kudot2020
Senior Member
- Jan 8, 2020
- 122
- 161
Endelea bhnBoss mimi mwenyewe muhanga ndugu yangu, hivyo nilitaka kulisongesha tu hili story ndio maana nimeomba ridhaa yenu mkuu 666 namba ya shetani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Endelea bhnBoss mimi mwenyewe muhanga ndugu yangu, hivyo nilitaka kulisongesha tu hili story ndio maana nimeomba ridhaa yenu mkuu 666 namba ya shetani.
Utajiri mwingine aurithiki wa makafaraHafu vijana wanataka utajiri bila ya kufanya kazi kwa bidii, Sasa Matokeo Yao ni huu ujinga uliokubuhu
NitagMiaka kama 13 imepita wakati huo tukiwa Ilboru sekondari nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye tulikuwa tunaishi jirani kwenye jiji moja la kanda ya ziwa
Tulikuwa hatufahamiani kabla, tulifahamiana wakati tunaanza kidato cha kwanza tulipokuwa shule na urafiki ukaanzia hapo
Siku moja tumerudi nyumbani likizo alinikaribisha nyumbani kwao nami nikafika
Tukiwa pale nyumbani aliniambia kuwa mama yake mzazi aliondoka yaani waliachana na baba na hivyo baba yake akaoa mke mwingine ambaye hakuwa na umri mkubwa sana kama 24 hivi
Familia hiyo yenye asili ya kaskazini mzee alikuwa na gereji kubwa hapo jijini, maduka mawili ya vifaa vya ujenzi na spea za magari
Pia alikuwa na uwekezaji wa madini huko kahama sasa siku hiyo tunaondoka kutoka nyumbani kwao alinisindikiza ,alichukua ufunguo wa gari akanambia panda humu nikusindikize ,nilishangaa sana kwamba kwa umri miaka 15 anajua kuendesha gari
Basi akaendesha tulipofika mjini akanambia kwanza tupige misele mjini mara tunaenda kuwatafuta mademu waliokuwa wanasoma nao huko seminary primary
Katika urafiki wangu na yule kijana alipenda starehe sana kuliko kusoma na likizo nzima nikimwambia tuanze kusoma anakwambia yupo bize mara aende dukani kumsadia mfanyakazi wao, mara aendeshe gari mpaka kahama, Geita na hakuwa na leseni ila pesa kila kitu njiani
Hata tulipokuwa shuleni dogo yeye hana muda wa kusoma stories zake ni pesa, madem na magari
Tukiwa kidato cha tatu dogo walivurugana na walimu na wakamuita mzazi wake kama hamhamishi watamfukuza shule hivyo mzazi wake akaamua kumhamishia private moja huko Bukoba
Urafiki uliendelea na tulikuwa tunakutana nyumbani kipindi cha likizo na maisha yake ni kudrive magari ya baba yake
Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka aliscore 0 wakati huo mimi nikiwa na 3 pia alichangia mimi kupata hizo alama kwa misele na stories zake
Baba yake alipopata habari kuwa mwanae aliscore 0 alimgombeza sana na wala kijana hakushtuka yeye aliendelea kula maisha na magari ya baba yake na pikipiki muda mwingine
Baba yake akamtaka amrudishe shule kijana akagoma baba yake akampeleka gereji yake afundishwe ufundi ,kijana akagoma mzazi akamtishia kumfukuza nyumbani lakini baadae kijana akakubali
Siku moja alichukua gari la baba yake akaondoka kusikojulikana na baada ya wiki moja akajikuta yupo lockup Dodoma kituo cha polisi kwa kuendesha gari bila leseni,mzazi wake aliambiwa akaenda akamtoa akamrudisha nyumbani na akamwambia mzazi wake hataki ufundi wala kitu chochote anahitaji akae nyumbani tu na hata kukaa dukani hataki
Basi mzazi wake akamuacha,kijana ni kudrive magari ya mzee mjini na kama hana hela ya mafuta anamuomba mama mdogo hela anaenda kujaza ,akaanza mazoea na mama mdogo wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi
Baba yake akaanza kuwa na mashaka kati ya kijana wake na mkewe ,baada ya baba kuwatia mashakani,kijana na mama mdogo wakaanza kuandaa mikakati ya kumuondoa uhai
Wakapanga kuwa wakisha muondoa huyo mzee wanauza kila kitu wanahamia Mbeya au Tunduma lakini kabla ya hayo ili kuwarahisishia kuchukua mali zote lazima watumie mbinu ili mzee aandike wosia wa kuwagawia mali kijana na mama mdogo ,cha kukuongezea ni kwamba mama mdogo alikuwa amezaa na mzee watoto wawili wa kike na kijana alikuwa na mdogo wake mmoja wa kike ambaye muda mwingi anasomea Uganda
Mipango ya kutaka kuandaa wosia inaanza kufanyika na lengo la wosia ni kuwa baada ya kumuondoa uhai ndugu wa marehemu wasiwe na nguvu ya kuongelea mali na sasa na mimi nadokezewa hili dili kwa posho ya milioni 5 nikifanikiwa kufanya yafuatayo
Itaendelea................Nilienda kunywa maji sasa naendelea
Baada ya kupewa hilo dili la milioni 5 Dada(mama mdogo wa jamaa) aliniita hotel moja maeneo ya Ghana ilikuwa saa 12 jioni akaanza kunitaka nifanye yafuatayo
Kwanza ataniletea documents za mzee vitambulisho,leseni na vitu vingine niende nimtafute mwanasheria tuandike wosia kisha tutumie mbinu na huyo mwanasheria zipate muhuri wa mahakama na akanipa orodha ya mali kwenye karatasi na picha ya saini ya mzee ,passport za mzee,huyo mwanamke,passport za watoto wote ,akanipa na akanipa barua ya serikali za mitaa iliyogushiwa na vyeti vya kuzaliwa na cheti cha ndoa
Akanipa milioni moja kwa kuanzia na nikimpata mwanasheria aliyetayari tutampa kitu kidogo na mwanasheria asiwe wa Mwanza wala Shinyanga
Nikaingia kazini kumsaka mwanasheria, nilipokuwa nawahusisha wanasheria kama watatu hivi walikataa ,wakawa wanashauri kwa nini tusitumie mbinu za ushawishi wa kawaida yeye mzee aandike wosie kwa kigezo cha kuhofia ukoo kuwanyang'anya mali lolote likitokea kwa mzee?
Iliposhindana kwa hao watatu nikaamua kwenda chuoni SAUT nikampata kijana mmoja akawasiliana na ndugu yake akakubali kufanya hiyo kazi alikuwepo Tabora na akawataka hao wanafamilia ndo waende Tabora na nyaraka zote zinazohitajika na kiasi cha milioni 7
Nikamwambia mdada akakubali nikampa nyaraka zake zote akamwambia msela wake wakapanga tarehe ya kwenda Tabora
Kweli zoezi lilifanikiwa na cha kwangu wakanipa milioni mbili na nusu ikabaki milioni mbili na nusu ambayo wangenipa baadae baada ya Dada kudai hela ametumia yote nisubiri akusanye
Baada ya miezi kadhaa mdada alinipigia simu akinihitaji mara moja hotel moja maeneo Bwiru ,nikataka kujua kulikoni akanambia niende tu kuna mazungumzo,nikataka nijue mzee alipo kwanza akanambia yupo nje ya nchi basi nikaondoa wasiwasi nikaenda
Alikuwa na msela wake wanakunywa pombe basi nami nikajumuika pale mezani ,siku hiyo ndo nilijua malengo ya kutaka kujimilikisha mali hii ni baada ya kulewa kijana akawa anatamka wazi wazi kuwa ile mali ni yake na muda wowote atamuua mzee apishe ,asiwe kizingiti
Basi mwanamke akachukua laki tano akanipa ila akanionya kuwa nililosikia pale hata siku moja asije akalisikia sehemu nyingine na wakisikia nitakufa mara moja
Ilipofika saa 5 hivi dreva wao akawafuata na mimi nikachukua tax nikasepa zangu home
Asubuhi nilikuwa na mawazo sana kutokana na vitisho nilivyopewa ,nikataka niwareport polisi ila nikasema moyoni acha tu wakishanipa million 2 zangu zilizobaki naweza kuchukua hatua
Siku moja nipo zangu mjini nilipigiwa sim na mzee (baba yake msela) akanambia niende mahala fulani mtaa Fulani anambie,kwanza nilishangaa amepataje namba yangu ila nikawaza au deal limebuma au kuna nini ngoja nikamsikilizie
Alikuwepo Vila park kwa nje uwanja wa furahisha amepark gari lake pembezoni akanambia ingia ndani ,nikaingia nikakaa na yeye siti ya mbele
Mazungumzo yaakaanza,"Wewe ni rafiki yake sana R na tangu mkiwa sekondari,na pale kwangu nina mwanamke na unamjua vizuri ,hebu nambie nini kinachoendelea kati yako na yeye?
Nikapigwa na butwaa,nikanyamaza kidogo nikamwambia mzee yule mama J alikuwa ananiita maeneo mbalimbali hapa mjini kwa mambo kadha wa kadha ila naendelea kufanya uchunguzi yakikamilika nitakutafuta nikwambie"
Mzee akafyumu "Mambo gani,sema mambo gani hayo,yaani ujue kabisa nina abc zako kuhusu mke wangu,awali nilikuwa namuwazia R lakini nilipoongea na R kwa kirefu alikutaja wewe kuwa unatembea na mama J '"
Nikamwambia mzee siyo kweli,akanizaba makofi mawili akanambia nishuke na akaniambia nisipoachana na mke wake atanifanyia mbaya
Wakati narudi zangu R akanipigia sim kwamba amebanwa na mzee kuwa huenda mimi natembea na mama J ,nilivyoona yamefika shingoni nikaamua kukutaja ila cool down kesho nitakupa laki mbili ukapoze mikikimikiki "Nikamwambia poa
Kesho yake nikatumiwa hiyo laki mbili na ghafla mama yangu ananiita nyumbani ,kufika ananiambia kuna polisi wamekuja kukutafuta wamesema leo ufike kituoni kuna kitu wanataka kujua kutoka kwangu"
Awali mama alikuwa amenigombeza na akiwa anataka kujua nimefanya kosa gani basi nikamwambia hamna kitu
Nikaenda polisi kituo nilichoelekezwa nikaanza kuhojiwa kwa nini natembea na mke wa mtu
Nitaendele baadae.............
Basi polisi mmoja akaanza kunihoji kuwa natembea na mke wa mtu nikamuuliza "mke wa nani afande mbona simjui" Afande akaniambia "Bwana mdogo usijifanye hujui ,unamtesa mzee wa watu na tamaa ya pesa,na inasemekana yule mwanamke anakuhonga ,uongo kweli?" Nikawaza kidogo nikamwambia afande ngoja nikwambie ukweli "Mimi stembei na yule mama, yule mama anatembea na kijana wa yule mzee sijui kama unamfahamu?" Afande akajibu "Hapana simfahamu" nikaendelea kueleza ,"Yule mama si unamuona siyo aged siye mama yake mzazi wa huyo mama bali ,yule mzee walizinguana na mke wake akafukuza " Afande akasema "Mimi siwafahamu familia ya yule mzee ,tofauti na mzee mwenyewe siwafahamu wengine"
Basi mwishowe afande akanionya kuhusu kuwa na ukaribu na huyo mwanamke ila sikumdokezea swala la familia ya mzee kutaka kumfanyia unyama nilipiga kimya nikaondoka
Ilikuwa imefika saa 12 inaelekea saa moja nikiwa natembea barabarani gari haice ikaja ikasimama pembezoni barabarani ,akapiga honi dreva akaniita ,nikajiuliza labda ananifahamu,ile nafika mlangoni kwa dreva kumsikiliza,nikashtukia mlango unafunguliwa upande wa abiria narushwa ndani mlango unafungwa gari linaanza kukimbia
Mle kulikuwa na watu watatu wote sura ngeni,wakaninyang'anya sim yangu ,mle ndani kuna sit moja tu,nikapigwa makofi nikalazwa chini,nikafungwa na kamba mikono ,wakanifunika uso kwa kitambaa,ndo nikaanza kusikia mmoja ananiambia "Yule mwanamke ulishatembea naye mara ngapi na mpaka sasa alishakupa sh ngapi?
Nikawajibu huku nimelazwa kifudifudi kuwa" Mbona hakuna mwanamke ambaye nimewahi kutembea naye" Nikashushiwa fimbo matakoni kama 20 hivi nikiambiwa dogo usiposema unaenda kufa
Nikawambia "Jamani mimi stembei na mwanamke yeyote hapa mjini ,ila kuna mwanamke wa tajiri mmoja anaitwa mama j ndo mme wake ananituhumu "
Ndo mwingine akadakia "Tayari amekiri kuwa anatembea naye kwa hiyo tuache kumpiga huyo dogo"
Wakaacha kunipiga ,gari likakimbia muda mrefu kweli na sijui ninapoenda
Baada ya masaa mengi tu,gari likasimama ,nikasikia kalipe kivukoni",Nikawauliza sasa mnanipeleka wapi jamani ,"mmoja akanambia "Dogo kaa tulia la sivyo utapotezwa"
Nikanyamaza ,gari likazidi kuchanja mbuga sijui tunaenda wapi,nikawaza sasa hapo kuwa lipia kakate ticket kivukoni ni wapi hapa,kwa masaa yote kweli hapa ni Busisi kweli
Gari likaenda masafa kweli kweli ,baadae wakanifungua kama na kitambaa wakaniambia shuka upesi,kufika nje wakasema hilo ni onyo ukirudia hiki utakachokutana nacho hapa ni kidogo
Gari likaondoka wakaniacha ,kuangalia naona mistu tu,giza kali kweli na hata sijui nilipo ni wapi ,
Nikaaa pembezoni mwa njia ndogo sijui hata ni saa ngapi ,nasikia tu kelele za wadudu wapiga kelele vichakani nyakati za usiku
Nikawaza acha nitembee nielekee popote liwalo na liwe kama nitakutana na wanyama wakali humu hamna shida
Kadri nilivyokuwa natembea nikawa nasikia mlio wa mashine kama jenereta kwa mbali,nikawaza ngoja nifuate hiyo mashine ilipo ,mstu mnene kweli kweli
Nikasogea nikakuta majengo mengi na umeme umewaka hilo eneo,nikawaza ngoja niende hapa niombe msaada ,kufika nikaanza kubisha hodi kwa sauti kubwa sana,mlinzi akajitokeza akaniamrisha kaa chini,nikaaa akaniambia tembelea magoti uje mpaka huku muda huo tochi ipo usoni kwangu
Nitaendelea
Mkuu songa mbele, usipoteze muda. Chap kwa harakaInaendelea...... Basi baada ya kuona yule bwana mdogo amenisababishia zengwe, na Mimi nikaona sasa ni bora niwalipue yeye na hawara yake.
Baada ya kupokewa na maswali mazito mazito na wale walinzi wa yale maeneo, maana mwanzoni nilizani yupo mmoja kumbe walikuwa wapo wanne na kumbe siku chache zilizopita eneo hilo walifanyiwa bonge la ambush na majambazi, hivyo walikuwa makini sana na kila kinachokaribia maeneo yao.
Ilikuwa nusura yangu kubwa sana kusogea maeneo hayo huku nikipiga hodi kwa sauti kubwa maana kama ningependa Kama naingia pale nyegezi stand ya mabasi wangenishona shaba wale wazee.
Nashukuru Mungu walinielewa na kuniamini, japokuwa usiku kucha sikulala ilibidi iwe macho macho, mimi siwaamini wao hawaniamini. Kulipokucha Sasa nikapatiwa maelekezo ya jinsi yakuondoka maeneo hayo, kwa sharti la kila nilichokiona yaani mali za pale nifanye Kama sijaona chochote, yaani ni sawa na kuwa kipofu, wewe hauoni lolote lile.
Safari kurudi home ikaanza Sasa, ikumbukwe simu sina, pesa sina muda huo nilikuwa na nguo zangu na kende tu... Itaendelea....
Tusonge mbele Sasa, kichwani nilikuwa na maswali kibao, ikafikia wakati nikajiona mjinga sana, yaani milioni mbili na nusu, mara laki tano na tena laki mbili ya kupozwa baada ya kulambwa makofi na mzee wa mskaji ndio Leo hii zinataka kunitoa roho kweli?? Hapana nikifika tu town nalivuruga chaap..
Aisee nilitembea kinyama, wale mabaunsa walinipeleka mbali sana na viboko kibao nilikula.
WADAU NILIENDELEZE STORY? Nasubili maamuzi yenu hapa.
Ndio utafte vyako hii kurithisha watoto mali ni ujinga watafte zao na hii mentality ndio inawafanya wawe lazy wakuue Ili wapate maliUtajiri mwingine aurithiki wa makafara
We ndugu una vituko. Ila ndo jf huwezipata stress.Kasha potelea kusiko julikana , moja ya mipango yangu ndani ya mwaka huu , ni kwamba nisijisumbue kufuatilia story yoyote ndani humu , ona sasa sijui nini kimenikuta mbaka nikaanza kuifuatilia story hii , natabaki nateska tu na kiu jamaa hata haendelei tujue mwishoe ikawaje .
Tena kwa Link ambayo unalipia kwanza ndio upate muendelezo.Duuu sijui kwanini story tamu, hazinaga mwendolezo, au utasikia tukutane telegram
Dunia imebadilika sana mwanadamu mbinafsi..na asiye aminika umzaniaye kumbe siye..ogopa usaliti na pesaSure trust nobody