga kengele watakiwa kugusa sehemu hiyo. Basi wakaniambia niwaonyeshe sehemuya kugusa ili gari isizime.

Nikapagusa nikawaambia wawashe, wakaiwasha, wakanisukumia huko chini wakatoka nduki na kuniacha kwenye viwanja vya chuo.

Nilitoka nduki hadi nilipopata daladala la kwenda Makumbusho nikapanda huku nikitweta, nikarudi nyumbani Kijitonyama.

Usiku mida ya saa tatu nikapigiwa simu kuwa gari yangu imepatikana mitaa ya Kimara Baruti ilizimika barabarani.

Kile kitufe kilikuwa kina sense fingerprint walishindwa kuendelea kuliendesha gari lile na hawakuwa na sehemu nyingine ya kunipata.

Tangu siku hiyo nikajifunza kwamba sitakiwi kuonana na mtu mara mbili sehemu mbili tofauti.

Pia nikajifunza nikipatwa na jambo lolote ni lazima nihame eneo la tukio.

Kingine nilichojifunza ni umuhimu wa mifumo ya usalama kwenye gari, gps for vehicle tracking nk.

Pia nilijifunza umuhimu wa kuwa na bima kubwa kwa chombo chako.

Hiyo ndiyo kumbukizi yangu ya Alhamis ya leo
 
Tangu siku hiyo nikajifunza kwamba sitakiwi kuonana na mtu mara mbili sehemu mbili tofauti.

Pia nikajifunza nikipatwa na jambo lolote ni lazima nihame eneo la tukio.

Kingine nilichojifunza ni umuhimu wa mifumo ya usalama kwenye gari, gps for vehicle tracking nk.

Pia nilijifunza umuhimu wa kuwa na bima kubwa kwa chombo chako.
Asante umetufundisha na wengine pia huku
 
Hapo itabidi tuongee vizuri kuhusu mfumo wa usalama unaotumia finger print. Je, unakubali idadi ya watu wangapi?

Namaanisha kama gari tunaendesha watu wawili, wote mnaweza kusajiliwa mkatumia mfumo bila tatizo?

Hapo kwenye bima kubwa nilishajifunza kitambo sana.

Hiyo ya kuona watu walewale maeneo tofauti inatakiwa ikushtue. Nikifika eneo lolote hua lazima niscan mazingira kwanza kuona watu waliopo eneo husika. Hata nikiketi ntaendelea kukagua mazingira kabla ya kufanya chochote, hii mara nyingi inaweza kuwakera wale nilionao. Wanaona kama siwapi attention, nna mambo yangu mengine kichwani, ila nikishaona mazingira na aina ya watu eneo hilo kwa kiasi flani yanaridhisha, tunaendelea na ratiba zetu.

Mshukuru Mungu ulibahatika kuipata gari.

Mentor mtumishi wa Bwana ameadimika sana.
 
Maisha ya mwanadamu yamejaliwa nankumbukumbu nyingi sana, nyingi na mbaya, zenye kutufundisha na zenye kuburudisha. Al mradi ni matukio yalitokea na yakapita.

Nakumbuka mwaka 2018, tarehe kama ya leo, na mwezi huu huu, nikiwa na gari ndio lina siku nne tu tangu lipite pale gati namba mbili na kutua mikononi mwangu, mzee nikajitoma nalo Bar, Maryland Mwenge.

Kilichonipeleka hapo bar, niweze kukutana na mrembo mantashahu, chotara wa Kigiriki na Kichaga, mtoto mwenye urefu wake wa futi tano point kumi na moja, chuchu mkuki, viwango vya kimataifa.

Kabla sijafika Maryland nilikuwa Break Point ya mjini, kisha nikaingia The Governors Kinondoni, lakini cha kustaajabisha nilikuwa nikikutana na sura zilezile.

Nilipofika Mwenge nikampigia bibie kwamba niko ndani ya nyumba namsubiri yeye ili tuanze safari ya kwenda Morogoro kula raha za dunia.

Kabla hajafika, wakaingia jamaa ambao nimekuwa nikiwaona tangu Break Point, na The Governors.

Moja kwa moja wakaja kwangu, mmoja akatoa bastola na kuniwekea kidevuni, wakati ubaridi wa mtutu wa bastola ukikikera kidevu changu, mara nikaona mwingine naye anatoa bastola yake na kupiga risasi tatu hewani, wakasema niwape funguo ya gari.

Nikawapa funguo, wakaondoka huku wakipiga risasi hewani kuwatisha watu wasiwafuate.

Nikabaki hapo bar nimepigwa na bumbuwazi. Nikawapigia simu rafiki zangu mapolisi akiwemo Mentor wa JamiiForums.

Jitihada za kulisaka gari zikaanza mara moja. Mimi na ubwege wangu nikaendelea kubung'aa pale Maryland kama kada wa CCM aliyekosa wali maharage wa kampeni.

Hazikufika dakika kumi, jamaa (majambazi) wakarudi tena na kunikuta pale, wakanibebamsobemsobe hadi kwenye gari yao, wakanitupia humo na wakatoa gari mbio huku wakiendesha kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tulipofika maeneo ya Udasa tukakuta gari imezimika, na haiwezi kuwaka mpaka uweze kugusa sehemu fulani.

Ilikuwa kila ikipiga kengele watakiwa kugusa sehemu hiyo. Basi wakaniambia niwaonyeshe sehemuya kugusa ili gari isizime.

Nikapagusa nikawaambia wawashe,wakaiwasha, wakanissukumia huko chini wakatoka nduki na kuniacha kwenye viwanja vya chuo.

Nilitoka nduki hadi nilipopata daladala la kwenda Makumbusho nikapanda huku nikitweta, nikarudi nyumbani Kijitonyama.

Usiku mida ya saa tatu nikapigiwa simu kuwa gari yangu imepatikana mitaa ya Kimara Baruti ilizimika barabarani.

Kile kitufe kilikuwa kina sense fingerprint walishindwa kuendelea kuliendesha gari lile na hawakuwa na sehemu nyingine ya kunipata.

Tangu siku hiyo nikajifunza kwamba sitakiwi kuonana na mtu mara mbili sehemu mbili tofauti.

Pia nikajifunza nikipatwa na jambo lolote ni lazima nihame eneo la tukio.

Kingine nilichojifunza ni umuhimu wa mifumo ya usalama kwenye gari, gps for vehicle tracking nk.

Pia nilijifunza umuhimu wa kuwa na bima kubwa kwa chombo chako.

Hiyo ndiyo kumbukizi yangu ya alhamis ya leo
Yani hao wezi wathubutu kujaribu kuniibia Mercedes Benz yangu Vision GT, 12 million USD patachimbika asee. Huo mkono nitakavyoutembeza itakuwa gumzo la aina yake
01mercedesamgvisiongt.jpg
 
Back
Top Bottom