Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 997
- 1,220
Nilikutana na rafiki niliyesoma nae msingi miaka mingi mno iliyopita akiwa kwenye gari stendi tayari kwa safari.....nami nilikuwa nafika hapo kwa ajili ya usafiri wa kwenda sehemu. Tukiwa na hamu ya kuongea mengi lakini tukiachwa na muda kwani gari yao ilianza kuondoka; ikabidi anitajie namba zake za simu kwa haraka.......nikaziandika katika simu yangu.
Ilipofika jioni nikampigia Ili nijue safari yao ilikuaje. Ajabu simu ikapokelewa na mwanamke. Nikadhani kuwa ni mkewe hivyo nikamuuliza kama mwamba amefika salama au la. Akaonyesha mshangao na kuniambia kwamba nimekosea namba....nikakata. Nikaichunguza tena ile namba nione kama nimekosea niliyempigia au la. Nikakuta ni ile ile 'niliyoisikia' pale nilipotajiwa. Nikachoka na maswali meeeengi yakajaa kichwani.
Kufupisha stori, sikuacha kupiga Kila baada ya wiki. Hatimaye mazungumzo yakatupeleka mpaka kwenye utambulisho ambapo mwenzangu alikuwa wa Musoma huko (tofauti kabisa na eneo alilokuwa yule rafiki'angu). Safari Moja kweli ikaanzisha nyingine na hatimaye nauli zikatumwa wimbo 'Siji' wa Zuchu akaupiuzia ye akaja na hatimaye Sasa zinasubiriwa Dua tu za kubariki hili unganiko.
Nilipomtafuta yule rafiki alishangaa sana tukagundua kuwa kumbe niliposikia 'tatu' ilikuwa 'tano'.
Uzazi una mvuto wenye nguvu sana aisee!