Nisamehe tu
Member
- Mar 9, 2019
- 29
- 70
Habari za wakati huu Ndugu,
Natumai mu wazima wa afya ,Nawasalimu katika jina la ( JAMHURI YA MUUNGANO )Wakubwa shikamooni wadogo habari za mida,,pasipo kupoteza muda hii ni historia halisi ya maisha yangu ,lengo ni kumtaka aliye tayari awe Ndugu yangu ila nina uhitaji wa mtu kama baba au mama ,au dada ,nitatoa sababu mbele
Mimi ni kijana wa miaka 23 sasa ,nilizaliwa mkoani kagera na pia katika familia yangu tulizàliwa watoto wawili ,yaani Mimi na Mdogo wangu wa kike ,ni katika familia ya kati maana mama alikuwa na duka na baba alikuwa akimiliki gereji hivyo maisha ya nyumbani hayakuwa ya kukosa mlo ,ni mwaka 2002 mama angu alianza kuumwa sana kwa ugonjwa ambao Mimi sikuujua ilibidi ahamie kwa bibi ambaye ni mama yake.
Utokana na ule udogo nilokuwa nao basi hakika sikujua ni nini hasa ,kilimsumbua mama angu mzazi ,kutokana na udhaifu ule wa mama angu ilinibidi Mimi na Mdogo angu tuamie kwa bibi ili tuwe chini ya malezi ya ujombani ambako mama alikuwa hakiuguzwa kwa mda ule ,japo katika kuishi kwetu ujombani ilikuwa ni Mara chache sana kumuona baba yetu kuja hata kumjulia hali mama yetu ,ndipo mwaka 2004 ,mama angu mzazi alifariki (PUMZIKA KWA AMANI MAMA) basi baada ya msiba kukatokea mgogoro ni wapi sisi tunaenda kulelewa ni ujombani au kwao baba mzazi.
Mgogoro huu ulitokana na Ndugu upande wa baba kutuhitaji sana ila Ndugu upande wa mama hawakuwa tayari kwasababu ya uwepo wa migogoro ya muda mrefu kuhusu masuala ya ushirikina ,ya kuwa upande wa baba yangu ni wachawi hivyo hawataweza kutuacha tuishi ,Hakika kilikuwa kipindi kigumu katika umri wangu Mdogo sana ,mwisho tulisalia upande wa mama yaani ujombani ,ni katika kipindi hicho nilishaanza darasa la kwanza ,nikiwa niko chini ya uangalizi wa bibi yangu.
KUGUNDUA UWEPO WA GONJWA LA UKIMWI KATIKA FAMILIA YANGU.
Niliendelea kusoma katika shule ya msingi iitwayo rwemishasha A ,nikiwa darasa la tano ,nilianza kushuhudia Mdogo wangu akipewa dawa alfajili na jioni japo zilikuwa dawa za hospitalini ila sikujua zilikuwa ni za nini ,dawa zile alikuwa anapimiwa anapewa na bibi zilikuwa ni za kunywa ,nikizikumbuka dawa zile kwa jina la ZINOVIDININE ,MENOVIC na majina mengine ambayo sikuyajua ,Ni wakati mmoja jioni Sana nilimsikia mdogo wangu akilalamika ya kuwa ni lini ataacha kunywa hizo dawa ,nikagundua kuwa basi ni mda atakuwa kaanza kutumia sawa zile ,Bahati mbaya ujio na huduma za baba yetu nyumbani pale vilikuwa adimu sana maana mda mwingi bibi alilalamika sana kuzidiwa na majukumu ya kutulea na baba kutotujulia hali ,Nimeishi na bibi kwa tabu sana maana naye hakuwa na kazi yoyote zaidi ya kutegemea kodi ya vyumba viwili alovyokuwa navyo pale
Hakika tuliishi kwa kubangaiza ila bibi alitukatza kuonesha shida kwa watu ,maana siku zote aliniambia "kidogo nikipata tutakula mwanangu nikikosa mridhike" watoto wake yaani wajomba zangu na mama wadogo zangu hawakuwa na msaada bado kwa bibi .Nikiwa niko darasa la saba ndipo baba yangu alifariki ,tukiwa msibani ndipo nilijua baba yangu alikuwa muathirika wa gonjwa la UKIMWI ,maana watu waliongea wazi na kuongeza pia ni ugonjwa huo huo ulimuuua mama yangu lakini ,wakaeleza kinagaubaga ya kuwa hata Mimi na Mdogo wangu tulizaliwa na ugonjwa huo pia ,nilipoyasikia haya na kuzikumbuka dawa Mdogo wangu anatumia niliumia sana na kujua ni kweli nikawa mwingi wa huzuni ila huzuni ule uliongezwa na fujo zilizotokea siku ya mirathi ya baba kuonekana kila kitu eti ni mali aliziwaachia Ndugu zake kwa maandishi ya kusema hakuwa na imani kama sisi tulikuwa wanae ,hakika niliumia sana na hali ya Mdogo wangu haikuwa sawa maana alisumbuliwa na magonjwa nyemelezi sana.
Baada ya msiba maisha yaliendelea sasa nikiwa yatima kamili ,mwaka 2010 nilifanya mtihani wa darasa la saba ,nikafauli vizuri kwa kuchaguliwa shule ya mkoa ,BUKOBA SECONDARY ,Ni pale nilisoma mpaka kidato cha nne ,japo kutokana na changamoto za kutohudhuria shule Mara kwa Mara kuifuatilia afya ya Mdogo wangu maana mda mwingi alikuwa akilazwa hivyo nilijikuta nakuwa na ufaulu wa wastani sana toka form 1mpaka 4 japo nilitokea kuwa kipenzi cha walimu wa masomo ya sanaa kwa uwezo wangu wa kujieleza na kujenga hoja na ushawishi ,japo walipenda kuniuliza kkwanini Mimi ni mtoro wa Mara kwa Mara sikuwahi waambia maana bibi alinikanya kupenda kueleza mambo binafsi kipindi hicho ,hivyo niliendelea kupewa adhabu kila niwapo mtoro sikujali sana ,
Baada ya matokeo ya form two kutoka niliffanikiwa kufaulu vizuri nikiwa mwanafunzi niliyeongoza kwa masomo ya sanaa katika ufaulu wa juu ,hivyo kutokana na shida nilizokuwa napitia ilinibidi form three niende ambako ni rahisi kwangu kwa hali yangu hivyo rasmi nikasoma mchepuo wa sanaa ,hivy matokeo ya form four nikafanikiwa kuwa na matokeo mazuri ya kuniruhusu kuendelea mbele kwa kiasi Fulani hali ya Mdogo wangu kipindi hiki iliimarika kidogo ,akaweza endelea na masomo yake pia ,nikawa nimechaguliwa kujiunga na kidato cha tano ,shule ya wavulana KAHORORO iliyoko mkoani kagera ,ila usisahau kuwa ninakumbuka msibani watu walisema mimi na Mdogo wangu ni waathirika wa UKIMWI, Hivyo nilikata shauri kuwa naenda kupima nikijikuta ni muathirika basi sitaendelea na mambo ya elimu ,
Baada ya kupima niliambiwa Mimi ni mzima wa afya ,ni hapo nikaanza kumtafuta mtu anidhamini katika masomo yangu hayo maana kwa hali ya bibi asingeweza Mimi kupata hela ya kununua vifaa na ada ,nilienda kwenye mashirika ya kidini mengi sikupata msaada zaidi niliambiwa nisubili ,nikiwa katika kuhangaika huko nikapata mfadhiri ambaye aliamua kunipeleka shule ya binafsi iliyoko dar ea salaam ,huyu aliitwa mchungaji samweli huyu aliniahidi kunisomesha huko dar es sala kwa makubaliano ,nikimaliza itanibidi nisome theology maana alisema ananiona nikiwa mchungaji na kiongozi ,hivyo alifanya maandalizi yote ikiwemo kutumia mda mwingi kumshawishi bibi kukibali Mimi kwenda kusoma huko hatimaye nilisafir na mchungaji mpaka dar ,na tulifikia ubungo riverside ambako alikuwa na wenyeji wake ,baada ya siku kadhaa alinipeleka katika shule iliyoko chini ya kanisa la Lutheran iliyoko kimara -bonyokwa ndipo nikaanza shule yangu ya upili yaani (advance) shule iliitwa Midlands high school.
ITAENDELEA