Jinsi nilivyonusurika kupata virusi vya UKIMWI

Jinsi nilivyonusurika kupata virusi vya UKIMWI

Naona mwandishi anataka atupige anaonekana kweli alisoma mchepuo wa sanaa na anajua kuyaumba maneno mpaka hapo izo comments zake zshamuonesha ni mtu wa aina gani
Kuna watu ni professional matapeli! Halafu kumbukumbu hawana!
 
Pole sana mkuu umepitia mazito lakini huna budi kukaza ukimtegemea mungu
 
Mi pia sijaelewa hapa, ukipewa ada hata asilimia 5 hela ya kujikimu lazima upewe
Chai hiyo mkuu. Kwa mtu anaesoma riwaya utajua tu kua hii ni chai.
Jamaa kasomasoma riwaya kaona atunge kisa chake. Kuna vionjo ambavyo kama msimuliaji ni muhusika hawezi kuviweka.
 
IMG_7157.jpg

Sasa mujomba huo mkopo ulikua wa dipuloma au masitazi
 
Watu kama nyie ndio wanaowafanya watu wawe na mioyo migumu kusaidia watu

You are totally liar!
 
Inaendelea...,..
Niliendelea na masomo yangu Kwa kupambans kimasomo maana chakula na maradhi nikiwa Midlands high school havikuwa shidq hata kidogo
Hatimaye muda ulienda Sana pasipokumuona Yule dada wala mchungaji samwel hata kwa kupata mawasiliano naye
Baadaye muda wa mtihani wa NECTA ,ulifika nikawa nina maandalizi mazuri ya mtihani .
Siku ya kwanza naingia katika mtihani wangu wa kwanza ,ndiyo siku ndoto zangu za kufanikiwa Mara baada ya Mkuu wa shule kunieleza mchungaji kafariki na kafia Ujerumani kwa kansa .
Kumbe muda wote wa ukimya ule ,mfadhiri wangu alikuwa katika hali mbaya kiafya ,nilifanya mtihani nikiwa sina raha ,huku nawaza baada ya hapa nini kinafuata .
Nilimaliza mtihani salama na kwa ile shule mahafali hufanyika baada ya mtihani ,kwañgu sherehe haikuwa na maana ,niliongea na Mkuu wa shule hata anipe namba ya mtu yeyote aliyekuwa karibu na mchungaji kwa hapa dar ila alisema hana .
Nilimuomba mhasibu kiasi cha hela alichokuwa akipolea kutoka kwa mchungaji na ile nyingine niliomwekesha ,alinipa ilikuwa ni jumla ya laki Tisa na elfu ishîrini
(920,000).
Nilitqmani nikitoka shule basi nikamuone yule dada ,alinipeleka msibani ,japo sikuwa napakumbuka vizuri upanga ,nilitoka shule kwa huzuni baada ya kuwaaga walimu wangu ,waliumia Mimi kutofanya sherhe ila waliujua wakati niliokuwa napitia ,walinichangia kiasi cha laki na elfu kumi na moja (110,000,) Kama nauli nifike kagera nyumbani.
Niliondoka Shule ,sasa rasmi kwenda upanga ili nikamuone yule dada.
Nilihangaika sana kwa kuuliza kwa watu ni vipi nifike upanga ,hatimaye nilifika ila kila nilipoulozia kwa watu kuhusu Yule dada kwa pale alikuwa akiishi walisema ana miaka mingi aliondoka baada ya kufiwa na mmewe.
Sikuwa na ziada ila kurudi ubungo nipate tiketi ya kwenda bukoba nyumbani ,nilipata tiketi ikabidi nilale stendi ,kwenye magari na asubuhi nilikuwa njiañi kwenda kumuona bibi yangu kipenzi.
Siku ya pili baada ya kuianza safari ,tayari nilikuwa nyumbani muda wa saa saba .
Naumizwa na taarifa ya majirani ya kuwa Bibi yuko jela sasa ni miezi kadhaa kwa kesi ya kuua bila kukusudia ,bibi alileteewa mjukuu ,mtoto wa mjomba ila mtoto alikuwa mtukutu hivyo bibi katika kumuadhibu basi mtoto alifariki.
Yakawa maisha mapya ya upweke pale nyumbani.
Sikuacha kuenda kumuona bibi gereza lililoko bukoba mjini japo baadaye alihamishiwa gereza linaitwa KITENGULE palepale mkoa.
Siku moja ilibidi nikamuulize yule mchungaji wa.kanisani kuhusu habari za mchungaji Samwel ila alisema hana taarifa naye zaidi ya kifo chake .
Niliamua kuwa najichanganya na vijana wenzangu wanaonunua dagaa kutoka visiwa vya kerebe na goziba ,kwakuwa nilikuwa na mtaji nilifanya ile biashara kwa weledi mpaka wenzangu wakawa hawanipendi japo walisahau kuwa Mimi nilikuwa na mtaji mzuri kuliko wao.
Kwa kipindi kifupi niliweza jengea makaburi ya wapendwa wangu kwa kisasa lakini pia nikanunua pikipiki kwa mtu kwa laki Tisa .
Hakika biashara ilikubali japo changamoto ilikuwa ni wamama na wadada wa visiwani kule nilikokuwa natoa dagaa kunitaka japo niliwaogopa sana kwa kukumbuka jins UKIMWI ulivyowachukua wapendwa wangu.
Matokeo yanatoka nina division 2 ,hivyo naweza kwenda chuo ,nilifurahi sana ,japo pia biashara katika kipindi huko iliyumba kidogo ,hivyo nikawa nimeacha kwanza ,nikajifunza pikipiki kwahiyo huo mda nikawa ni bodaboda wa kutegeshea maana sikuwa na leseni ,kwa upande wa hii biashara niliambulia kuwa napata hela ya kula tu na mafuta ila hakuna malengo .
Nilifanya utaratibu wote wa kwenda chuo na kuomba mkopo nikawa nimemaliza ,sasa nasubili kuchaguliwa na mkopo niende.
Siku moja nikiwa nyumbani ,alikuja bodaboda mwenzangu akaomba nimpe pikipiki yangu afanyie deiwaka (DAY WORK) kwa masaa mawili ili alafu atanipa elfu tano ,nilikubali maan mda huo nilikuwa nafanya usafi ndani ,kumbe alikuwa anaelekea mpaka na UGANDA ,mtukula kuchukua MIRUNGI (dawa za kulevya ) baada ya masaa kadha kupita sikumuona ikabidi niende kijiweni kumuulizia ,ni hapo nikaambiwa alikimbizwa na Polisi akiwa anatoka mutukula hivyo kapata ajali na kafariki na pikipiki haieleweki tena .
Huo ukawa mwisho wa Mimi kuwa na pikipiki ,akiba nilikuwa na laki sita na nusu tu ,hivyo nikasema niitunze mpaka mda wa kwenda chuo .
Muda ulifika nikapangiwa vyuo viwili UDSM-DUCE kusomea ualimu au UDOM -Kusomea sosholoji ila Mimi nilipenda ualimu ,na mkopo nikapata nusu ya ada bila hela ya kujikimu ,bila kusahau Mimi sikupata ile chance ya kwenda jeshini yaani kwa mujibu ,japo nilitamani sana nipate huko mazima.
Rasmi niliripoti UDSM -DUCE ,nikafanya tartbu zote nikaanza chuo ,nikiwa naishi hosteli ,hiyo ni baada ya kuna dar ,nilijitaidi kuwaaga wajomba japo hakuna hata mmoja alipenda Mimi kuendelea .
Kama mjuavyo maisha ya chuo bila hela ya kujikimu ni shida kwa sisi watto wa mkulima ,hivyo baada ya malipo yote ya pale DUCE na hela ya safari na nusu ada na hosteli ,ni laki mbili tu ,ilikuwa mfukoni ,hiyo nile mpaka mwaka wa kwanza wote uishe ,ni kitu ambacho nilikuwa kigumu.
Niliamua kuwa nasoma kwa bidii huku nikifuatilia hata Kazi yoyote ya muda ila sikupata ,japo kutokana na maisha yangu ya kujichanganya basi nikajichanganya na vijana wa kike ili nipate hata fursa ,ila haikuwa rahisi maana wengi walinigwaya kwa kuwa nilikuwa mwanachuo japo pia walinihisi labda nawafuatlia maana wengi walikuwa wanavuta bangi na kujidunga sindano ,haikuwa rahis kuwazoea ila niliweza.
Mwisho sikupata chochote kwao ila kupitia wao basi mitaani keko yote Mimi sikuwa mgeni tena .
Ni huko baada ya wiki nne najuana na kijana muuza nyama kwa kutembeza ,nilimuuliza mengi kuhusu ile biashara akanielekeza ,mfukoni mda huo nina laki na ishirini tu.
Masomo yaliendelea na hiyo biashara ilitakiwa hela zaidi ya hiyo ila sikuwa na jinsi ila kubana mpaka itoshe .
Rasmi mimi chuo nahudhuria semina tu ,pasipo vipindi ili asubuhi niungane na jamaa wa nyama kwenda vingunguti tununue nyama na pia tuitengeneze na baadaye tuingie mtaani kuzungusha.
Yalikuwa ni maamuzi magumu maana mda wangu wa semina ilibidi niwe naingia chuo na jiko langu la chuma ,nihudhurie semina alafu badae niendelee na biashara yangu ,nilichekwa sana na wenzangu na pia walinzi ,getini ilinipa shida sana kila siku kuwashawishi. Baadae walinizoea.
Niliweza kuwa napata uhakika wa hela ya kula Milo mitatu ,kulipa hosteli na kutoa michango ya kutype Kazi za semina japo pia hela ya ada iloyokuwa imebaki niliweza kuwa nailipa vyema bila kusahau na hela kidogo kuwapoza wale watu niliokuwa napangwa nao ili wanivumilie utoro wangu ,nilienda hivyo mpaka mwaka wa tatu ,muhula wa kwanza ,pasipo kupata shida kwa hivyo japo nilihangaika sana na kuwasumbua jamaa zangu kunielekeza waliyosoma .
Mwaka wa kwanza na wa pili nilibahatika kuwa na GPA 3.4 ,ninamshukuru sana Mungu maana niliipata hii GPA kwa tabu san ,pasipo kusahau ya kuwa Mimi ni nwanafunzi niliyekuwa nimebobea katika masomo ya LINGUISTIC AND LITERATURE (KIINGEREZA NA FASIHI) .
Niliendelea na utaratibu huo mpaka mwanzoni kwa semester ya kwanza ,ndipo katika kozi moja ya lugha nilikuwa nimebahatika kufundishwa na mwalimu aliyekuwa ni wa advance sasa amekuwa mhadhiri ,katika makundi ya Kazi zake za semina ,kundi langu liliripoti utoto wangu katika ktayarisha hizo Kazi ,aliniita baada ya kujua ni Mimi hakutaka kuniuliza sababu us utoto ila alisema jitaidi hata Mara moja moja uhudhurie.
Hivyo ikabidi niwe najitaidi
Mimi kama kawaida likizo nilikuwa naomba nabaki hosteli ila kwa kulipa kawaida .
Tukiwa likizo ndiyo nije kuingia semister ya mwisho ya mwaka wa tatu ,Ndiyo gonjwa la CORONA likaibuka ,hivyo hata biashara yangu ikadorora maana nilikuwa napitisha sana maofisini na sehemu za mikusanyiko ila sikufanikiwa tena kama mwanzo. Hivyo nikawa napambana pasipokujua nitalipa nini tukifungua chuo .
Baadae ndiyo vyuo vikafungwa kwa mda ni hapo nikajipa moyo nitapambana .
Hela ya hosteli ikawa imeisha nikaamua kitafuta Kazi ya ulinzi ,Mungu akanisaidia nikapata katika kampuni ya GIRAFE kwa malipo ya laki moja na arobaini ,nikawa nawaza mpaka wakijasema turudi chuo nitakuwa na hela ya kuongezea ada na ya kujikimu nimalizie mda wangu .
Ilikuwa Kazi ngumu kwangu ila nilijikaza maana sikuwa na sehemu ya kulala zaidi ya lindoni kwangu .
Mwezi wa kwanza uliisha na mshahara hakuna wakidai mteja tunayemlindia hajalipa hela hivyo tuwe na subira ,Ndugu Mimi nimelinda 0pale kwenye kiwanda cha PANASONIC ,kilicho karibu na QUALITY CENTRE ,niliendea kuwa mvumilivu ,baada ya nusu mwezi mwingine ,tulitakiwa kurudi chuo ,hivyo nikaamua kwenda ofisini kuwaelekeza pia niombe hela yangu ili nikajichangechange nimalize chuo ila ajabu sikupewa hiyo hela wakadai hawana hela nisubili mwisho wa mwezi .
Chuo sikuweza kwenda nilisubili nipate hela nilipe hiyo nusu ada ili niendelee ,baada ya mwezi nilirudi ofisini pale GIRAFFE ila muda huu niliambiwa hela bado na hawajui mteja atalipa lini .
Basi baada ya hapo nilienda chuo nikauliza taratibu za kuahirisha au kupostpone mwaka nilipewa nikaandika hiyo barua baada ya wiki tatu nikajibiwa kuwa nimekubaliwa ..
Muda wote huo nikiwa naishi kwa jamaa yangu wa nyama ,hali yake ya uchumi ikiwa mbaya kama yangu pia .
Mwez wa Tisa nilioanza nao chuo walimaliza ,Mimi niko bado sijapata ada nimetafuta sana Kazi ila sijapata bado naishi kwa kuungaunga ,labda Mara chache nilipata daywaka ya ukonda ,hapo kidogo nakuwa na uhakika wa hata wiki kula na kuchangia chochote kwa rafiki yangu ninapoishi. Nipo keko -magurumbasi nyuma ya gereza la keko .
Ndugu awali nilisema nahitaji mmoja atakayenikubali awe kama baba yangu nikiwa ni wa kiume ,au mama yangu nikiwa ni wa like au Dada yangu ,Yote ni katika kumbukizi za wapendwa wa familia yangu .
Ila mwisho ndugu zanguni Mimi naomba aliyetayari anisaidie mtaji kwa makubaliano ,nitajituma nirudishe kwa wakati ,hata laki mbili yanitosha ,japo akitokea mtu anatamani kunisaidia nimalizie masomo yangu nitashukuru sana pia ila mwisho kabisa hapo kwako kama yote ni magumu basi nipe Kazi nakuahidi kuifanya kwa weledi sana .
NISAMEHENI KWA KUWACHOSHA NA MUANDIKO MBAYA NI SIMU ,TUSAIDIANE PASIPO KUSAHAU KUWA MIMI NIMENUSURIKA UKIMWI WA KUZALIWA NAO ,HIVYO MUNGU ANA KUSUDI NA MIMI
WHAT GOES AROUND COMES AROUND.
Nashukuru sana ,naipenda jamii forum

Njoo dm
 
Mbona coment za waja zinanishtua[emoji15][emoji15] nilitaka kumsaidia ila mmeniogopesha

Kuna kijana alikuja na kisa kama hiki hapa Jf nikamchukua nakaa nae he is the best[emoji122] nilitaka nimchukue na huyu wakae wote nae kama atakuwa kama mwenzake nimsaidie pia ila coment zenu zimeniogopesha
 
Back
Top Bottom