Jinsi Nilivyomtapeli Mganga wa Kienyeji: Simulizi ya "Mjanja Aliyekutana na Mwerevu"

Jinsi Nilivyomtapeli Mganga wa Kienyeji: Simulizi ya "Mjanja Aliyekutana na Mwerevu"

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Watu wengi husema mganga wa kienyeji ni mtu wa kuogopwa. Wanasema ana macho yanayoona mbali na majini yanayompa taarifa za kila anayemtembelea. Lakini siku hiyo, niliamua kuthibitisha kuwa hata "nguvu za giza" hupigwa na giza la njaa na tamaa.

Mtego wa Kisaikolojia
Mganga huyu, ( jina kapuni") alikuwa maarufu kwa kutajirisha watu kitapeli.
Mimi Nilijua udhaifu wake mkuu: Tamaa.
Waganga wengi hutapeli watu kwa kutumia hofu, lakini mimi nilitumia "ndoana ya utajiri."

Nilifika kilingeni kwake nikiwa nimevaa suti ya gharama kubwa (niliyokodi), nimebeba mkoba wa ngozi, na simu mbili za kisasa ambazo zilikuwa zikiita kila dakika (marafiki zangu niliowaelekeza wanipigie). Nilionekana kama mfanyabiashara aliyefanikiwa ambaye ana "mzigo" wa maana.

"Dili" la Dhahabu ya Bandia
Baada ya kutoa fedha nyingi ya "kuingilia kilingeni" nilutoa laki..😂ili kumchanganya akili, nilimweleza shida yangu:

"Sheikh, mimi ni mfanyabiashara wa madini. Nina kilo tano za dhahabu ambazo nataka kuzisafirisha kwenda nje, lakini nahofia usalama. Nataka unipe kinga ya giza ili polisi au mashine za uwanja wa ndege zisizione."
Nilimwonyesha "sampuli"—vipande vya chuma vilivyopakwa rangi ya dhahabu kwa ustadi mkubwa. Macho yakamtoka pima!😂 . Badala ya kunipa kinga, tamaa ilimjaa. Alianza kuwaza jinsi ya kunidhulumu zile "dhahabu."

Sasa nikaanza michezo yangu !
Mchezo wa Kubadilisha Karata

Mganga aliniambia, "Ili dawa ifanye kazi, lazima hizi dhahabu zilale kilingeni kwa siku tatu zikizungukwa na kafara ya shilingi milioni tano taslimu." Nikamkubalia lakini Hapo ndipo nilipomgeuzia kibao.

Nilimwambia, "ndugu yangu, sina cash hapa, lakini nina hizi kilo tano. Nitakuachia kilo mbili kama dhamana, unipe milioni mbili nikanunue vitu vya kafara, kisha nikirudi nitakupa faida mara mbili."
Kwa kuamini kuwa kilo mbili za dhahabu zina thamani ya mamilioni, alitumbukia kwenye mtego. Alitoa akiba yake ya milioni mbili akiamini amepata "dili" la maisha.

Niliziweka dhahabu za bandia kwenye sanduku lake la siri, nikachukua pesa, na kutokomea.

Siku tatu zilipopita na sikurudi, jamaa aligundua kuwa alichobaki nacho ni vipande vya chuma vilivyopakwa rangi.

Hakuweza kwenda polisi kuripoti kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa anafanya utapeli wa kishirikina.


Waganga ni binadamu: Wanaongozwa na hisia zilezile za kibinadamu—tamaa na hofu.Watu wengi huibiwa kwa sababu wanatoa mamlaka ya akili zao kwa watu wengine.
Mtapeli huingia mkenge akikutana na mjanja zaidi

Mganga alishindwa kutumia "majini" yake kugundua kuwa dhahabu ni feki kwa sababu akili yake ilikuwa imezibwa na tamaa ya utajiri wa haraka.😂

sehemu ya pili

Baada ya siku saba kupita bila mimi kurudi, na simu zangu zote zikiwa hazipatikani, jamaa alianza kuhisi mapigo ya moyo yakienda kasi. Aliamua kuchukua kile "kilo mbili za dhahabu" na kwenda kwa sonara mmoja wa siri mjini ili kuzigeuza ziwe pesa taslimu.
Ukweli Mchungu

Sonara alizitazama zile chuma kwa sekunde mbili tu, kisha akacheka kwa dharau. "Akamwambia..hivii ni vipande vya chuma viliyopakwa rangi ya dhahabu kwa ustadi. Thamani yake haifiki hata shilingi elfu tano."

Jamaa alihisi dunia inazunguka. Ile milioni mbili aliyonipa ilikuwa ni akiba yake ya miezi sita aliyowatapeli wajane na vijana wanaotafuta kazi. Alikuwa ameingia kwenye mtego wa "utapeli wa kioo"—alichozoea kuwafanyia wengine, kimefanywa kwake.!

Kiuhalisia mganga hategemei tu dawa; anategemea na kujiamini pia (Confidence).
Mara tu alipojua ametapeliwa na binadamu wa kawaida, hofu ilimjaa. Alianza kuwaza: "Ikiwa huyu kijana kanichezea hivi, je, majini yangu yameenda wapi? Je, mimi bado ni mganga?"

Siku iliyofuata, mteja mmoja alikuja kilingeni kwake. Jamaa, badala ya kutoa utabiri kwa mbwembwe kama zamani, alianza kutetemeka sauti. Alishindwa hata kupiga ramli chonganishi😂. Wateja walianza kuona kuwa "mzee amepoteza nguvu

Sasa ikaanza Presha ya Madeni na Fedheha
Taarifa zilianza kusambaa chini kwa chini mtaani kuwa mgangav"amepigwa" na kijana mmoja mtanashati.
Sifa yake ya kuwa mtu anayeona yajayo ilifutika papo hapo. Watu walianza kumcheka.
"Mganga gani anashindwa kujitabiria kuwa atatapeliwa?" Hilo ndilo lilikuwa swali la kila mtu.

Kufungwa kwa Kilinge
Ndani ya mwezi mmoja, kilinge cha jamaq kiligeuka kuwa gofu. Alishindwa kulipa kodi ya nyumba kwa sababu wateja walitoweka. Alilazimika kuhama usiku wa manane na kuelekea kijijini kwao kuanza maisha ya kulima, huku akiwa na chuki kubwa!

Placebo Effect ya Upande wa Pili: Mganga anapoamini amepoteza ulinzi, akili yake inakata tamaa (mental breakdown), na hapo ndipo "nuksi" ya kweli inapoanza—sio kwa sababu ya uchawi, bali kwa sababu ya kupoteza hali ya kujiamini.

Karma ya Kisaikolojia: Unapoishi kwa kuwatapeli wengine kwa kutumia hofu, siku ukigundua kuwa nawe unaweza kutishiwa au kutapeliwa, mfumo wako wa ulinzi wa akili unaporomoka kabisa.
Simulizi hii inatufundisha kuwa hofu ndiyo inayowapa waganga nguvu. Ukiondoa hofu na ukatumia akili ya kawaida (logic), unagundua kuwa wao pia ni binadamu wenye madhaifu makubwa.

NB: hii simulizi haihusiani na kuachana na kilinge changu😂
 
Mganga aliduwaa, akapata gagaziko, bumbuwazi na butwaa pamoja na mshangao wenye weweseko, mshituko mkubwa, pale sonara alipotamka NENO ELFU 5.
5852e011-c96f-4830-801a-2b6b50b33585.jpeg
 
Hapo sasa Leo nimegundua kumbe ujanja wako sio uchawi, ni tamaa tu 😏 Umemtapeli tapeli mwenzio kisha unakuja kutupigia story za ushindi huku Sasa hiyo milioni mbili bado ipo au na wewe majini ya mjini yameshaichukua ? Maana jasusi bila hela ni sawa na mganga bila manyoya!l?
 
Kaka mshana nijibu komenti yangu na mimi nijisikie, maana mastaa hawataki kujibu komenti, sijasema wewe sio staa, wewe ni nyota kaka.

Jamani mganga wa watu hadi huruma,
Ila ndo akome sasa tutafenyeje, jua na mwezi vyote vinaandama.
 
Kaka mshana nijibu komenti yangu na mimi nijisikie, maana mastaa hawataki kujibu komenti, sijasema wewe sio staa, wewe ni nyota kaka.

Jamani mganga wa watu hadi huruma,
Ila ndo akome sasa tutafenyeje, jua na mwezi vyote vinaandama.
Hahahaha Bajuda ni ipi hiyo ambayo sijaijibu mkuu?
 
Back
Top Bottom