Jinsi nilivyokuwa nadhani nimeokoka kumbe ni wakala wa ibilisi kanisani

Jinsi nilivyokuwa nadhani nimeokoka kumbe ni wakala wa ibilisi kanisani

Mwaka 2017 nilipata neema ya wokovu, niliombewa sala ya toba na nikakaribishwa rasmi kundini, kwenye kuitenda kazi ya BWANA.

Maisha yangu kabla ya wokovu yalikuwa ni maisha meusi, ulevi, umalaya, uvutaji wa mioshi mbalimbali, uhuni, udhalimu, uporaji, udhulumaji, na ubazazi usiolezeka.

Maisha yangu yalinifanya nichukiwe na wengi, ila wengi waliniogopa na waliogopa kunisema na kunikosoa.

Ukiwa mwovu, fanya urafiki na polisi, hii ilikuwa ndio njia yangu kubwa ya kupata ulinzi.
Ukinipeleka polisi utalala mahabusu wewe huku Mimi mtuhumiwa nikikuletea chai na bigijii.

Maisha yangu ya mwanzo ya wokovu yalikuwa mazuri, hakika hata Mimi mwenyewe nikajiona hakika nimebadilika.

Hamna kitu kibaya kwenye maisha ya mwanadamu kama mazoea. Siku zilienda na Mimi nikazoea wokovu, nikalizoa na jina la YESU.

Taratibu taratibu nikaanza ku slide back na kuurudia utu wangu wa kale.

Kanisani nikaacha kutoa sadaka, nikawa naiba sadaka nikipewa zamu ya ukisanyaji. (Nilipewa uzee wa kanisa)

Nikaanza kunyandua binti mmoja baada ya mwingine. Nikaanza kuwafundisha mabinti walokole kunywa pombe, wengine nikawafundisha na uvutaji wa sigara na mioshi mingine, nikawafundisha maisha ya starehe za usiku.

Miingoni mwa mabinti niliowapeleka puta ni binti wa mchungaji, mwanafunzi wa kidato cha tatu tu.

Nikaanza kuwatapeli waumini wa kanisa. Wengine niliwadanganya kwamba Mimi naweza kuwaagizia Magari mazuri kupitia kampuni ya SBT.

Waliponipa pesa zao nikazitumia.

Wengine niliwauzia Beach plots feki wilayani Mkuranga na Bagamoyo.

Mchungaji nilimrubuni anipe milioni 50 nimletee mganga kutoka Nigeria atakayempa nguvu za kuvuta watu wengi na kutenda MIUJIZA mikubwa. Licha ya kukataa sana, mwisho wa siku nikafanikiwa kumrubuni na akakubali.
Jina langu likaanza kupata rangi nyeusi, Mambo mengi niliyoyatenda sirini yakaanza kuonekana hadharani.

Mabinti wanne walitengwa na kanisa kwa kushika ujauzito nje ya ndoa, zote zikiwa ni mimba zangu.

Kanisa nikawa nimelichafua kwelikweli. Nikaacha kusali na nikabadilisha namba za simu.

Wito wangu kwa umma usiwaamini watu haraka haraka. Hata Biblia inasema msiziamini kila roho ila mzichunguze
Duh wapo sana watu kama hawa chini
Ya mwamvulli wa Dini "TRUST NO "
 
Wacha bwana huyu ndio Mzee Bujibuji og naemjua!
Stori za kuchangamsha genge
Wapi Giresi?

Karibuni tupate Alkasus mujarab!
☕☕☕☕
 
Luka 6:41-45​

Kwa nini wakiona kibanzi jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako. “Mti mzuri hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri. Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili. Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
 
Ila mabandiko yako ya hivi karibuni yanatia shaka sana kama ni wewe kweli au kuna kiumbe ka hack akaunti yako. Tunaweza kuja sikia kumbe umehamia CCM. Muda utaamua....
 
Mk

Luka 6:41-45​

Kwa nini wakiona kibanzi jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako. “Mti mzuri hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri. Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili. Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
Mkuu unayo NAFASI ya KUTUB.MUNGU HAJAKUTUPA MJA WAJE WAKE
 
Back
Top Bottom