Jinsi nilivyonyanyuka tena baada ya kuanguka kimaisha

Mie watu wanao toa stori za mafanikio ya kilimo na washangaa jambo moja wanafanikiwa kupitia kilimo tena hapo wanakikimbia haraka kufungua biashara mjini badala yakuendeleza hicho kilima awe kwenye large scale production, kwanini wanakikimbia?
Mkuu ukirudia kulima inakukata vibaya. Angalia hii trend
Mwaka 2018 viazi mviringo viliuzwa junia mpaka 70000 mwaka uliofuata junia lilikuwa 20000 tena kwa kubembeleza dalali. Mwaka 2020 junia lilicheza 45000 mpaka 30000 .
Mwaka huuu 18000. - 25000.
Unaiona teend hio. Unaweza tajirika vilevile unaweza filisika ndani ya mwaka mmoja.
 
Mnaosema kwanini nimerudi town nimerudi mjini kusimamisha biashara yangu inendelee alafu pia kilimo ukitaka utoboe usilime kwa mihemko na uwe na biashara nyingine pembeni,
Kilimo kinahitaji timing kali sana ya kujua ulime nn kwa wakati gani ili unapoingia sokoni uuze kwa bei yenye manufaa ukitumia mihemko utarudi mikono kichwani alafu unapaswa uwepo asilimia 100 shamba so mm nimerudi town biashara iamke tena wakati nacheza na nyakati by January nitarudi tena shamba bila shaka kilimo ndio kitu nakifahamu kuliko kingine chochote nitafanya na nitafanya tena maji na ardhi ninavyo pia kupitia wazee wangu
 
Mkuu nikupe siri usilime mazao ya msimu na kama utalazimika kufanya hivyo nenda kinyume chake wenzio wakiwa wanavuna ww panda wakiwa wanapanda ww vuna na lima kwa rotation mzee wangu hua nalimaga vitunguu mwaka mzima kwa rotation yeye hua bei ikishuka kabisa anaweka kitalu hajali bei anauza kenya na ikishuka ikipanda yeye yumo hii ikikataa ingine italeta inafidia nyingine faida so kilimo ni sayansi ya kucheza na nyakati mkuu
 
Mkuu sio wa kishua wala nn wazee wangu wafanyakazi wa kawaida tu serikalini ni walishtukaga mapema wakawekeza kwenye kilimo wakati huo watu wanaona kilimo utumwa
Kunyanyuka kwako naona wazee wamehusika.
 
Viazi huwa havilimwi kwa msimu, ni mwaka mzima. Kwa ishu ya viazi ni soko ndio linaloamua sio msimu.
 
Mkuu kumbe hawa viumbe ni hatari sana eti,
 
Heka ya maharage ya njano inatoa gunia ngap na mbegu n kias gan kwa heka

Jana Kuna shamba nilienda kuona hvyo jumatatu nataka niamue trekta uende kulima Mana vuli unaanza sio muda kutoka sasa
 
Heka ya maharage ya njano inatoa gunia ngap na mbegu n kias gan kwa heka

Jana Kuna shamba nilienda kuona hvyo jumatatu nataka niamue trekta uende kulima Mana vuli unaanza sio muda kutoka sasa
Heka ikihudumiwa vizuri inatoa gunia 5 net na mbegu mm hua sibananishi natumia sado 8 tu wengine wanatumia hadi sado 12
 
Heka ikihudumiwa vizuri inatoa gunia 5 net na mbegu mm hua sibananishi natumia sado 8 tu wengine wanatumia hadi sado 12
Mbona inatoa gunia chache aisee huko n wapi unalimia.

Huku wadau wanasema huwa wanaotesha kwa kutupa yan wakati shamba linavurugwa nyuma mtu wa mbegu anapita anafanya yake na mavuno wanasema heka inatoa kuanzia gunia nane sasa ndo Mana nataka kujua labda we unalimia wap niweze kuamua kabla ya kulima shamba
 

Naona unawinda kwa kasi ya 4G location ya mtoa mada [emoji28]
 
Mzee wako amekubeba sana yeye ndo wa kupewa pongez sio wewe
 
Uko mkoa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…