Story yako kama yangu tu, mimi na sister wangu ila sio tumbo moja tulikua tunasoma darasa moja.
kipindi nipo form two ndo niliamiaga hiyo shule aliyokuwa anasoma huyu ndugu yangu wa kike,tulikua tunasoma darasa moja.
Tulivoingia form 3 tukatengana madarasa sister yeye alikua kwenye masomo ya biashara, Kuna shoga ake na sister alikuaga ananipenda sana anaitwa zawadi
Huyo dem alikua anakujaga sana hom kwa shoga yake yaanib(sister wangu)kumbe huyo dem ndo alikua ananifukuzia mimi[emoji23].
Nikaja kusikia stor kwamba me natembea na zawadi, mpka darasani ikawa ndo story nataniwa sana wakati hata sijawahi kutoka na huyo zawad. Yaani hata mazoea hatuna zaid ya salam. Kumbe huyo zawad ndo aliwaambia madem wenzake kwamba jbst ni mchumba wangu na sister alikua anajua kinachoendelea ila anakausha.
Huyo zawad akawa anajiletaga sna tu hom anajifanya kuja kumtembelea shoga ake kumbe hana lolote ananifukuzia ananitaka. Kipindi hicho tupo form four sasa ikaja ikatokea tukazoeana kama ma rafik maana sister ndo kama alituunganisha kishkaji.
Yule zawad sikuwahi mtongoza ila alikua anaitega sana nimtongoze, tulikuwa tunachart ananichatisha sana sio kawaida ila sikuwahi mtongoza, mpaka tunamliza form 4 sikumtongozaga tukaja kupoteana maana aliondokaga na akawa hapatikanagi.
Ikapita miaka 5 siku moja naperuzi FB nikawa naangalia walioniomba urafiki maana walikua wengi kama 30 hivi,mimi huwa nakubali urafiki mtu mpaka nimkague kwanza picha zake au vitu anavyopost kama nikivielewa nikiona haeleweki nafuta na kama hajaweka picha nafuta pia.
Yule zawad nikaona picha yake kumbe aliniomba urafki mda tu nikamcheki messenger tukabadilishana na namba tukatumiana picha siku hiyo nilijikuta nampenda na kumtaman sana ila nikakausha kwanza.
Nikaona kesho yake status kampost brother mmoja anaonekana ndo mtu wake kutokana na caption aliyoandika, alafu jamaa anaonekana kanizidi hata uchumi maana nilikua najitafuta
Nikaanza utaratibu wa kumtongoza zawadi nisijechelewa zaidi, aliniambia ukwel nimechelwa na ana mtu wake wanakaribia kuoana!! Akasema ananipenda hata yeye ila nimechelewa akanimbia alianza kunipenda toka tupo shule ila ndo nilikua najifanya Mgumu simuelewi. Nikamjibu ulikua utoto dah!
Nilikubaliana na hali halisi tukabaki washkaji tu japo huwa ananitafuta sana yeye kuliko mimi kumtafuta kwenye sim ,ananiona kama rafk tu na mimi nilishakubaliana na ukweli tunaheshimiana tu.
Ila roho iliniuma sana nikajuta sana bora ningemlaga kipindi kile, dem pisi kali balaaa nimeikosa