25/08/22 Wilayani Kisarawe kata ya Sanze mtaa wa Kibon'gwa ndipo ilipokuwa kiwanda changu kidogo cha kutengenezea silaha bandia kwaajili ya filamu na video za muziki.
Ilikuwa saa 10:30 jioni muda ambao niliacha kufanya kazi na kutaka kutoka ndani ili niende kupata chakula cha mchana lakini kwa mbali nikaona gari nyeusi aina ya Noah ikija upande wangu isivyo kawaida nikatia shaka lakini nikajipa ujasiri na kutulia. Walishuka askari kama 8 wakiwa na silaha Ak47 kila mmoja na mwingine kiongozi wao alikuwa na bastola. Wakaniamuru nikae chini nikatii.
Waliniambia niingie ndani nikatii na pia wakaniamuru nilale nikalala wakanifunga mikono kwa nyuma na kamba za viatu vyangu kwakua hawakua na pingu. Wengine wakaziona silaha kwenye chumba cha pili na kupeana maelekezo "wahi silaha zile haraka" wakazikimbilia na kuziangalia kwanza "usiguse kwanza chochote vipige picha na video" alisema askari mwingine.
Baada ya kumaliza kupiga picha wakaanza kuzichukua na kugundua kuwa sio halisi na ndipo waliposhikwa na mshangao na askari mwingine akaanza kunipiga kwa mguu wenye buti mabegani na kunikanyaga mgongoni na kichwani akitaka niwaoneshe silaha halisi na mimi nikawajibu " mimi sio mhalifu bunduko hizi huwa natengeneza kwaajili ya filamu na video za muziki" hawakutaka kunielewa na kutaka nioneshe bunduki ambayo huwa naangalizia ili kupata vipimo halisi kwani bunduki zangu zilifanana kabisa na za kwao, nikawaelewesha kuwa huwa najifunza kupitia mtandao wa YouTube.
Wakaniuliza elimu yangu nikawaeleza ni kidato cha 4 na nilifeli. Baada ya muda kidogo ikaja gari nyingine aina ya difenda na nikaamriwa niingie kwenye gari hiyo na nikapelekwa kituo cha polisi cha Kisarawe. Nikachukuliwa maelezo na kuwekwa mahabusu.
Asubuhi ya siku iliyofuata nikapelekwa mkoani ambako kuna kituo kikuu cha mkoa wa Pwani kipo Kibaha. Nikakutana na jopo la wazee kama 12 wakinihoji na nikawaeleza kuhusu kazi zangu nilizowahi kufanya ka tamthilia ya Chini ya Kapeti, Huba, Hatia, Moyo nk. P
ia nilisha fanya kazi kwenye video kama Unapunguza utamu ya Mabantu na Harmonize, Bakhresa ya Harmonize, Tunda man Mtu mbadi, Rayvany Tecquero nk.
Walifurahi na kusema hakuna kesi na ndipo walipoamuru nirudishwe Kisarawe kwaajili ya dhamana. Nikalala tena Kisarawe na kutoka Jumamosi kwa dhamana

Upvote
1